Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,206
- 33,223
kwanini kisiwemo kipengele cha mda wa uongozi katiba ya 2006,ndo kusema sasa mwenyekiti aweza kuwa kiongozi hata kwa miaka 50?Uchaguzi ngazi za majimbo, wilaya, mikoa na taifa haujafanyika kwa chama wala kwa jumuiya. Kikatiba, chama kinaanzia ngazi ya msingi halafu tawi, ili ngazi za mbele zifanye uchaguzi lazima ngazi ya chini si chini ya 50 ziwe zimekamilisha uchaguzi. Maeneo yaliyofanya chaguzi ni ngazi hiyo ya misingi na matawi. Tuliamua kufanya uhakiki wa uongozi na ukaguzi na kubaini kwamba tunahitaji kukamilisha chaguzi vitongoji, vijiji na mitaa kwa maana ya matawi na misingi katika maeneo mengi zaidi. Ndio maana ratiba na mkakati vikabadilishwa na sasa kwa sehemu kubwa kanda ndio zinazoratibu kazi katika maeneo yao kupitia M4C ya Kanda na program ya CHADEMA ni msingi. Kuhusu Katiba, nina nakala mango (hard copy) tu ya katiba ya 2004, ilikuwa na kipengele cha vipindi viwili vya nafasi ile ile. Hata hivyo, katiba mpya iliyoandikwa mwaka 2006 haikuwa na kipengele hicho. Hivyo, sio kwamba kimeondolewa kinyemela ila hakikuwepo kwenye katiba mpya. Juu ya uchaguzi wa ndani ya chama, kwa sasa kanda zinaendelea na kazi kwa upande wao kwa vyovyote vile mpaka tumalize kata, majimbo, wilaya na mikoa uchaguzi wa taifa hauwezi kuwa Disemba 2013; iwe ni kwa chama au mabaraza yake. Itakuwa mwaka 2014, na haya yatakuwa ni mabadiliko tu ya ratiba sio ya katiba wala hakutakuwa na kuvunja katiba. Ni kujipa muda tu wa kufanya kazi ya ujenzi wa chama ngazi ya chini kuweza kushinda chaguzi zijazo kwa kuwa na mtandao thabiti. Juu ya ruzuku, toka mwaka 2010 mara baada ya kushinda Ubunge silipwi posho yeyote ya chama, mimi ndiye ninaye kichangia chama. Hivyo, madai yako kuwa nanufaika na ruzuku ya chama hayana msingi wowote. Chama hiki kinajengwa na wengi wanaojitolea kwa hali na mali, ruzuku ni sehemu ndogo sana ya mahitaji ya ujenzi wa chama. JJ