Ufafanuzi wa Nape juu ya TBC kubadilisha utaratibu wa kurusha LIVE matangazo ya Bunge

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,371
2,377
Saa 3 usiku huu Waziri wa Habari/Utamaduni na Sanaa Nape Nnauye ataongea na waandishi wa Habari
Fuatilia kujua atakachoongea hasa baada ya kulikoroga asubuhi ya leo ma kusababisha vurugu bungeni jioni
Tune in Azam TV for coverage
 
Sioni haja yoyote kwa Nape kufafanua kitu chochote.

Mijitu ya upinzani haielewi na itabaki hivyo hivyo tu.

Hivyo waziri hana haja ya kutoa ufafanuzi wowote ule....

Sisi wananchi wenye akili tumeelewa sababu ya bunge kutorushwa LIVE na hatuna tatizo na bunge kuonyeshwa katika kipindi kilicho rekodiwa....lengo la serikali lipo very clear - Kubana matumizi.

Ikiwa wapinzani wanataka sura zao zionekane LIVE....waende TBC wakalipie kwa pesa zao.
 
Shida yetu ni kupata live matangazo ya bunge siyo recorded na zilizochujwa kutoka kwa Nape. Labda aongelee kuhusu TFF. Hata hivyo yeye siyo msemaji wa Bunge labda aongee katibu wa Bunge
 
Asipoteze muda na hela za walipa kodi hapa si kakataa wabunge wasionyeshwe ,halafu akatumie hiyo hiyo platform aliyokataza kutoa ufafanuzi wake ,yeye na hoja za wabunge zaidi ya 300 kipi cha maana ??
Angeenda kutolea ufafanuzi Facebook ningemwelewa
 
Azam wenyewe wasitufanye wananchi kuwa wajinga, walizima matangazo sasa kuna haja gani ya kumpa muda wa hewani Nape?. Halafu ni kwa gharama za nani?
 
#Tetty,

Kuona utaona tu kwenye kipindi cha "Bungeni Leo". Utapata taarifa ya matukio yote yaliyojiri bungeni.

Ila kama mnataka bunge lionyeshwe LIVE....nendeni mkalipie Bilioni 4 tu za Kitanzania pale TBC ili mjionee LIVE kipindi cha bunge.

Mengine uliyoandika hapo ni 'irrelevant'.
 
Nape ana wasiwasi mkubwa huenda rafiki yake Jack Gotham aliyepiga pesa ndefu kwenye tenda ya vitambulisho vya taifa atajadiliwa bungeni na siri zote za magoli ya mkono kuvuja live, kaamua kuwanyima uhuru wa kupata habari ili kuficha maovu ya Watu wake.
 
Wewe Nyumbu kwanza kusoma hujui achilia mbali kuelewa. Nimesema hapo kuwa taarifa wananchi wataipata katika kipindi maalum cha "Bungeni Leo" kitakacho rushwa na TBC....Sasa sijui hapo uelewi nini. Kama habari ndio hiyo.. ..LIVE ya kazi gani nyinyi Manyumbu!?

Mkitaka LIVE nyinyi Manyumbu kalipieni gharama ya kurusha matangazo.
Mnataka mfanye kwanza editing siyo? Ili kama mijadala imeibuka ya kuibana serikali mnaamua msirushe kabisa. Mnadhani hatujui namna mlivyokuwa mnalazimika kuzima matangazo na kurudi studio kila mara serikali inapokuwa imebanwa? Magufuli hana tofauti na watangulizi wake. Hizi sarakasi zake zinaisha hivi hivi tu!
 
Back
Top Bottom