Ufafanuzi; Waziri Mkuu alilidanganya Bunge na Taifa

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,027
1,299
WAZIRI MKUU ALIDANGANYA TAIFA:

Waziri mkuu wa Tanzania anazidi kujitengenezea rekodi isiyofaa baada ya jana tena kuliongopea taifa kupitia bunge,Mh Pinda(mb) jana kwenye kipindi cha maswali kwa waziri mkuu aliutangazia umma kuwa yeye analipwa jumla ya tsh milioni sita iwapo atajumlisha na posho ya mkewe, waziri mkuu alitoa majibu hayo bila kufafanua kuhusu malipo mengine ayapatayo.

UKWELI WA MAPATO YA WAZIRI MKUU Waziri mkuu anapokea tsh mill 11.3 kama mshahara wa mbunge,anapokea tsh mill 6.2 kama mshahara wa waziri, pia anapokea tsh mill 4 na mkewe tsh mill 2 kama stahili ya waziri mkuu na mkewe, aidha waziri mkuu anapokea sitting allowance kubwa kuliko mbunge wa kawaida, na marupurupu kibao ambayo iwapo atachukua kwa pamoja basi ataingiza zaidi ya tsh mill 30 kwa mwezi mmoja.
 
Watanzania tuna kawaida ya kuchukulia vitu poa lkn vinatuangamiza taratibu,Mtu kama Pinda hata sijui kwanini bado anaendelea kuwa waziri mkuu......ana orodha ndefu sana ya drama...
 
HAPA SASA NINGEPENDA NIMWONE KIJANA WA KAZI, UKWELI, UWAZI NA UMAKINI ZZK AKITHIBITISHA BUNGENI JUU YA MALIPO YA WAZIRI MKUU NA KISHA AMWOMBE SPIKA AMSAMEHE PINDA KWA KULIDANGANYA BUNGE. Peoples!!!!!!
 
unaweweseka wewe mleta mada. waziri mkuu anapokea milioni 6.2, zingine ni za ubunge. kawadanganye watoto wadogo
 
Kama Waziri Mkuu,alilenga kujibu ni mshahara gani anaupokea kama ''Waziri Mkuu'',bila kuzungumzia nafasi nyingine,kwa kiwango cha milioni sita alichotaja yuko sahihi.Ila kama suala la mshahara limeongelewa yeye kama Pinda,na vyeo vyake vyote hapo atakuwa amedanganya.Inahitaji tafakari kubwa hapo.
 
"....CCM ni chama cha kilaghai...." - by ZeMarcopolo.
Waziri mkuu (Pinda) amedangaya tena bungeni...!!
Wapi Ritz, Simiyu Yetu (mrembo sana huyu), FaizaFoxy, na Mamndenyi.

EDdude.jpg
 
Last edited by a moderator:
WAZIRI MKUU ALIDANGANYA TAIFA:

Waziri mkuu wa Tanzania anazidi kujitengenezea rekodi isiyofaa baada ya jana tena kuliongopea taifa kupitia bunge,Mh Pinda(mb) jana kwenye kipindi cha maswali kwa waziri mkuu aliutangazia umma kuwa yeye analipwa jumla ya tsh milioni sita iwapo atajumlisha na posho ya mkewe, waziri mkuu alitoa majibu hayo bila kufafanua kuhusu malipo mengine ayapatayo.

UKWELI WA MAPATO YA WAZIRI MKUU Waziri mkuu anapokea tsh mill 11.3 kama mshahara wa mbunge,anapokea tsh mill 6.2 kama mshahara wa waziri, pia anapokea tsh mill 4 na mkewe tsh mill 2 kama stahili ya waziri mkuu na mkewe, aidha waziri mkuu anapokea sitting allowance kubwa kuliko mbunge wa kawaida, na marupurupu kibao ambayo iwapo atachukua kwa pamoja basi ataingiza zaidi ya tsh mill 30 kwa mwezi mmoja.

waziri mkuu alikuwa sahihi wewe ndio unapotosha umma.
waziri mkuu ni mbunge kwa hiyo lazima apokee posho na mshahara wa mbunge, kumbuka ana watu jimboni anapaswa kuwatumikia, lazima alipwe mshahara wa waziri na sitting allowance ni mhm pia. tuwekee pia malipo ya ziara ya slaa kwa siku 10 za ziara yake inayoendelea hivi sasa japo imedoda
 
Hivi Josephine Mshumbusi ni nani ndani ya Chadema?ni mchumba wa katibu mkuu au ni mke wa katibu mkuu?
Kwangu mimi mke wa katibu mkuu ni Mh.Rose kamili,Josephine ni kama hawala tu kwa sababu hana power yoyote ya kusema slaa ni Mume wake.

Inakuwaje josephine anakuwa na power ndani ya chadema hasa katika uongozi?anatumia tuzuku za chama kama nani?

JOSEPHINE MSHUMBUSI amesababisha haya.

Amesababisha mgogoro mkubwa sana kati ya Mkurugenzi wa Fedha wa chadema na Mmiliki wa mwanahalisi Bwana Anton komu ambaye ameshaambiwa na katibu mkuu ajiuzulu uongozi,ili Josephine apewe kiti cha kumanage fedha za chama.

Josephine amemuundia zengwe erasto tumbo pale makao makuu kwa sabau eti Erasto tumbo hamheshimu Josephine na anamshawishi Dr.slaa amtimue,wanashindwa kwa sababu hawana kosa la kumbambikia Erasto tumbo.

Josephine ameleta mgogoro mkubwa kwa madreva wa chama pale makao makuu,yaani anawacontrol as if ni watoto huku akiwatupia matusi na vijembe mbalimbali.(madreva wanamgomo wakimyakimya kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa viongozi wetu wa chama).

Josephine amemshawishi Dr.slaa aandikishe jina la YAYA wa mtoto wa Dr.slaa kwenye kitabu cha watu wanaotakiwa kulipwa na chama kwenye kesi ya arusha(ili hali yule binti hana hata kadi ya chama) Pia cha kushangaza ni Josephine,slaa na Yaya ndio wanaolipwa kwenye ile kesi wakti kunawatu ambao hawalipwi hata posho ya sent kumi.

Sasa huyu Josephine yupo chadema kwaajili ya kutuulia chama au kwaajili ya kumpiga piun Dr.slaa ili maamuzi yote yawe yana toka kwa josephine
 
mawaziri wa ccm MUNGU amewanyima busara hawana hata hofu ya MUNGU waziri mkuu pinda na amepinda kweli anadanganya bunge tatizo bunge linaendeshwa na spika wa ccm
 
waziri mkuu alikuwa sahihi wewe ndio unapotosha umma.
waziri mkuu ni mbunge kwa hiyo lazima apokee posho na mshahara wa mbunge, kumbuka ana watu jimboni anapaswa kuwatumikia, lazima alipwe mshahara wa waziri na sitting allowance ni mhm pia. tuwekee pia malipo ya ziara ya slaa kwa siku 10 za ziara yake inayoendelea hivi sasa japo imedoda

Kwa hizo fedha zingine hazipokei kwasababu ni Mp?
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom