Ufafanuzi zaidi kuhusu udahili wa elimu ya juu (vyuo vikuu) 2017/2018

Apr 18, 2012
95
213
xBn9GkNXDRXhKM5T-Od-VHQVR6z2FHmypZ-hu8jnMQHP6xzEUkfg-DW9BZLqJ7avAk6-uM8S0_QB8HWcWRreP4L-wAypzKgYUTNixbNOMAm2EgRRaPEzGU6J_8sRDHZPw7ssFPBkg575vqtm2db5pJV5W01rdlPl4OsGqqXn5jUOpNkUXbGF_5ziq7gLUK8cgvtVGxwItQ=w1200-h630-p-k-no-nu

1.Kwa waliomaliza Cheti na Diploma wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zao online NACTE ili zihakikiwe(verification) kupitia Link ambayo imetolewa kupitia mtandao wa *NACTE* baada ya uhakiki huo utapewa *code namba* kulingana na ufaulu wako ambayo ndio itakuwezesha kufanya *UDAHILI* kwenye chuo kikuu unachokipenda,kumbuka Hakuna chuo kitapokea maombi ya udahili bila code namba hiyo,zoezi limeshaanza na linaendelea Hadi sasa.

VIWANGO VYA UFAULU KWA WENYE DIPLOMA NI GPA 3.0 ILI UWEZE KWENDA CHUO KIKUU
2.Kwa walimaliza Kidato cha Sita maombi UDAHILI kwa mwaka huu Unafanyika moja Kwa moja kupitia chuo na sio *TCU* kama miaka iliyopita, UDAHILI utaanza *tarehe 22.07.2017* hadi *30.08.2017*,hivyo mwanafunzi atafanya maombi ya kusoma shahada kupitia chuo anachokipenda, vyuo vikuu vyote vimeshapewa maelekezo kupitia maafisa UDAHILI (admission officers) kupitia mafunzo maalum yaliyoisha tarehe 15.07.2017,

VIWANGO VYA UFAULU NI 4.0 ILI UWEZE KWENDA CHUO KIKUU
Kitu cha muhimu ni kwamba mwanafunzi hatolazimika kusafiri kwenda chuo husika kila kitu kitafanyika kupitia mtandaoni (Online), Anachotakiwa kufanya mwanafunzi ataingia kwenye

Mwanafunzi atajaza taarifa chache Sana ,maana chuo kinamuingiliano Wa *mfumo data* na NECTA na NACTE, mwanafunzi atajaza taarifa muhimu tu ikiwa ni Pamoja na majina, Kozi unazoomba hata kama utajaza kozi tano, index namba zote Hata kama uliwahi ku Reseat zaidi ya mara moja na email ya wezekana ukatakiwa kuweka na namba zako za simu inategemea chuo husika kimeweka vipengele gani ili kurahisisha zoezi zima la UDAHILI.
Muda uliotengwa ukiisha baada ya tarehe *30.08.2017* hakutakuwa na nyongeza ya muda .

Mwanafunzi anaruhusiwa kuomba chuo zaidi ya kimoja anavyopenda yeye.
Baada ya hapo majina yatatolewa kwa kila chuo na mwanafunzi aliyedahiliwa chuo zaidi ya kimoja atatakiwa kuthibitisha ni chuo kipi atakachoripoti, kila chuo kimejipanga katika hilo la mwanafunzi kuthibitisha kuwa ataripoti bila mwanafunzi kuhangaika kusafiri kwenda kuthibitisha kwenye chuo anachopenda kusoma. Vyuo vingine vitatumia mfumo wa sms, au online confirmation na mwanafunzi akishathibitisha kushiriki chuo kimoja jina lake litaondolewa kwenye orodha ya vyuo vingine alivyojitokeza kwenye udahili zaidi ya chuo kimoja. UMAKINI UNATAKIWA SANA HAPA KWA WANAFUNZI HUSIKA ILI USIJECHAGUA CHUO AMBACHO HUKIPENDI

Unapo fanya udahili zingatia vigezo vya kozi unazoomba ili kuepuka kukosa chuo sababu ya kozi ulizoomba haziendani na sifa ulizonazo mf. mtu unaomba Kozi ya Udaktari wakati umesoma masomo ya biashara kitu ambacho haviendani.

NB: Maelekezo zaidi yanapatikana kupitia
*www.nacte.go.tz kisha Bofya Award verification*
*www.tcu.go.tz kisha Bofya Admission procedures for 2017/18* uzisome kwa umakini na kuzielewa kuepuka kusumbuka dirisha likifunguliwa.
Tufuatilie katika Page yetu kwa Msaada zaidi
#School_Base_Online
POWERED BY [HASHTAG]#SBO[/HASHTAG]
 
mim nilikuwa nauliza kwenye uchaguz wa course mm nimesomea IT je naweza somea electrical engineering au mechanical??
 
Napata tatizo kupata verification number. Nikiapply naambiwa Registration number na graduation year haviendani. Nacte wananiambia hawana data zangu, nimeenda chuo wameniambia wameshatuma taarifa zangu nacte! Nifanyeje! Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzumbe mbeya campus
Wapigie nacte watakuelekeza chakufanya... Kuna mtu wangu wakaribu alikumbana na tatizo kama hili alishalitatua...kuna sehemu pale pakuandika graduation year click pale uniambie pameandikwa nini nanini nikusaidie kuna neno.unatakiwa ku click nimelisahau...fanya fast nikusaidie..
 
Wapigie nacte watakuelekeza chakufanya... Kuna mtu wangu wakaribu alikumbana na tatizo kama hili alishalitatua...kuna sehemu pale pakuandika graduation year click pale uniambie pameandikwa nini nanini nikusaidie kuna neno.unatakiwa ku click nimelisahau...fanya fast nikusaidie..
 
Wapigie nacte watakuelekeza chakufanya... Kuna mtu wangu wakaribu alikumbana na tatizo kama hili alishalitatua...kuna sehemu pale pakuandika graduation year click pale uniambie pameandikwa nini nanini nikusaidie kuna neno.unatakiwa ku click nimelisahau...fanya fast nikusaidie..
Sorry, nlikosea mwanzo.
Kwenye graduation year pameandikwa click here kama mwaka wako haupo, kisha kuna 2014-16

Sent using Jamii Forums mobile app
 
avijatoa - havijatoa
swara - suala
udaili - udahili
But thanks for information keep together.
 
Kuna baadhi ya vyuo havipo TCU guide book, je ndiyo vimefutwa au? Telimishane.
1.eckernforde Univ Tanga etc
2. Tumaini Unive--kcmc (MD programme) hakuna
3. etc

Tatizo ni nini?
 
Back
Top Bottom