Ufafanuzi wa Ziara za Mkuu Wetu Nje ya Nchi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi wa Ziara za Mkuu Wetu Nje ya Nchi.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Boflo, Apr 17, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naomba kupewa ufananuzi kuhusu ziara za Rais (JK) nje ya nchi.Haupiti mwezi mmoja bila Bwana Mkubwa kusafiri nje ya nchi.
  Ninabaki na maswali kichwani! hivi hana watu anaowaamini wa
  kumwakilisha nje ya nchi kwenye shughuli zinazompeleka huko?
  Ninakuwa na wasiwasi kama anapata muda wa kukaa ya kuambiwa au kuyaona
  matatizo tuliyonayo watu wake. Sijaona na labda sio rahisi kuona
  impacts za ziara zake kwenye uchumi na maendeleo ya nchi zaidi ya T-
  shirt ya Cristian Ronaldo -(BWIN). Kutumiwa T-shirt si kitu cha kuvijunia
  mpaka unaita press kuwaonyesha. Kwa Lumpen wa mitaani, Yes; lakini kwa
  president, No. Kwa sababu wananchi wako hawajaona any added value kuwa
  na T-shirt Ya Cristian.
  Hebu angalia President wa Kenya, how often he travels outside the
  country? very rare and when it happens, it is justified. Na sio Kenya
  tu, bali Uganda Rwanda,Zambia na Malawi. Angekuwa President wa Burundi
  kwenda nje mara kwa mara ningeelewa, lakini sio kwa Rais ambaye
  amekuwa Foreign Minister kwa muda mrefu.
  Kitu kingine, ni bahati mbaya gharama za safari zake hazitajwi, lakini
  naamini zingejulikana, huenda Watanzania tungeandamana kwa sababu bila
  shaka ni za kutisha.
  Inawezekana kabisa moja ya hobbies zake kubwa ni kusafiri. na kitu
  kikiwa hobby, oops! tutakuwa tunamuonea kumsema.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Boflo,
  Unless kuna kitu kimenipita lakini katika hii ziara ya karibuni New York Tanzania ingeweza kuwakilishwa vizuri tu na Waziri anayeshughulikia masuala ya gender.
  Haikuwa lazima rais wetu awepo kwenye huo mkutano.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mie nilisha mpendekeza ni bora aturudishie nchi yetu na awe muhudumu wa ndege!!!:confused3::behindsofa::angry:
   
 4. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du!
   
 5. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni kweli hizi ziara zimekuwa nyingi sana, na kila siku ni nchi ile ile tu....why is so proud of US? na nini maana ya kuwa na waziri wa mambo ya nje? na akifika marekani kuna mambo anafanya huku nyumbani hafanyi....sijawahi kusikia JK ameenda kuongea na wanavyuoni hapa nchini achia mbali hata walimu wa vyuo ambao ni wataalamu katika nchi hii, hata makongamano mengi yameandaliwa nchini hapa lakini amekuwa simhudhuriaji, lakini mengi yanayofanyika marekani ana-atend....mi nadhani kuna ajenda ya siri...na tutaijua tu siku, hata kama nikatika kutafuta misaada lakini huwezi kila tatizo lako unapeleka sehemu moja tu utadharaurika....lazima JK ajue kwamba watu waku-impress ni wananchi wake walioko hapa nchini nasio wa nje....wale washashiba hata kuwatumia mwakilishi ytosha.
   
 6. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #6
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ukiangalia kwa undani suala la msingi si mara ngapi "Muungwana" ameekuwa akisafiri kwenda nnje ya Inchi,ila swali la msingi ni kiasi gani anatilia mkazo matatizo ya kimsingi yanayotukabili kuliko safari husika. Na lilio la karibu ni hili la kuchangishana bilioni 40 za kampeni huku kwenye gazeti la the guardian la tarehe 25 March Waziri wa Elimu J.Magembe anakaririwa akisema uhaba wa vifaa vya kufundishia mashuleni unaitia aibu serikali ya awamu ya nnne.

  Sina nia mbaya ya kuipaka matope serikali yetu au kuwa mtu wa kutupa lawama,ila hebu tuulizane....kama mkuu wetu anaenda New York kuomba misaada ya kimaendeleo,halafu huku nyumbani unafanya harambee ya kuchangisha mabilioni kwa ajili ya tshirt,khanga,magari, na helikopta za kampeni ilhali una uhaba wa kutisha wa vifaa vya kufundishia....kweli....kweli inaingia akilini?.Je huku si kujikanyaga kwa baba mwenye nyumba kwenda kwa jirani kuomba msaada wa chakula huku amebeba kreti la bia alilojinunulia..

  Kama tungekuwa tunaona serikali yetu inatilia mkazo matatizo ya msingi hasa Afya,Elimu na chakula...hata kama mkuu wetu angekuwa analala New york na kuja kufanya kazi asubuhi mimi nisingekuwa na maswali,ila ninaposikia matukio ya ujambazi ukerewe, manesi mwananyamala, mauaji tarime,mafuriko kilosa,uhaba wa vifaa kufundishia,migomo ya wafanyakazi,wanafunzi wa chuo wakishindia mikate na maji ya kunywa, wazazi wakifa kizembe wakati wa kujifungua, miradi ya maendeleo siyokwisha kwa kuwa wakurugenzi wametafuna hela, mafisadi wakishinda kesi,wakulima wakihaha kutambika ili mvua za msimu zisikate mapema....halafu mkuu unasikia yuko Brazil.....

  Nanyong'onyea...na kubaki kumkumbuka Hayati baba wa Taifa....LAITI NYERERE ANGEKUWEPO!!! Ila alisema "Mtanikumbuka!!!"
   
 7. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana marafiki wengi wafanyabiashara, wawekezaji na mabalozi Mbona anawachangisha pesa kwa ajili ya kampeni za CCM lakini siyo madawati mashuleni
  Za madawati anaomba US kwa nini?
  mh? something must be wrong
   
 8. m

  mtoto wa mjini JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2010
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 1,536
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  Bajet ya tanzania 40% ni misaada kutoka nje,asipo safiri nje utalala njaa.
   
 9. K

  Kekuye Senior Member

  #9
  Apr 17, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninafikiri kuna kila sababu ya kukaa chini na kufanya tathmini ya mafanikio ya safari zake. Kulikuwa kuna hoja kuwa amekuwa akienda kuitangaza nchi katika maswala uwekezaji na vivutio vya utalii. Inawezekana ni kweli kuna ongezeko (sina takwimu) ila inawezekana vilevile matumizi ya safari yameongezeka kwa kiasi kikubwa (sina takwimu vilevile). Ingekuwa busara iwapo tungejizatiti kwanza kwenye maswala kama kuimarisha viwanja vya kimataifa vya ndege tulivyo navyo, bandari na huduma nyingine ndiyo tujitangaze tukiwa tumeandaa mazingira ya kunufaika na kazi anayoifanya ya kuitangaza nchi.
   
 10. c

  cerezo Senior Member

  #10
  Apr 17, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kenya 40% misaada kutoka nje, Uganda 60%, Rwanda 50%, Burundi 60%....the list goes on and on...hujaona maraisi wa hizo nchi wakisafiri kwenda nje kila mara!!
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Dr Shein apewe uraisi october,Membe hawe makamu wa raisi na JK arudishiwe uwaziri wa mambo ya nje hili haweze kumalizia safari zake ambazo hakumaliza wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje mwanzo.Tunataka raisi ambaye ataweza kutatua matatizo yetu ya ndani sio amabye anasafiri safiri tu au kama vipi wavunje wizara ya mambo ya nje. JK afanye kazi zote mbili na bajeti ya wizara ya mambo ya nje ipelekwe wizara ya afya tupate uduma nzuri hospitalini.
   
 12. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Prezidaa wetu ni 'hands on type of a leader', kwa hiyo kila kitu lazima ahakikishe kinakwenda sawia ili kuliletea taifa letu maendeleo.....my thought :confused2:
   
 13. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Si kwa JK tu,na mawaziri na wabunge pia.
  Watu hawa wameona unono wa kusafiri nje ya nchi,kwa hiyo kumlaumu Mbeba BOX eti anakaa Ulaya ni hypocricy ya hali ya juu.UK kuna kitu kinachoitwa FOI(Freedom of Information),ambapo raia yoyote unaweza kuulizia na kupata details kama hizi kwenye chombo kinachohusika.

  Ni kweli Kibaki hasafiri safiri sana kama wa kwetu.Na UK kwa sasa ni jamvi la mawaziri wetu.Na kuwanzishwa matawi ya SISIEM na TAUk ndio imekuwa nongwa sasa,mtawaona hawa vilaza kila siku.Tangu mwaka umeanza tumewaona akina Msekwa,Nchimbi Na Membe wakijipa trip UK eti kutoa kadi za CCM au kuhutubia wa TZ huku.Hata Vice wa UDSM alikuwa naye kwenye mkumbo huu,ningemweshimu kama angekwenda kutoa lecture Oxford,LSE au Uni yoyote kama kweli huo uprofesa wake ni class act.

  Angalia Pinda naye ziara zake Mashariki ya Mbali.Hakuna lolote watu hawa,na wazungu wanadharau sana hili,ila watakuchekea tu,maana wanajua what is going on on your country.I bet kuna siku ya Muungano inakuja ,kuna VILAZA mawaziri watasafiri Ulaya eti kusheherkea.Kwa nini wasiende majimbo yao kuungana na wananchi wao kusheherekea ?

  Nasikia naye 'dr' Aman Karume yuko London vilevile eti kuonana na Wazenj wa UK!
  Nchi hii inaliwa ,hakuna mwenye uchungu !
   
 14. M

  Mutu JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unaweza kukuta kila anakokwenda anakuwa rais pekee yake ,marais wezake wanatuma wawakiliisi kama mabalozi,waziri n.k kutokana na uzito wa mambo.
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inawezekana! lakini hili la utegemezi lipo hata kabla ya yeye kuingia madarakani na kama tutakuwa tukiona fahari kwa hili la kuombaomba badala ya kutafuta njia za kujitegemea basi tatizo lipo hapo.

  Halafu kwanini mkuu anachukua msururu wa watu unaogharimu mabilioni kwa ziara za kutafuta msaada ambao huenda ukapatikana au usipatikane au pengine msaada huo uje baada ya miaka na huku tushatumia viakiba vyetu tunavyovihitaji hivi sasa.
  Kiongozi wa nchi huitaji washauri lakini kwa hili la safari washauri wa Rais wetu hawatomshauri kinyume chake hata kidogo kwani ni wao wanaofaidika na safari hizi.
   
 16. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #16
  Apr 18, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwani hii nchi ina Rais? Kwa sababu kila siku hayupo nchini, sijui kazi za kitaifa anafanya nani? kazi yake sherehe, makongamano, uchangishaji wa chama, sijawahi kumsikia akizungumzia elimu yetu ya Primary, Secondary etc inavyoshuka, sijamsikia akizungumzia nini suruhisho la shule za kata alizozileta na wale waalimu wake wa VODA FASTA.

  MUDA UMEFIKA WATU TUKAWA MACHO NA WATU TUNAOWAWEKA MADARAKANI, WENGINE WANATUMIA NAFASI HIZO KUFULFILL DREAM ZAO ZA UTOTONI.
   
 17. F

  Firdous Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heeeee, Tumpeni nafasi kwanza

  Jamani huku tunakoelekea sasa siko kabisa. Hivi hizi safari hata kama zitakuwa nyingi kiasi gani tulishapima kujua tunafaidika nazo vipi ama tunalaumu tu. Hemu wenye data za uhakika watuambie ni kiasi gani cha pato la taifa kimepotea kwa safari hizi. Ni kiasi gani taifa limefaidika na safari hizi.

  WEngine humu ndani tunasema eti mbona maraisi wengine hawasfiri. Hivi jamani tunajua Maaana ya urasi ama tunasema tu.

  Hivi kweli tunajua ni kipaumbele gani serikali hii na rais ameweka katika awamu yake hii ama tunalaumu tu bila ya kujua.

  sasa kama kila kazi tunataka rais awepo hapa nyumbani na hao mawaziri na wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya wanafanyakazi gani hapa nyumbani na kwa nini wapo

  Jee tunajua kwa nini tumeamua kuwa na VP na Waziri Mkuu katika serikali yetu. na jee tunajua muundo wa kazi zao ukoje. ama nao hao pia tuwe tunawalipa bure tu bila ya kazi na kazi zote afanye RAIS.

  Nadhani huku tunakokwenda itabidi kila kazi afanye rais hata zile zinazopaswa kufanywa na wajumbe wa nyumba kumi ama wakuu wa serikali za mitaa.

  Hivi hawaa jamaa wa huku nje tunawajua walivyo na dharau na bara letu la afrika. Anakuja rais wala hawajali si kwambia aje waziri mkuu ama mkurugenzi kutoka afrika.  Ukiamua kutafuta kwa manufaa ya familia yako ni vyema ukatafuta wewe mwenyewe kwani ndio mwenye jukumu . na usimtume mtu.

  Jamani tumpe nafasi RAIS , anafanya hayo kwa manuafaa ya waliomuweka madarakani na hilo ni jukumu lake.
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  It is simple ,unauliza tufanye utafiti tunapoteza kiasi gani kwa ziara zake nyingi za nje?????
  Just simple mathematics ni kiasi gani tunge save kama asilimia 90% ya ziara zake angewakilishwa na mabalozi husika? Je tunahitaji takwimu kujua tunapoteza senti .......?????? wake up !
   
 19. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  No comments
   
 20. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  No comments
   
Loading...