Ufahamu Ugaidi na Sheria ya kuzuia Ugaidi Tanzania (POTA, 2002)

Dec 23, 2016
31
69
Sheria hii ni miongoni mwa sheria za kipekee, ambayo vifungu vyake vimepewa nguvu dhidi ya sheria nyingine pale ambapo mgongano utatokea (kikawaida nguvu hii hupewa katiba ya nchi/nguvu yakitatiba pekee).

Baada ya vita baridi ya dunia kuisha miaka ya 1990s, dunia ilianza kushuhudia vita nyingine ijulikanayo kama vita dhidi ya ugaidi, “War on Terror”.

Vita hii imeanza rasmi mwaka 2001, baada ya kauli ya aliekua raisi wa marekani George W. Bush kufuatia shambulio la September 11.

Baada ya shambulio hili marekani ilianza kusambaza kampeni ya vita dhidi ya ugaidi duniani kote.

Nukuu ya Bush

*Our war on terror begins with al-Qaida, but it does not end there. It will not end until every terrorist group of global reach has been found, stopped and defeated.*


Eneo moja wapo katika kampeni iliyoanzishwa na marekani lilikua ni utungaji wa sheria maalumu za kudhibiti ugaidi katika mataifa duniani kote.

Tanzania haikua nyuma, hinvyo mwaka 2002 bunge lilitunga sheria yakudhibiti na kupambana na Ugaidi ijulikanayo kama PREVENTION OF TERRORISM ACT, au kwa kifupi POTA chini ya uangalizi na usaidizi wa Marekani.


Na;
Mfaume Hassani.


Ugaidi ninini?

Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii yakimataifa na vyombo vyake.
Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.

Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.

Ugaidi una historia ya mbali kuanzia miaka ya 1837 lakini umeongezeka tatika karne ya 20 na 21. Hii imepelekea dunia kwenda katika vita mpya ya kuzuia na kudhibiti ugaidi.

Ugaidi una madhara makubwa kwa watu na vitu na ni tishio kubwa la usalama katika dunia ya sasa. Maelfu ya vifo katika karne hii ya 21 yanatokana na ugaidi, ambapo magaidi wana lenga raia wasio na hatia.

Tanzania ilikubwa na tukio lakigaidi kwaka 1998 lililoacha vifo vya baadhi ya watu. Tukio hili lilielekezwa katika ubalozi wa marekani hapa nchini. Wakati huohuo magaidi walishambulia ubalozi wa marekani jijini Nairobi, Kenya.


POTA
Sheria hii imejinaisha ugaidi, katika ngazi tofauti. Kuanzia kutenda au kujihusisha na vitenndo vya kigaidi, ikiwemo kusaidia magaidi, kushauri, kudhamini fedha au vitu vitakavyopelekea ugaidi kutendeka.


Nguvu ya kutangaza mtu, jumuiya au kikundi cha watu kua chakigaidi.

Sheria imempa mamlaka waziri wa mambo ya ndani kumtangaza mtu au kikundi au jumuiya yoyote kua yakigaidi baada yakujiridhisha kua mtu huyo au kikundi hicho kinajihusisha na ugaidi au mambo yanayoweza kutafsiriwa kua ni yakigaidi kuilinganga na vifungu vya sheria. Kifungu No. 12.


Nguvu ya kukamata bila kibali cha mahakama.

Kifungu No. 28 cha sheria hii kimetoa mamlaka kwa afisa polisi, au uhamiaji kukamata bila ruhusa/kibali cha mahakama gaidi au mtu atakaemuhisi kua ni gaidi au anashirikiana na magaidi.


Afisa usalama wa taifa.

Halkadhalika, kifungu hiki (No. 28) kimetoa mamlaka na nguvu kwa afisa usalama wa taifa kukamata mtu ambae ni gaidi au atamuhisi kua ni gaidi.
Mamlaka haya ni yakipekee kwakua sheria ya usalama wa taifa *TISS Act, 1996* hairuhusu maafisa usalama kukamata wahalifu. TISS wana mamlaka pekee yakukusanya taarifa za kiusalama, kuchambua, kutafsiri nakuwasilisha ripoti kwa raisi au waziri mwenye dhamana.


Jukumu la kutoa taarifa za ugaidi/magaidi.


Kifungu No.40 cha sheria hii kinatoa jukumu la lazima kwa raia au mtu yeyote mwenye taarifa zinazohusu mtu au tukio lakigaidi kuzifikisha polisi ama kwa mrakibu msaidizi wa polisi au mkuu wakituo cha polisi. Mtoa taarifa pia amepewa kinga yakuto kufunguliwa mashtaka yoyote juu yataarifa alioitoa akiwa anaamini ni yakweli.
Adhabu yakutokutoa taarifa kama kifungu hiki kinavyo hitaji ni kifungo kisicho pungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano.



Baadhi ya makosa na adhabu zake.

1. Kutoa au kukusanya fedha kwa lengo la kufanikisha ugaidi. (kifungo miaka 15-20).

2. Kutoa au kukusanya mali, au kumkaribisha mtu atoe mali au kuweka mazingira ya uwepo wa mali au fedha na huduma zifananazo ili kufanikisha. (kifungo miaka 20-25).

3. Kuwapa silaha magaidi. (miaka 20-30)

4. Kushawishi au kusaidia katika kushawishi watu kujiunga na makundi ya kigaidi. (kifungo miaka 15-20).

5. Kutumia mali, au kumiliki mali kwa njia yoyote ambayo inakusudio lakusaidia kutekeleza ugaidi (kifungo miaka 15-20).

6. Kujimilikisha mali za magaidi kwa lengo la kuficha umiliki wa wahusika ili kuwasaidia kutojulikana, au kuhamisha au kwa nyovyote. (kifungo miaka 15-20).

7. Kuishi na gaidi au kumficha gaidi ili asikamatwe na mamlaka husika. (kifungo miaka 18-30).

8. Kua mfuasi wa kundi la kigaidi. (kifungo kisichopungua miaka 8).

9. Kupanga kikao, au kusaidia kwa vyovyote kikao cha magaidi. (miaka 10-15).

10. Kupanga njama, kusaidia, kujaribu, kuficha, kushauri katika utekelezaji wa ugaidi.

NOTA BENE
There is no universally acceptable definition of terrorism. The same differ according to various jurisdiction.

They say

"One man's terrorist is another man's freedom fighter."

mfaumehassan@gmail.com
14/09/2019

The Eye That Never Sleeps.
 
Wafuasi wa gaidi Mbowe wasome hii, soon tunamsahau mwamba huku uraiani,naimani Sheria itatenda haki dhidi ya huyu mwamba wa ugaidi.

Eee Allah wajarie wepesi mahakimu wetu.
 
Wafuasi wa gaidi Mbowe wasome hii, soon tunamsahau mwamba huku uraiani,naimani Sheria itatenda haki dhidi ya huyu mwamba wa ugaidi.

Eee Allah wajarie wepesi mahakimu wetu.
Wewe poyoya acha roho mbaya.Maisha yenyewe yako wapi Kwani??.
 
Back
Top Bottom