Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,445
Pichani uwaonao kwa ujumla wao unaweza kuwaita mapaka, nilichokifanya kwa leo nitakutajia kila mmoja kwa jina na sifa zake, ili siku ukimuona uweze kutoa taarifa kwa jina lake sahihi, usije sema chui kumbe ni vinginevyo, karibu......!
1. Mondo (Serval)
Ni mnyama mdogo jamii ya paka, kama walivyo wanyama wengine wawindaji naye hula nyama tuu, huwinda wanyama wadogo pamoja na ndege, ni mjanja mjanja wapo wa aina mbili huyu kafanana na chui lakini mwingine hufanana na simba, Sifa zake
- Ndio mnyama mdogo jamii ya paka waishio polini kuliko wote
- Ana uwezo wa ajabu katika kukamata ndege huweza kuruka naye angani anapojaribu kupaa.
2. Chui mweusi (black Panther)
kwa bahati mbaya mnyama huyu hatuna Tanzania wanapatikana sana amerika, naye chakula chake ni nyama tuu, sifa zake mbili
- Tofauti na wenzie yeye ana rangi ya kipee nyeusi.
- Ni bingwa sana wa kujificha hata kuonekana kwake ni nadra.
3. Chui milia (Tiger)
Kama walivyo wengine ni mla nyama, ndiye mnyama pekee jamii ya paka anayeweza kufugika kiurahisi, tofauti na wenzie wote ambao ni kama kunguru tuu, kama ni mfuatiliaji mzuri wa sanaa ya muziki, utakuwa umemuona akiwa na wasanii mbalimbali kama akina Eve nk. Na hapa nyumbani alitokeza katika video ya mwanamuziki Rich Mavoko, sifa zake
- Ndiye mkubwa kwa umbo kuliko wote wa jamii yake na ukubwa wake huzidi kwa simba.
- Ni mpole kupita kiasi.
4. Chui (Leopard)
Nadhani hapa kwetu huyu jamaa ndio maarufu kupita wote, na ndiye mnyama ambaye wanyama wenzie wa jamii yake huitwa jina lake, wana nguvu sana miguu ya mbele, katika wanyama walio ua binadamu anashika namba kumi, ni hatari na wakuogopwa zaidi, katika mapambano huwa hapimi mpaka aumie ndio atakimbia, sifa zake
- Ni mnyama mzinzi kuliko wenzie wote, anahonga majike na yakishika mimba huyatekeleza.
- Ana aibu sana ukimtizama atajifanya amelala ili msigongane macho, pia ana tabia ya uchoyo chakula chake huficha juu ya miti.
5. Duma (Cheetah)
Ukikaona ni kadogo dogo kwa umbile, mbuga kama serengeti vipo vya kutosha ni miongoni mwa wanyama ambao wapo katika hatari ya kutoweka duniani, kametawaliwa na hasira muda wote, na hupenda kutembea kwa makundi makundi, Sifa zake
- Ndio mnyama anayeongoza kwa kukimbia kwa wanyama wa ardhini kuliko mnyama yoyote duniani.
- Katika jamii yao huyu ndio mwenye mikwala usiombe ila wakimfuata anatumia kipaji chake (mbio).
6. Jagwa (Jaguar)
Anafanana sana na chui tofauti yao ni moja tuu huyu rangi yake imekolea sana, lakini usipokuwa makini yawezekana kabisa ukafikiri yeye ndio chui, lakini si rangi tuu hata baadhi ya matendo pia hufanana, sifa zake
- Ni mkatili pasina mfano pamoja na uzuri alionao, akihasama mdomo wake huwa harudi nyuma vita yake ni mpaka mmoja afe ama yeye au wewe
- Ana nguvu za ajabu ndio mnyama pekee ambaye huwawinda mamba na kuwatoa nchi kavu kisha kuwaua, kama umepata kuona baadhi ya video ukawa unasema chui amebeba mamba basi nakuhabarisha chui mchezo huo hauwezi kazi hiyo anafanyaga huyu bro
Je umefanana na paka yupi kati ya hao ?
Wasalaam !