Ufafanuzi zaidi kuhusu udahili wa elimu ya juu (vyuo vikuu) 2017/2018

ukiona chuo na kozi haipo katika tcu guide book, ujue haijasajiliwa hivyo hata ukiukuta katika chuo wameiweka iogope na ikwepe kama ukoma
 
ukiona chuo na kozi haipo katika tcu guide book, ujue haijasajiliwa hivyo hata ukiukuta katika chuo wameiweka iogope na ikwepe kama ukoma
TCU imetoa kitu ambacho hakija kamilika. Hakina hata utagulizi na maelezo yeyote.
 
ukiona chuo na kozi haipo katika tcu guide book, ujue haijasajiliwa hivyo hata ukiukuta katika chuo wameiweka iogope na ikwepe kama ukoma

Kwa akili yako,Doctor of Medicine za CUHAS na KCMC hazijasajiliwa?Kwa hiyo waikwepe kama ukoma ehh?
 
Kwa akili yako,Doctor of Medicine za CUHAS na KCMC hazijasajiliwa?Kwa hiyo waikwepe kama ukoma ehh?
TCU waje tena na maelezo ya ile orodha walio toa na ukamilifu wake ili waombaji wasivurugwe kwa kuwa na taarifa tofauti kati ya list ya TCU na website za vyuo.
 
Kuna baadhi ya vyuo havipo TCU guide book, je ndiyo vimefutwa au? Telimishane.
1.eckernforde Univ Tanga etc
2. Tumaini Unive--kcmc (MD programme) hakuna
3. etc

Tatizo ni nini?
Mkuu tafuta vyuo vya maana sasa eckenford nacho ni chuo kikuu?
 
Imekamilika hivyo na hakuna lazaidi ya hapo!

unataka nini ili ikamilike
Lakini mimi pia sikuona chuo cha ST. FRANCIS cha IFAKARA ndani ya hii guideline ya TCU. Ila ukiingia kwenye website ya St. Francis wanaonesha wanadahili mwaka huu. Kutakuwa na mapungufu kwa hii guideline
 
xBn9GkNXDRXhKM5T-Od-VHQVR6z2FHmypZ-hu8jnMQHP6xzEUkfg-DW9BZLqJ7avAk6-uM8S0_QB8HWcWRreP4L-wAypzKgYUTNixbNOMAm2EgRRaPEzGU6J_8sRDHZPw7ssFPBkg575vqtm2db5pJV5W01rdlPl4OsGqqXn5jUOpNkUXbGF_5ziq7gLUK8cgvtVGxwItQ=w1200-h630-p-k-no-nu

1.Kwa waliomaliza Cheti na Diploma wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zao online NACTE ili zihakikiwe(verification) kupitia Link ambayo imetolewa kupitia mtandao wa *NACTE* baada ya uhakiki huo utapewa *code namba* kulingana na ufaulu wako ambayo ndio itakuwezesha kufanya *UDAHILI* kwenye chuo kikuu unachokipenda,kumbuka Hakuna chuo kitapokea maombi ya udahili bila code namba hiyo,zoezi limeshaanza na linaendelea Hadi sasa. [SOMA ZAIDI..https://goo.gl/C5owo7]

VIWANGO VYA UFAULU KWA WENYE DIPLOMA NI GPA 3.0 ILI UWEZE KWENDA CHUO KIKUU
2.Kwa walimaliza Kidato cha Sita maombi UDAHILI kwa mwaka huu Unafanyika moja Kwa moja kupitia chuo na sio *TCU* kama miaka iliyopita, UDAHILI utaanza *tarehe 22.07.2017* hadi *30.08.2017*,hivyo mwanafunzi atafanya maombi ya kusoma shahada kupitia chuo anachokipenda, vyuo vikuu vyote vimeshapewa maelekezo kupitia maafisa UDAHILI (admission officers) kupitia mafunzo maalum yaliyoisha tarehe 15.07.2017, [SOMA ZAIDI...https://goo.gl/tz379E]

VIWANGO VYA UFAULU NI 4.0 ILI UWEZE KWENDA CHUO KIKUU
Kitu cha muhimu ni kwamba mwanafunzi hatolazimika kusafiri kwenda chuo husika kila kitu kitafanyika kupitia mtandaoni (Online), Anachotakiwa kufanya mwanafunzi ataingia kwenye *Website* ya chuo kwa kufuata *link hii*[https://goo.gl/3McXhj] ya udahili na kufata taratibu ambazo zimewekwa.

Mwanafunzi atajaza taarifa chache Sana ,maana chuo kinamuingiliano Wa *mfumo data* na NECTA na NACTE, mwanafunzi atajaza taarifa muhimu tu ikiwa ni Pamoja na majina, Kozi unazoomba hata kama utajaza kozi tano, index namba zote Hata kama uliwahi ku Reseat zaidi ya mara moja na email ya wezekana ukatakiwa kuweka na namba zako za simu inategemea chuo husika kimeweka vipengele gani ili kurahisisha zoezi zima la UDAHILI.
Muda uliotengwa ukiisha baada ya tarehe *30.08.2017* hakutakuwa na nyongeza ya muda .

Mwanafunzi anaruhusiwa kuomba chuo zaidi ya kimoja anavyopenda yeye.
Baada ya hapo majina yatatolewa kwa kila chuo na mwanafunzi aliyedahiliwa chuo zaidi ya kimoja atatakiwa kuthibitisha ni chuo kipi atakachoripoti, kila chuo kimejipanga katika hilo la mwanafunzi kuthibitisha kuwa ataripoti bila mwanafunzi kuhangaika kusafiri kwenda kuthibitisha kwenye chuo anachopenda kusoma. Vyuo vingine vitatumia mfumo wa sms, au online confirmation na mwanafunzi akishathibitisha kushiriki chuo kimoja jina lake litaondolewa kwenye orodha ya vyuo vingine alivyojitokeza kwenye udahili zaidi ya chuo kimoja. UMAKINI UNATAKIWA SANA HAPA KWA WANAFUNZI HUSIKA ILI USIJECHAGUA CHUO AMBACHO HUKIPENDI

Unapo fanya udahili zingatia vigezo vya kozi unazoomba ili kuepuka kukosa chuo sababu ya kozi ulizoomba haziendani na sifa ulizonazo mf. mtu unaomba Kozi ya Udaktari wakati umesoma masomo ya biashara kitu ambacho haviendani.
NB: Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia
*www.nacte.go.tz kisha Bofya Award verification*
*www.tcu.go.tz kisha Bofya Admission procedures for 2017/18* uzisome kwa umakini na kuzielewa kuepuka kusumbuka dirisha likifunguliwa.
Tufuatilie katika Page yetu kwa Msaada zaidi
#School_Base_Online
POWERED BY [HASHTAG]#SBO[/HASHTAG]
Samahani mkuu,naomba msaada kwa hili suala.
Nina kijana hapa,amemaliza kidato cha sita mwaka huu.amefaulu kwa kiwango cha daraja la 3 point 13 (division 3,point13).alama zake ni kama zifuatazo:-
General study-S
History-E
Kiswahili-C
English language-E
Anataka kuchukua degree ya sheria,je akiomba chuo cha mzumbe,watampokea?,na kama awatompokea,chuo gani watampokea kwa ufaulu huo?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
This is amaizing...
Since that day official announcement was announced that every higher level education istitution will conduct selection by themselves until now not yet put any advancement in their online system!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu,naomba msaada kwa hili suala.
Nina kijana hapa,amemaliza kidato cha sita mwaka huu.amefaulu kwa kiwango cha daraja la 3 point 13 (division 3,point13).alama zake ni kama zifuatazo:-
General study-S
History-E
Kiswahili-C
English language-E
Anataka kuchukua degree ya sheria,je akiomba chuo cha mzumbe,watampokea?,na kama awatompokea,chuo gani watampokea kwa ufaulu huo?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo hawezi kwenda chuo kikuu maana hana principle ambazo angalau D mbili ,na hapo anayo moja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu,naomba msaada kwa hili suala.
Nina kijana hapa,amemaliza kidato cha sita mwaka huu.amefaulu kwa kiwango cha daraja la 3 point 13 (division 3,point13).alama zake ni kama zifuatazo:-
General study-S
History-E
Kiswahili-C
English language-E
Anataka kuchukua degree ya sheria,je akiomba chuo cha mzumbe,watampokea?,na kama awatompokea,chuo gani watampokea kwa ufaulu huo?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ana C na E jumla point 4 kutoka masomo 2. Hivyo anaweza kuomba kudahiliwa chuo. Ana jumla ya point 5. Kuhusu chuo gani kinaweza kumpokea, wenye uzoefu na degree za sheria watatujuza lakini nina wasi wasi kama Mzumbe wanaweza kumpokea. Itabidi asiweke mayai yake kwenye kapu moja.
 
Back
Top Bottom