Ufafanuzi wa Ndalichako wa Necta haukubaliki, awajibishwe kwa manufaa ya UMA- Mwanahalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi wa Ndalichako wa Necta haukubaliki, awajibishwe kwa manufaa ya UMA- Mwanahalisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Mar 7, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kuna makala moja ktk gazeti la Mwanahalisi la Leo kuhusu majibu ya Dk Ndalichako aliyoyatoa Zanzibar alipokutana wanahabari.
  Hoja ya msingi.
  Ndalichako amekataa kukiri kwamba mtihani 2011 ulivuja. lakini alidai kwamba wapo wanafunzi waliokutwa na majibu ya mtihani ndani ya simu zao. Jee walipata wapi majibu haya?
  Lakini mwandishi amedai Ndalichako hakusema source ya message hiyo. inawezekana zilitokea ktk shule zilizopata div 1 yaani st.
  Amedai walimu na wasimamizi walihusika kwa kiwango kiubwa.
  hoja kama hivyo ndivyo, huu ushahidi wa NECTA waliupata wapi au ndio huu unaolalamikiwa wa Kufikirika uliofanywa kwenye meza za mahotelini wakati wa vikao?

  hoja kwamba wanafunzi walikuwa wakipeana vikaratasi ndani ya Chumba.
  Jee kama wanafunzi 120wanapeana vikaratasi ndani ya masaa 3?, jee kitakuwa chumba hicho au soko la wauza samaki pale FERI?
  Lakini wasimamizi hawa sio ndio waliopewa na tuzo na NECTA 2010 kwa usimamizi uliotukuka?Iweje 2011? na sio 2010, 2009?
  Eti dk ndalichako amekataa kukiri mtihani umevuja ili kulikimbia joto la Vyombo vya habari na wanaharakati, isipokuwa anatumia njia hii ya kuwakndamiza watoto kwani sauti zao hazisikiki popote.
  Alipoulizwa anahisi vipi sheria hii ya miaka 3 kwa mwanafunzi aliekutwa na hatia. alijibu aaaaa ndio sheria ban.
  Hivi sheria hii kwa watoto wa Zanzibar mbona darasa la 7 2011 wameruhusiwa licha ya kuiba mitihani inayotungwa na hawa hawa walioshindwa Kazi yaani NECTA ya Ndalichako?


  DK ndalichako na kundi lake wanatakiwa wajiuzulu kwa kashfa hii nzito, vyenginevyo
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Huyu mama hii phd yake sijui ni feki? lkn tatizo ukabila ndio ulioangamiza taifa. maana baadhi wabunge walitaka mama huyu awajibishwe kabla ya 2010 . lkn wabunge wa kabila lake walikuja juu. hili ndio tatizo la tanzania. huyu mama hafai kabisa NECTA
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kweli tz ni shamba la bibi. anaetakana anafanya lolote. kama huyu mama uarabuni au South Afrika tungalikuwa hatunae tena. lkn tz bana. kuna anaefanya anaetaka tena kwa kujiamini
   
 4. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Jamani Tuwe Systematic!! Suala la Elimu Halina siasa!! Nashangaa suala Nyeti Kama Hili linapelekwa Kisiasa!! Tunapigania Jumuiya ya Africa Mashariki Tujue pia elimu Ni sehemu Muhimu ya Kazingatia!! Hakuna mtu anaweza kuchezea suala la Elimu!! Hakuna Shortcuts!! Hivyo namsihi mama Ndalichako asimamie anachokiamini kwa Haki!! Kwani ukweli usiopingika Elimu Imeshuka sana hasa Tanzania kutokana kuchanganywa na siasa!!
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  tatizo linakimbiwa, tatizo ni huyu mama Ndalichako na NECTA yake, au kwa kuwa mnapata div 1 za st ndio mnafumba macho?
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kunguru Mweusi unaweza kutuwekea hiyo habari yote kama ilivyoandikwa kwenye Gazeti la Mwanahalisi. Halafu chini kama utataka ndiyo uweke comments zako.

  Maana Jana kwenye mapitio ya magezeti Gazeti la Zanzibar Leo liliandika kwamba Wazanzibari wameunda TUME kuishitaki NECTA (something like that).

  Kitu kimoja ambacho sijaelewa kwanini hao wote wanaohisi kuwa wameonewa kwanini hawataki kukuta rufaa na mitihani yao ikasahihishwa upya? Maana fursa hiyo IPO.
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  na serikali inamfumbia macho
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  unajua hapa sio kukataa rufaa. hawa hawakusahihishiwa, wamefutiwa matokeo, ni vitu 2 tofauti. kufutiwa na kusainishiwa vibaya. hii ni kwa mara 1 duniani kutokea kitu kama Hichi.
  120 kati ya 121 wanafutiwa matokeo anabaki 1 halafu Necta inadai hakuna mtihani uliovuja. Inasemakana hii mitihani huanzia kwenye hizo shule za SEMINARY
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ushahidi wa udanganyifu katika mitihani huanzia shule husika ni vema wanahabari wangefika katika shule zilizokumbwa na kadhia hii na kutupa ukweli kama wanafunzi hao walikutwa na udanganyifu wa ama kuingia na karatasi, kuwa na majibu kwenye simu, kuwa na vikarasi vyenye majibu chumba cha mtihani, kusaidiawa kufanya mtihani na mtu mwingine au waalimu wa shule husika.

  Udanganyifu ambao unapatikana baraza ni ule wa majibu ya mtihani kufanana kwa watahiniwa wengi wa darasa moja au shule moja ambayo ni ishara ya kuvuja au kutofautiana kwa mwandiko katika karatasi za mtahiniwa jambo linaloonyesha kwamba mtihani ulifanywa na watu wawili tofauti.

  lakini pia tusichanganye kuvuja kwa mtihani na kufanya udanganyifu ni mambo mawili yenye tofauti kubwa.

  Wanahabari wangechukua japo wanafunzi wawili tu wenye malalamiko ya kuonewa wawapeleke baraza la mtihani kukata rufaa ambapo karatasi zao za mtihani waliofanya zitaitishwa mbele ya jopo jipya na mashahidi kufukua ukweli. Hatua hii haina gharama ingeweza kusaidia kupata ukweli.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Takbiiiiiiir
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hapa wanu wanataka kujua jee 2011 mtiahani ulivuja? na kama ulivuja ulaithiri vipi div 1 za seminary?
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mtihani hauwezi kufutwa wote bila kusahihisha japo karatasi moja na kulinganisha na mitihani inayofuata ambayo sio lazima kumaliza kusahihisha kama hitimisho limefikiwa kwamba ulivuja au kulikuwa na udanganyifu.

  Mitihani ambayo haisahihishwi kabisa inatokea baada ya ushahidi kuwa wazi lakini ni lazima timu ya kusahihisha mitihani hiyo ipitie karatasi moja baada ya nyingine kujiridhisha na tuhuma lakini pia kuna baadhi ya udanganyifu baadhi ya wanafunzi wanakuwa hawajahusika hata kama yamefanyika ndani ya darasa moja. Mtihani unaweza kuvuja lakini baadhi ya wanafunzi wanaweza kuwa hawakupata timu ya kusahihisha itapitia na kujiridhisha kwamba wapo ambao hawakufanya udanganyifu au kuvuja.
   
 13. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Lakini mwandishi amedai Ndalichako hakusema source ya message hiyo. inawezekana zilitokea ktk shule zilizopata div 1 yaani st.
  Amedai walimu na wasimamizi walihusika kwa kiwango kiubwa.
  hoja kama hivyo ndivyo, huu ushahidi wa NECTA waliupata wapi au ndio huu unaolalamikiwa wa Kufikirika uliofanywa kwenye meza za mahotelini wakati wa vikao?


  hoja kwamba wanafunzi walikuwa wakipeana vikaratasi ndani ya Chumba.
  Jee kama wanafunzi 120wanapeana vikaratasi ndani ya masaa 3?, jee kitakuwa chumba hicho au soko la wauza samaki pale FERI?  Tuache siasa kwenye mambo ya kitaaluma, kama huna uwelewa wa jinsi mitihani inavyofanyika basi usipende kulaumu kwa vile hujui. Wasimamizi wanaweza kushirikiana na wanafunzi na kila mmoja anaadhibiwa kivyake mwanafunzi kufutiwa mtihani, msimamizi kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa sheria za kazi. Sasa hivi tusonge mbele kwa kutatua tatizo la ubora wa elimu, kama kumbukumbu za mwandishi zipo sahihi Rais Mkapa wakati huo alisema kabla ya kuanza kujadili ubora wa elimu watoto wote wawe shule, kama tunataka kuanza kujadili ubora wa elimu sasa Rais msaafu aliomba wamshauri ni mtoto wa nani abaki nyumbani ili tuboreshe elimu.
   
 14. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wewe Kunguru mweusi unasumbuliwa na ugonjwa mbaya wa UDINI ambao mtu akiuangalia vibaya anaweza sema una wivu na shule za Seminari, maana matokeo ya shule za Seminari inaonesha kama yanawanyima usingizi kwelikweli.
  Hatahivyo yawezekana Wazanzibar mna hoja ya msingi, lakini tulieni na mfanye mambo kiutaratibu mtaeleweka, mbona watu wote wanaoweza kumuwajibisha Ndalichako ni Waislamu wenzenu? Sidhani kama wanaweza kuruhusu huo mnaouita "mfumo kristo" uwameze wakiwa wanaangalia. Mkuu wa kaya, waziri wa elimu wote hao si ni wenzenu?
  Pelekeni malalamiko yenu na huo ushahidi wenu washughulikie, siyo kukaza mishipa na kutoa povu kila siku kwenye vyombo vya habari bila ya kuchukua hatua yeyote.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hivi nyie wanzanzibati nani anawazuia kuwa na NECTA yenu? Hebu acheni kulalama kila siku
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  uSHAWAHI KUSIKIA NCHI YOYOTE DUNAANI AU TAASISI YOYOTE YA ELIMU YA JUU AU HATA NACTE hali kama hii? 201 kati ya 202 wanafutiwa mtihani Chumba kimoja anabaki 1 Ulipowahi kufanywa na Chombo chochote cha elimu Dunaani. Toa mfano basi
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hapa sio swali la UDINI. udini unaongiza wewe? HAPA Ushawahi kuona nchi yoyote duniani aliwahi kufanya vituko hivi? au ndio kwanza NECTA ya Ndalichako?
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Lazima ujue tofauti ya mtihani kuvuja na wanafunzi kuigiliziana.....Kuiigiliziana ndio lilikuwa tatizo ambapo majibu ya watoto yalifanana hata kama hayakuwa sahihi na ndio sababu ya kufutiwa....huyo mmoja pengine ndie alikuwa malaika peke yake.....majibu yake hayakyfanana na ya wenzake
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama una mashaka na matokeo ya shule yoyote ya seminary unaruhusiwa kama mtu binafsi au timu ya watu kukata rufaa kwa maelezo kwamba una mashaka kuna udangayifufu wa matokeo.

  Jambo hili ni kwa maslahi ya taifa haitoshi kupiga kelele tu bali ni pamoja na kuchukua hatua za kusonga mbele hadi baraza la mitihani.


  kuna shule kama St. Paul na St. Magreath hazina Div 1 hata moja, hakuna Div 2 na Div. 3 hazizidi tano wengi wako div. 4 na ziro. Tazama kwenye tovuti ya baraza la mitihani zipo shule za kutosha za st. ambazo hazikufanya vizuri.
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ninashangazwa sana na ukimya wa walimu wa shule zinazodaiwa kuonewa kwani wao ndio wanajua uwezo wa wanafunzi waliokuwa wanawafundisha kuliko hata sisi tunaobishana hapa JF wangeweza kuwa msaada mkubwa wa kuwaumbua wahusika wa kupendelea ndani ya baraza.

  Kama kuna ugumu waombe taasisi za kujitolea hasa za wanasheria kuwasaidia kukata rufaa na kusahihisha mbele ya wanasheria wao. Mitihani huandikwa kwa mkono kila mwanafunzi aliyekata rufaa anakuwepo kutambua mwandiko wake ili jopo jipya lipitie kwa mara ya pili.
   
Loading...