Ufafanuzi wa kinachosambazwa mitandaoni kuhusu DC Muro

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
UFAFANUZI WA KINACHOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU DC MURO

Mimi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Ndugu Mika Lucas likapakapa naomba kuweka wazi ukweli wa tukio linalotajwa katika mitandao ya kijamii kuhusu Dc Muro

Salamu nimeona niseme kidogo kuondoa upotoshaji umaofanywa kwenye mitandao

1. Tarehe 14/07/2021 Nilifanya ziara ya dharura ya kichama CCM katika kijiji cha Minyinga kata ya Makiungu jimbo la singida mashariki, nikiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ikungi nililazimika kufanya ziara ya dharura kufuatia baadhi ya wananchi kuchoma moto nyumba ya mkazi kutokana na mgogoro wa ardhi ambapo kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kuchunguzwa zinataja kuwa baadhi ya viongozi wa siasa walihamasisha wananchi kwenda kuchoma nyumba ya mkazi mwenzo kwa kusingizio cha mgogoro wa Ardhi

Ofisi yetu ya chama ilipokea taarifa kutoka kwa Diwani na mwenyekiti wa CCM kata kuwa kuna machafuko, nikalazimika kuitisha kikao cha ndani cha chama na baadhi ya wananchi na wazee maarufu na viongozi wa dini kujadili changamoto hiyo mana kuna viongozi wetu wa chama pia wanatajwa kuhusika katika mgogoro

Katika jitihada za chama kutatua changamoto hii nililazimika kumuomba Mhe Mkuu wa wilaya ya Ikungi tuambatane wote katika kata ya Makiungu japo Dc Muro alisema jambo hilo linashughulikiwa na vyombo vya kiusalama na hakupenda kuwa sehemu ya mchakato wa hatua za kisheria, ila kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya chama ilitulazimu kwenda nae

Mimi mwenyekiti wa CCM wa wilaya ndie niliekuwa mwenyekiti wa kikao hicho ambacho kilikuwa cha ndani nilitoa nafasi kwa wajumbe kuongea kisha nikamkaribisha Dc Muro kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wananchi haswa wa chama chama mapinduzi na baadhi ya wazee mashuhuri

Dc Muro alitoa ufafanuzi wa kutosha wa hoja zilizoibuliwa na kubwa alilosema ni kuwapiga marufu wanasiasa wanaotengeneza Migogoro ya ardhi kwa ajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa kauli ambayo hata sisi chama tumeiunga mkono mana amani ni jambo la muhimu kwa ccm

UPOTOSHAJI
Wako watu wanasambaza taarifa kuwa Dc Muro amepiga marufuku watu kuongelea katiba mpya

1. Hii ni hoja dhaifu maana kwa Ikungi hakuna mkutano au watu wanaozungumza au kuongelea katiba mpya na hata ofisi ya Dc Muro haina maombi ya watu kuomba kufanya mikutano au makongamano ya katiba mpya hakuna uku Ikungi sisi tuko busy na kilimo na biashara, hivyo Dc Muro hakuwa na haja ya kupiga marufuku mana hatuna mambo hayo sisi wa ccm wala wa vyama vingine na ndio mana hawajafanya mikutano wala sidhani kama wana nia ya kufanya hivyo

Katika hii hoja nachokumbuka ni Dc Muro alikuwa anaongea na kina mama wa pale ndani na Dc Muro aliunga mkono kauli ya mama Martha ambae alisema kwa Ikungi hata wao hawaoni haja ya katiba mpya kwa sasa zaidi wanataka shule na maji na huduma bora za afya jambo ambalo Dc Muro katika hali ya mazungumzo alisema na yeye kwa mtazamo wake anaona aweke kipaumbele katika kuharakisha mchakato wa utoaji wa huduma bora za afya elimu pamoja na miundombinu ya barabara

2. Kuna kipande cha sauti ambacho kinasambazwa mitandaoni

- Hapa naomba niseme kwanza katika kikao cha ndani hakuna alierekodi, na hata ukisikiliza kwa makini utaona mwanzoni kabisa watu wanaongea wenyewe kwa sauti kubwa kuonyesha wanatengeneza kitu, kisha baadae inasikika sauti kwa mbali sana ya mtu kama Dc Muro akiongea

- Udhaifu wa sauti hiyo ni kwamba kuna sehemu zinakatwa katwa kabisa kisha kinaanza kitu kingine kwa mbali ili ukisikiliza vizuri utasikia maneno ambayo pia Muongeaji pia akiomba wanasiasa kuacha kutengeneza migogoro ya ardhi kwa ajili ya kujipatia umaarufu

- Katika clip hiyo pia yanasikia maneno ambayo wanasiasa wa vyama vyote wanaombwa kushirikiana kuijenga ikungi na kufanya siasa za Maendeleo

- Katika clip hiyo pia inasikika sauti ambayo wajumbe walicheka pale ambapo sauti inasema mimi nawabatiza kwa maji na mama samia atawabatiza kwa moto kauli ambayo iliwafanya wajumbe wacheke kwa utani

HITIMISHO

Nataka kusema kuwa ule ulikuwa mkutano wetu wa chama wa ndani na ulifanyika katika ofisi za chama tawi la CCM Minyinga na sisi tulialika wazee maarufu na viongozi wa dini, tunaomba sana mambo yetu katika chama yasiingiliwe na wasio wa kwetu

Kama mna jambo na Dc Muro mumsubiri akiwa kwenye mikutano yake na Wananchi au katika ziara zake za kata na sio uku kwenye mambo yetu ya kichama

Tunamshukuru Dc Muro maana katika kikao kile cha ndani alitolea suluhu mgogoro wetu wa ardhi na muafaka ulipatikana, sisi kama chama tunaunga mkono jitihada za Dc Muro katika kutatua kero na kuwaletea wananchi Maendeleo

Dc Muro ameanza vizuri Ikungi, tunaendelea kumuunga mkono

Wenu katika utumishi,
Mika Lucas likapakapa
Mwenyekiti wa ccm Ikungi
16/07/2021

Screenshot_20210717-002804.png
 
CCM haijawahi kupigania maslahi ya umma.

Nyumba za serikali ziliuzwa zote na hakuna zilizojengwa kwa ajili ya wananchi wala viongozi zaidi ya kwenda Dodoma na kuanzisha jiji bila kujenga mipango bora na nyumba za NHC kwa ajili ya wananchi wa kawaida na wafanyabiashara kama wanazoishi wahindi kwenye majiji mengine zilizojengwa na Mkoloni na Nyerere.

CCM hawakupinga uuzwaji huo na uporaji huo wa Mali za umma na kuwamilikisha watawala ambao ni Walafi wa kila kitu chema kwa taifa kwa kutamani kuwa Mali zao na familia zao kwa kuungwa mkono na Chama huku wananchi wa kawaida wakibebeshwa mzigo wa kugharamikia pesa za pango kwa ajili ya watawala waliofuata mpaka Leo.

Likaja suala la kubadili magari kila linapokuja gari la kifahari. CCM wakakaa kimya huku wananchi wakiwa wanatwishwa mzigo wa watawala kutembelea misururu ya magari ya mabilioni ya fedha kwenda kuzindua choo cha shule cha shimo hata maeneo yenye maji wakati shule za mkoloni vilikua vyoo vinavyotumia maji na majumbani kwao na watoto wao hawatumii vyoo vya mashimo visivyo hata na maji wanatumia michanga kama jangwani kutawadha na makaratasi .
CCM hawaoni hayo wala hawajawahi kuzungumzia na wanaozungumzia kama Antony Mataka na Dialo wanalaaniwa na kupigwa vita mana sio kawaida ya CCM kukemea uovu wa serikali yao inayoumiza wananchi huku watoto wao wakiwa wanakalia Mali na kila aina ya ufahari kwa migongo ya wanyonge waliokosa mtetezi ndani ya CCM.

Likaja suala la Kikokotoo kwa wafanyakazi. Wakubwa walishiriki kupora mabilioni kwenye mifuko ya jamii kwa kujifanya wameikopesha serikali na kuacha madeni kwa serikali huku wafanyakazi wakiwa wanakosa stahiki zao na mwishowe wabunge wa CCM na CCM yao wakakubali kuwa mzigo ubaki kwa wafanyakazi wenye maisha duni wanaotegemea kulipwa vvinua mgongo vyao ili wainuke mana wale waadilifu walikua hawana uwezo wa kutumia mishahara midogo kusomesha watoto kujenga, kutunza familia na kulipa kodi na kujigharamikia usafiri na pango la nyumba kwa mishahara midogo hivyo wakawa wanategema kiinua mgongo ili wawape watoto wao waliowasomesha kwa jasho mitaji ili wajiajiri ,serikali ikaweka kikokotoo cha kuwaumiza wafanyakazi huku mawaziri na wabunge wakiwa wanalipwa viinwa mgongo kila baada ya miaka mirano na uzalendo kwa ukawa ni Sifuri.
Wao hawakuwekewa kikokotoo.
Hakuna CCM ya wazazi wala ya wazaliwa wala vijana au ya ujana wala ya Waikungi waliopinga dhulma iliyofanywa kwa wafanyakazi .

Leo wanasema wanataka maendeleo sio katiba. Hawajafika kwenye maofisi ya halmashauri wakaona mamilioni ya nakala za Katiba Pendekezwa yaliyozuiwa ili yasiwafikie wananchi wakazisoma na kujua jinsi katiba ilie Pendekezwa au ile ya warioba zilivyokua na Haki kwa wananchi wanaokamuliwa Kodi na Watawala wanaogeuka kuwa kama vile ndio wamiliki wa nchi hii.

Kikaja suala la Makato ya wanafunzi wa Chuo kikuu. CCM ilikaa kimya mpaka wapinzani wakapuga kelele. Wao wakaziba masikio.

Hivyo hakuna jema hata moja linalotokana na CCM wala wabunge wa CCM zaidi ya Kutengeneza uhalifu na kusikiliza kilio toka kwa wananchi na kisha kujifanya kuwa wanakuja kutoa msaada.

Katiba Mpya ni takwa la wananchi sio CCM mana wao wanaitumia ile ya zamani kujinufaisha Kwa dhulma.
Kama mfano wangekua wanaitumia kwa haki na kuongoza kwa haki hata pasingekua na katiba tungefuata vitabu vya dini na mila zetu kujiongoza tu mana pakiwa na haki hakuna haja ya Sheria Kali. Sheria inakua Kali kwa sababu ya wavunja Sheria kuwa wengi.
CCM wamefanya dhulma nyingi ndio mana watu wanahitaji Katiba itakayowabana waovu ndani ya serikali wanaitumia fedha za umma wanavyotaka huku wakiwaumiza wananchi kwa kodi.
Mabilioni ya fedha wanatumia kuagiza Magari ya kifahari na kuweka mafuta ya kuzurura Dodoma ,Mwanza ,Darisalam na kukimbiza Mwenge huku Wananchi wakikamuliwa pesa kwenye mafuta ili watawala wasiolipa kodi na wanaowekewa pesa za kupiga simu wakiwa wanaogelea kwenye fedha.
Haiwezekani kuwa na nchi yenye watu wa madaraja kwa kodi za maskini.

Tunataka katiba mpya ili tuwachague viongozi wenye uwezo kwa haki na wanaposhindwa kusimamia Rasilimali zetu tuwatoe kwa haki kwa kuwanyima kura kwa haki . Sio ule ujinga wa Mwaka 2020 uliotuletea Wabunge ,wenyeviti wa mitaa ,madiwani wanaoweka maslahi yao mbele na kuilinda serikali hata kwenye makosa kwa kulipa fadhila ya kuvuruga uchaguzi.

Katiba ni dira.
Kama tuna dira inayoshindwa kutufikisha tunapokwenda basi ni bora kuitupa na kutafuta dira mpya.

Viongozi wa dini wasiojua umuhimu wa katiba ni waajabu kabisa.

Hawajasoma katiba iliyopo inayokataza dini kwenye nchi hii kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini.

Wakati Katiba mpya imeweka bayana kuwa Tanzania ni Nchi isiyofungamana na dini yaoyote.

Kwa Katiba iluyopo siku akitokea Dikteta anayekula nyama za watu atafuta dini zote na kuwaweka gerezani maaskofu wote na mashekhe ndipo watakapojua kuwa katiba ni takwa la haki kwa wananchi na sio fadhila toka kwa Wakoloni weusi na Mabeberu wa karne ya 21 Afrika.
Iliyopo Tanzania ni nchi isiyokuwa na Dini. Kwa hiyo hakuna dini inayotambulika hivyo zilizopo serikali inaziacha tu kama fadhila.


Katiba Pendekezwa na ya Wananchi ya warioba iko vizuri inasema Tanzania ni Nchi isiyofungamana na dini yoyote.
Hivyo ni kusema kuwa serikali inatambua uwepo wa dini ila haifungamani na dini yoyote.
Hii ndiyo katiba tunayoitaka sio hiyo inayoweza kutuletea kiongozi asiye na dini yoyote na kuamua kufuta dini zote kwa kutumia katiba ya waovu ya CCM na wabunge wake wasiojali kesho ya watoto wa maskini wasiojua kingereza wala kichina pakitokea vurugu hawana pa kwenda ila watoto wao na wake zao hao viongozi watakimbilia Ulaya na Kwa wachina na wafaransa mana wao wanajua lugha zao.

Watanzania msitegemee CCM Maslahi wawatetee kamwe mpaka atokee tu Rais mwenye hulka ya upinzani kidogo.
Mana nilidokezewa kuwa kuna mmoja aliwahi kuwa NCCR mageuzi na Katibu wake alikua CUF wakajaribu kutetea tetea wananchi lakini aliponogewa akabadilika na kuwaangamiza wapinzani wenzake ili akubalike ndani ya CCM.
Hiyo ndiyo CCM.Haibadiliki zaidi ya kucheza na akili za watu wakidhani watu hawaoni hata mchana.
 
CCM haijawahi kupigania maslahi ya umma.

Nyumba za serikali ziliuzwa zote na hakuna zilizojengwa kwa ajili ya wananchi wala viongozi zaidi ya kwenda Dodoma na kuanzisha jiji bila kujenga mipango bora na nyumba za NHC kwa ajili ya wananchi wa kawaida na wafanyabiashara kama wanazoishi wahindi kwenye majiji mengine zilizojengwa na Mkoloni na Nyerere...
Naunga mkono hoja
 
UFAFANUZI WA KINACHOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU DC MURO

Mimi mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ikungi Ndugu Mika Lucas likapakapa naomba kuweka wazi ukweli wa tukio linalotajwa katika mitandao ya kijamii kuhusu Dc Muro..
DC Murro alisema ataua watu mchana kweupe, kwanini asingiziwe Murro usisingiziwe wewe?

Kama jambazi mkuu alikufa naye huyo jambazi mtoto hatoishi, bodi chini miguu juu
 
CCM haijawahi kupigania maslahi ya umma.

Nyumba za serikali ziliuzwa zote na hakuna zilizojengwa kwa ajili ya wananchi wala viongozi zaidi ya kwenda Dodoma na kuanzisha jiji bila kujenga mipango bora na nyumba za NHC kwa ajili ya wananchi wa kawaida na wafanyabiashara kama wanazoishi wahindi kwenye majiji mengine zilizojengwa na Mkoloni na Nyerere...
Nina sababu zaidi ya billion Moja za kuichukua CCM
 
UFAFANUZI WA KINACHOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU DC MURO

Mimi mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ikungi Ndugu Mika Lucas likapakapa naomba kuweka wazi ukweli wa tukio linalotajwa katika mitandao ya kijamii kuhusu Dc Muro...
Mwenyekiti.....yaani ulichofafanua ni kama vile katiba tunayoitaka itakavyokuwa.Tukushukuru saana kwa kutusaidia ktk juhudi za kuipata katiba mpya.

Atakalo MOLA binadamu hawezi lipinga.
 
Back
Top Bottom