Ufafanuzi wa hotuba ya "upotoshaji" ya Zitto kwa watanzania waishio Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi wa hotuba ya "upotoshaji" ya Zitto kwa watanzania waishio Marekani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, May 30, 2012.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  1. KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

  Katika hotuba yake anadai kwamba mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea hivi sasa unatokana na shinikizo la CHADEMA, Asasi za kiraia na viongozi wa dini.

  UFAFANUZI
  Huo ni upotoshaji mkubwa na wa wazi kabisa unaolenga kufuta historia sahihi ya mchakato wa uandikaji au upatikanaji wa Katiba Mpya unaoendelea hivi sasa.

  Ni jambo lililo dhahiri kabisa kwamba mchakato wa Katiba Mpya ni utekelezaji wa hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyoitoa katika salamu za kuaga mwaka 2010 kukaribisha mwaka 2011 na baadaye katika sherehe za Chama Cha Mapinduzi kutimiza miaka 34 Mjini Dodoma. Hili ndilo chimbuko halisi la hoja ya Katiba Mpya.

  Akitoa maamuzi hayo alisema Katiba iliyopo sasa ni nzuri, imetuvusha salama miaka hamsini iliyopita, tukiwa wamoja, imetujengea umoja wa Kitaifa. Lakini katika kipindi hicho hicho kumetokea mabadiliko mengi duniani na hapa nchini ya kisayansi, kiteknolojia, kitamaduni, kisiasa n.k. Hakuna shaka kwamba sasa tunahitaji Katiba Mpya itakayotuvusha miaka mingine 50 ijayo. Jambo hili Zitto Kabwe kalinukuu kwenye hotuba yake anaposema kuwa:-

  "Tanzania tunayoitaka kwa miaka mingine hamsini …." Mantiki hii ya miaka mingine 50 inatokana na hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya M. Kikwete sio yeye.


  1. KUHUSU UBADHIRIFU SERIKALINI
  Katika hotuba yake amedai kuwa CHADEMA ndio viongozi waliobeba dhamana ya mpito huu, kutoka Serikali ya kibadhirifu isiyojali watu mpaka Taifa lenye demokrasia iliyokomaa na lenye maendeleo na ustawi wa watu wake. (Developmental Democratic State).

  UFAFANUZI
  Kwanza CHADEMA haina "dhamana" ya uongozi wa nchi, mwenye dhamana ya uongozi wa nchi ni Chama Cha Mapinduzi ambacho kina Rais ambaye ni Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. CHADEMA wanachokitafuta ni Mob leadership ambayo ni fujo "Anarchy or law lessness" kitu ambacho huwezi kukidhibiti hata ukishika madaraka (mfano ni Libya, Mali, Algeria n.k.).

  Mob leadership ni fujo kwa sababu ina watu ambao hawana sera ya pamoja hawana wajibu wa kisheria, hawana maslahi ya kijamii na kidini, wanadai haki bila wajibu.

  Dhamana ya kuwafikisha watu katika Serikali ya kidemokrasia imo mikononi mwa Serikali iliyopo madarakani. Matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA yanaonyesha dhahiri kuwa hawathamini demokrasia ya nchi, umoja wa kitaifa wala amani na utulivu.
  Mfano:-

  1. Tamko la Mhe. Joshua Nassari la kumzuia Rais, Mkuu wa Nchi, asikanyage Mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania.


  1. Tamko la Mhe. Kabwe la kudai kuwa Wazanzibar wameporwa mafuta na gesi.


  1. Hata kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini mwaka 2009 CHADEMA ilitamka kwamba Mhe. Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu asikanyage Mbeya.


  1. Tamko la Mhe. Wenje kuwa Mwanza inajitosheleza kuwa nchi kwa rasilimali zake na hivyo kupendekeza serikali za majimbo ili Mwanza ijiendeshe yenyewe.

  Matamko haya hayawezi kutamkwa na kiongozi mmoja wa CHADEMA bila ridhaa ya Chama ama sivyo wangekuwa wanachukuliwa hatua na Chama chao.

  Kwa kuwa matamshi haya ni uhaini, uchochezi na ufashisti (ANARCHY). Kauli hizi zinaweza kupelekea machafuko katika nchi, mgawanyiko, ubaguzi, fujo na umwagaji damu, mambo ambayo yatamwathiri kila raia wa Tanzania bila kujali Chama chake cha kisiasa.

  Kwa hiyo, Chama Cha Mapinduzi ambacho kina dhamana ya uongozi wa nchi hii kinalaani matamshi hayo na kinawataka viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa matamshi ya hovyo na hatari kwa mstakabali wa Taifa letu. Chama Cha Mapinduzi kinaitaka Serikali kufuatilia matamshi haya kwa kina na itoe taarifa kwa wananchi.


  1. KUHUSU WATANZANIA KUTAKA UONGOZI MPYA

  Katika utangulizi wa hotuba yake amedai kuwa "watanzania kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu wameamka na kutaka mabadiliko ya kisiasa na hasa kutaka kabisa uongozi mpya wa nchi kutoka Chama kingine tofauti na Chama kinachoongoza hivi sasa."

  UFAFANUZI
  Chama kinachoongoza hivi sasa ni Chama Cha Mapinduzi "CCM" unapozungumza kauli kama hii lazima uangalie na hali halisi ya Chama chenyewe kama Taasisi.

  Kwanza, Chama Cha Mapinduzi kina wanachama hai wengi ambao ni watanzania kuliko CHADEMA.

  Pili, Chama Cha Mapinduzi kina mashabiki na wapenzi wastaarabu ambao ni watanzania wengi kuliko CHADEMA.

  Tatu, Chama Cha Mapinduzi katika mfumo wake hakijapata ombwe la uongozi, kina uongozi katika ngazi za Shina, Tawi, Kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa na hao wote ni watanzania. Na kama kuna Chama chenye heshima ya kuwasemea watanzania wote kila kona ni CCM sio Chama kingine chochote.

  Nne, katika uchaguzi wa ndani ya Chama wa mwaka 2012, watanzania wameendelea kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani ya CCM. Mpaka sasa Mashina yamekwishafanya uchaguzi kwa asilimia 97.56. Hao walioshiriki uchaguzi huo wa mashina ni watanzania.

  Tano, katika chaguzi ndogo za Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji CCM imeendelea kuongoza na wanaopiga kura nao ni wantanzania.

  Sita, Chama Cha Mapinduzi tangu 2007 kimefanikiwa kufungua matawi yake nje ya nchi maeneo mbalimbali mfano India, Uingereza na Marekani. Hao ni watanzania waishio katika ulimwengu wa kwanza na wanaamini kuwa CCM bado ni imara na hata Mhe. Rais alipoalikwa juzi kuhudhuria mkutano wa G8 alikutana na wanachama wa CCM Tawi la Marekani. Kitendo cha Mhe. Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kualikwa G8 ni heshima kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi na Taifa kwa kuwa kigezo cha kumwalika kilikuwa ni demokrasia, utawala bora, amani na utulivu nchini vigezo ambavyo vinavutia wawekezaji kutoka nje.

  Kwa hiyo, hoja ya Mhe. Zitto ni Batili (futile) kwa sababu anatazama kwa macho ya ubinafsi kwa lengo la kugombea Urais mwaka 2015.

  Uongozi mpya kabisa wa nchi ni upi? Kwa kuwa uongozi wa nchi yoyote huru na ya kidemokrasia unapatikana kwa utaratibu wa uchaguzi wa kawaida unaozingatia Katiba na Sheria za nchi katika mazingira ya uhuru na uwazi na vyama vyote vinashiriki. Afafanue maana ya uongozi mpya kabisa na namna utakavyopatikana huku akijua kabisa kwamba vyama vyote vya siasa vitakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi. Lazima utapata uongozi mchanganyiko kama ilivyo hivi sasa katika mfumo huu wa vyama vingi.


  1. KUHUSU SERA YA MADINI YA 2009 NA SHERIA YA MADINI YA 2010
  Katika hotuba yake amedai kuwa Tanzania haina sera ya Gesi asili na kwamba, sheria ya madini ya mwaka 2010 imetokana na shinikizo la CHADEMA na Asasi za kiraia.

  UFAFANUZI
  Chama Cha Mapinduzi katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo inapatikana katika website ya CCM www.ccm.or.tz katika ibara ya 55 ya ilani imeeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini kwa kipindi cha 2005/2010, ambayo ni pamoja na kukamilika kwa sera ya madini ya 2009 na kupitishwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010.

  Mhe. Kabwe mwaka 2009 alikuwa wapi kutoa mchango wake?

  Hoja hii ni ya CCM yeye na Chama chake wameidandia kwa malengo ya kibinafsi na sio maslahi ya nchi.


  1. SUALA LA URAIA WA NCHI MBILI (DUAL CITIZENSHIP)

  Mhe. Zitto anadai kwamba suala la uraia wa nchi mbili ni sera ya CHADEMA.

  UFAFANUZI
  Suala la uraia wa nchi mbili limekuwa ni sera ya Chama Cha Mapinduzi na limesimamiwa na Serikali yake, hususan Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.

  Katika hotuba ya bajeti ya 2011/2012 iliyotolewa na Mhe. Bernard Membe Bungeni katika Bunge la Nne kikao cha 31 cha tarehe 22 Julai, 2011 alisema:-

  "Ni dhamira ya Wizara yangu kuona suala la uraia wa nchi mbili linazinduliwa sanjari na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

  Watanzania mnapaswa kujua jinsi Zitto Kabwe anavyoiba hoja kwa manufaa binafsi alipowadanganya watanzania waishio nchini Marekani na dunia kwa ujumla akisema:-
  "CHADEMA inataka suala hili lifikie mwisho kwenye mjadala wa Katiba."

  Huo ni uwongo mkubwa na uzushi, kwa kuwa dhamira hiyo ni ya Serikali ya CCM na ilishawasilishwa na Waziri mwenye dhamana Bungeni na yeye akiwepo.

  6. HALI YA UCHUMI WA NCHI
  Amedai kuwa uchumi unaokuwa hivi sasa sio uchumi wa watanzania bali ni uchumi wa watu wachache kwenye sekta chache kama madini, mawasiliano na ujenzi; hivyo kupelekea watanzania wengi zaidi ya 15m kuishi chini ya Tshs. 500 kwa siku, kutokuwa na uhakika wa kula na kukabiliwa na mfumuko wa bei.

  UFAFANUZI
  Kwanza, takwimu zake sio za kitafiti kwani hazionyeshi chanzo. Pili hazina ulinganisho wa hali ya maisha ya wananchi wa nchi zinazotuzunguka ili uchungu alionao moyoni uonekane waziwazi kama ni kweli au ni uzushi.

  Mhe. Kabwe amepotosha kwa makusudi ya kulinda maslahi binafsi ya Urais wa 2015 kwa kuwa haiingii akilini kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama takwimu hizo yeye hajazisoma.

  Kwa mujibu wa kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2010 kilichotolewa na Wizara ya Fedha kukuwa kwa sekta ya kilimo kumeongezeka kwa 4.2% mwaka 2010 tofauti na asilimia 3.2% mwaka 2009. Lakini katika taarifa yake anadai kuwa uchumi wa vijijini ambako ndiko kwenye kilimo umekuwa kwa asilimia moja tu (flat lining).

  Katika uchambuzi wake wa hali ngumu ya uchumi na mfumuko wa bei kama angelinganisha na nchi jirani angegundua kuwa mfumuko wa bei kwa Tanzania upo chini zaidi kwa asilimia 19 ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka ambao mfumuko ni mkubwa zaidi mfano Ethiopia ni 30%.

  Katika hali halisi ya maisha ya watanzania wa vijijini chakula chao hakitokani na pesa, wanakula vitu vingi ambavyo haviingii kwenye takwimu za uchumi mfano, kuku, mayai, maziwa, mihogo, viazi vitamu, nyama n.k. Hivyo vinaliwa bila kuingia kwenye mzunguko wa soko ndio maana hakuna mtanzania anayekufa njaa. Lakini nchi jirani wanakufa njaa na wanakimbia nchi zao kwa njaa. Mfumuko wa bei ni tatizo la Dunia nzima sio Tanzania peke yake.

  Huyu ni mgombea Urais wa aina gani ambaye si mkweli kwa nchi yake, hasomi takwimu na anaropoka mambo ya ndani ya nchi hovyo hovyo duniani.

  7. SUALA LA FURSA YA ELIMU
  Katika hotuba yake ameeleza kuwa "leo mtoto wa maskini Tanzania hapati elimu anayopata mtoto wa mwenye uwezo." Na kwamba Tanzania ijiandae kupokea bomu litakaloletwa na kundi kubwa la vijana wasio na elimu wala ujuzi."

  UFAFANUZI
  Huo ni uwongo na uzushi unaolenga kutetea maslahi binafsi. Kwa kuwa katika uchambuzi wake amejikita kwenye shule binafsi na sio shule za serikali ambazo zipo katika vijiji vyote Tanzania, vinatoa elimu huru, sawa na bila ubaguzi.

  Serikali ya Tanzania imetoa fursa ya Elimu kwa kila mtoto wa Tanzania tangu awali. Mpaka imefikia wakati hata mabinti wa kazi za ndani (house girls) hawapatikani wote wapo mashuleni.

  Kuthibitisha hilo mnamo tarehe 20/9/2010 Tanzania ilipata tuzo ya utekelezaji mzuri wa miradi ya Elimu katika ngazi za awali, elimu ya msingi na sekondari kutoka umoja wa mataifa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokea Tuzo hizo Mjini New York.

  Hivi huyu Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA anakuwa wapi asiyaone haya mpaka kwenda kuwadanganya watanzania waishio Marekani huko huko ilikotolewa Tuzo?

  Serikali ya CCM imejenga Vyuo vya kutosha vinavyozalisha wasomi wa kutosha na hata bomu tunalojiandaa kulikabili ni la vijana wasomi ambao hawana ajira na sio vijana wasio na elimu kama anavyodai yeye.

  IMETOLEWA NA TAWI LA CCM MAKAO MAKUU
  DODOMA
  28/05/2012
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Magamba hamna cha kujadili kuokoa chama chenu kinazama, mnapoteza muda kuijadili peopless power, pamoja na nape wenu anaye endelea kukiua chama chenu. Mtabaki kupakaza maneno ya uzushi.mafuta ya wazanzibari yatabaki kuwa ya wazanzibari. Peoplessssssssssssssssssssss poweeeeer
   
 3. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  hahahahaaaaa...!!!. kama kweli zote ni sera za ccm mbona hakuna kilichofanyika ndani ya miaka 35 ya uwepo wa ccm?
  Sema nyie leongo lenu ni kujionyesha mnapinga kila kitu. ccm sio muwe mnapinga kila kitu bali kufanyia kazi ushauri mnaopewa na CHADEMA.
  Naomba mtoe ufafanuzi kwanini mumeshindwa kujivua magamba ndani ya siku 90 mlizosema(chenge, lowasa,rostam azizi, kikwete na nape).
   
 4. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Ndani ya tamko hili kuna hasira,chuki,wivu na mwendelezo wa uzandiki.Hivi suala la elimu kwa mfano unahitaji kuambiwa kuwa elimu yetu hivi sasa ni ya makundi makundi?Kama ni kweli watu wote yaani watoto wa maskini wa vijijini na vigogo wa ccm waliopo Dodoma na Dar,wanaenda kwenye hizo shule anazotamka kweli?Wanagapi ni watoto wa vigogo na matajiri wanaenda shule za St Marian,St Fransis badala ya kwenda shule ya Ikwiriri au Makambako,au Kazuramimba kule kigoma?Mtoto gani wa kigogo wa ccm anaenda shule hizo?Tamko ni batili.

  Tazama suala la kufa njaa.Hivi kweli kule Dodoma hawalii njaa watanzania hawa?Saula la kuishi chini ya mia 500 hivi ni kweli hawajaona kuna watu hata kuipata 100 ni kasheshe?Kama wanataka kushuhudia haya waje mtaani.Tatizo ni kutembea kwa kutumia magari ya viyoyozi.Huoni joto la nje.
  Hizi ni propaganda na nadhani limekuja pabaya juu ya hotuba hii.
   
 5. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ujinga mtupu!
   
 6. B

  Beethoven JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa hoja ya katiba bora CCM mkae kimya.

  Atuambie kwanini
  1)haikuwekwa kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010!!!
  2) haikuzungumzwa hata kwa bahati mbaya kama ahadi za mgombea wa CCM kwenye kampeni!!!!
  3) mgombea wa CCM alipotengeneza mdahalo feki aliulizwa watanzania wategemee kumkumbuka kwa lipi-mbona alijikanyaga sana asiseme kwa katiba mpya!!!!
  4) Waziri wa sheria na mwanasheria mkuu walipinga hadharani suala la hoja ya katiba mpya-huu mkanganyiko ulitokea wapi kama kulikuwa na dhamira???
  5)mchakato wa kufanya mikutano Dodoma, Dar na Zanziba tulishuhudia makada wamekusanya watoto wazibe nafasi ili watu wasitoe maoni-kwa hujuma kama hizi dhamira iko wapi??

  Tafuteni cha kuzungumza ila kwa suala la katiba mlidandia treni ya umeme kwa mbele ikiwa kasi na mkianguka mnafikia kwenye reli yenye umeme ~1000KV!!!

  Mmekwisha tu!
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona twiga wanapotoroshwa hamji na kasi kama hii kukanusha? mtasema na sera ya mgombea binafsi ya kwenu pia. wapi katika ilani yenu kuna kipengele cha katiba mpya? safari yenu imewadia
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nilifikiri ni mtu tu kazuka na kuandika hizi porojo kumbe ni official response ya CCM?

  Sasa ndugu mleta hoja, naomba utuambie hoja ya katiba mpya iko kwenye ukarasa gani wa ilani ya chama cha mapinduzi 2010-15. Au ni number ngapi kwenye orodha ya ahadi za mgombea na sasa ni rais (alitoa ahadi 67), hiii ya katiba mpya iko number ngapi?

  Tuanzie hapo halafu ndio tuendelee na hizo porojo nyingine. Nitata hasa kujikita kwenye uchumi. Jibu swali, katiba mpya iko wapi kwenye ilani ya CCM?
   
 9. h

  hamsinij JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona tunasahau mapema? Cuf walikufa 2001 wakidai mambo 4 ikiwemo katiba mpya, tume huru, muungano na serikali za majimbo
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  aaaa,mdau mbona unawaambia ukweli hivi?????
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  labda atakuja na jibu.....namsubiri hapa siondoki Ng'o!!!!
   
 12. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  UFAFANUZIWA MAMBO MBALIMBALI YALIYOPOTOSHWA NA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE – NAIBU KATIBUMKUU WA CHADEMA KATIKA HOTUBA YAKE ALIYOITOA KWA WATANZANIA WAISHIO NCHINIMAREKANI  1. KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

  Katika hotuba yake anadai kwamba mchakato wa Katiba Mpyaunaoendelea hivi sasa unatokana na shinikizo la CHADEMA, Asasi za kiraia naviongozi wa dini.

  UFAFANUZI
  Huo ni upotoshaji mkubwa na wa wazi kabisa unaolengakufuta historia sahihi ya mchakato wa uandikaji au upatikanaji wa Katiba Mpyaunaoendelea hivi sasa.

  Ni jambo lililo dhahiri kabisa kwamba mchakato wa KatibaMpya ni utekelezaji wa hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyoitoakatika salamu za kuaga mwaka 2010 kukaribisha mwaka 2011 na baadaye katikasherehe za Chama Cha Mapinduzi kutimiza miaka 34 Mjini Dodoma. Hili ndilo chimbuko halisi la hoja ya KatibaMpya.

  Akitoa maamuzi hayo alisema Katiba iliyopo sasa ninzuri, imetuvusha salama miaka hamsini iliyopita, tukiwa wamoja, imetujengeaumoja wa Kitaifa. Lakini katika kipindihicho hicho kumetokea mabadiliko mengi duniani na hapa nchini ya kisayansi,kiteknolojia, kitamaduni, kisiasa n.k. Hakuna shaka kwamba sasa tunahitaji Katiba Mpya itakayotuvusha miakamingine 50 ijayo. Jambo hili Zitto Kabwekalinukuu kwenye hotuba yake anaposema kuwa:-

  “Tanzania tunayoitaka kwa miaka mingine hamsini ….”Mantiki hii ya miaka mingine 50 inatokana na hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya M.Kikwete sio yeye.

  2. KUHUSU UBADHIRIFU SERIKALINI
  Katika hotuba yake amedai kuwa CHADEMA ndio viongoziwaliobeba dhamana ya mpito huu, kutoka Serikali ya kibadhirifu isiyojali watumpaka Taifa lenye demokrasia iliyokomaa na lenye maendeleo na ustawi wa watuwake. (Developmental Democratic State).

  UFAFANUZI
  Kwanza CHADEMA haina “dhamana” ya uongozi wa nchi,mwenye dhamana ya uongozi wa nchi ni Chama Cha Mapinduzi ambacho kina Raisambaye ni Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. CHADEMA wanachokitafuta ni Mob leadershipambayo ni fujo “Anarchy or law lessness” kitu ambacho huwezi kukidhibiti hataukishika madaraka (mfano ni Libya, Mali, Algeria n.k.).

  Mob leadership ni fujo kwa sababu ina watu ambao hawanasera ya pamoja hawana wajibu wa kisheria, hawana maslahi ya kijamii na kidini,wanadai haki bila wajibu.

  Dhamana ya kuwafikisha watu katika Serikali yakidemokrasia imo mikononi mwa Serikali iliyopo madarakani. Matamshiyanayotolewa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA yanaonyesha dhahiri kuwa hawathaminidemokrasia ya nchi, umoja wa kitaifa wala amani na utulivu.
  Mfano:-(i) Tamko la Mhe. Joshua Nassari la kumzuia Rais, Mkuu wa Nchi, asikanyageMikoa ya Kaskazini mwa Tanzania.

  (ii) Tamko la Mhe. Kabwe la kudai kuwa Wazanzibar wameporwa mafuta na gesi.

  (iii) Hatakwenye uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini mwaka 2009 CHADEMA ilitamka kwamba Mhe.Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu asikanyage Mbeya.
  (iv) Tamkola Mhe. Wenje kuwa Mwanza inajitosheleza kuwa nchi kwa rasilimali zake na hivyokupendekeza serikali za majimbo ili Mwanza ijiendeshe yenyewe.
  Matamko haya hayawezi kutamkwa na kiongozi mmoja waCHADEMA bila ridhaa ya Chama ama sivyo wangekuwa wanachukuliwa hatua na Chamachao.
  Kwa kuwa matamshi haya ni uhaini, uchochezi na ufashisti(ANARCHY). Kauli hizi zinaweza kupelekea machafuko katika nchi, mgawanyiko,ubaguzi, fujo na umwagaji damu, mambo ambayo yatamwathiri kila raia wa Tanzaniabila kujali Chama chake cha kisiasa.
  Kwa hiyo, Chama Cha Mapinduzi ambacho kina dhamana yauongozi wa nchi hii kinalaani matamshi hayo na kinawataka viongozi wa vyama vyasiasa waache kutoa matamshi ya hovyo na hatari kwa mstakabali wa Taifaletu. Chama Cha Mapinduzi kinaitakaSerikali kufuatilia matamshi haya kwa kina na itoe taarifa kwa wananchi.

  3. KUHUSU WATANZANIA KUTAKAUONGOZI MPYA

  Katika utangulizi wa hotuba yake amedai kuwa “watanzaniakuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu wameamka na kutakamabadiliko ya kisiasa na hasa kutaka kabisa uongozi mpya wa nchi kutoka Chamakingine tofauti na Chama kinachoongoza hivi sasa.”

  UFAFANUZI
  Chama kinachoongoza hivi sasa ni Chama Cha Mapinduzi“CCM” unapozungumza kauli kama hii lazima uangalie na hali halisi ya Chamachenyewe kama Taasisi.

  Kwanza, Chama Cha Mapinduzi kina wanachama hai wengiambao ni watanzania kuliko CHADEMA.

  Pili, Chama Cha Mapinduzi kina mashabiki na wapenziwastaarabu ambao ni watanzania wengi kuliko CHADEMA.

  Tatu, Chama Cha Mapinduzi katika mfumo wake hakijapataombwe la uongozi, kina uongozi katika ngazi za Shina, Tawi, Kata, Jimbo,Wilaya, Mkoa na Taifa na hao wote ni watanzania. Na kama kuna Chama chenye heshima yakuwasemea watanzania wote kila kona ni CCM sio Chama kingine chochote.

  Nne, katika uchaguzi wa ndani ya Chama wa mwaka 2012,watanzania wameendelea kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani yaCCM. Mpaka sasa Mashina yamekwishafanyauchaguzi kwa asilimia 97.56. Haowalioshiriki uchaguzi huo wa mashina ni watanzania.

  Tano, katika chaguzi ndogo za Kata, Vijiji, Mitaa naVitongoji CCM imeendelea kuongoza na wanaopiga kura nao ni wantanzania.

  Sita, Chama Cha Mapinduzi tangu 2007 kimefanikiwakufungua matawi yake nje ya nchi maeneo mbalimbali mfano India, Uingereza naMarekani. Hao ni watanzania waishio katikaulimwengu wa kwanza na wanaamini kuwa CCM bado ni imara na hata Mhe. Raisalipoalikwa juzi kuhudhuria mkutano wa G8 alikutana na wanachama wa CCM Tawi laMarekani. Kitendo cha Mhe. Rais ambayeni Mwenyekiti wa CCM Taifa kualikwa G8 ni heshima kubwa kwa Chama Cha Mapinduzina Taifa kwa kuwa kigezo cha kumwalikakilikuwa ni demokrasia, utawala bora, amani na utulivu nchini vigezo ambavyovinavutia wawekezaji kutoka nje.

  Kwa hiyo, hoja ya Mhe. Zitto ni Batili (futile) kwasababu anatazama kwa macho ya ubinafsi kwa lengo la kugombea Urais mwaka 2015.

  Uongozi mpya kabisa wa nchi ni upi? Kwa kuwa uongozi wa nchi yoyote huru na yakidemokrasia unapatikana kwa utaratibu wa uchaguzi wa kawaida unaozingatiaKatiba na Sheria za nchi katika mazingira ya uhuru na uwazi na vyama vyotevinashiriki. Afafanue maana ya uongozimpya kabisa na namna utakavyopatikana huku akijua kabisa kwamba vyama vyote vyasiasa vitakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi. Lazima utapata uongozi mchanganyiko kama ilivyo hivi sasa katika mfumohuu wa vyama vingi.

  4. KUHUSU SERA YA MADINI YA 2009NA SHERIA YA MADINI YA 2010
  Katika hotuba yake amedai kuwa Tanzania haina sera yaGesi asili na kwamba, sheria ya madini ya mwaka 2010 imetokana na shinikizo laCHADEMA na Asasi za kiraia.

  UFAFANUZI
  Chama Cha Mapinduzi katika ilani yake ya uchaguzi yamwaka 2010 ambayo inapatikana katika website ya CCM Welcome to the Frontpage! katika ibaraya 55 ya ilani imeeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini kwakipindi cha 2005/2010, ambayo ni pamoja na kukamilika kwa sera ya madini ya2009 na kupitishwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010.

  Mhe. Kabwe mwaka 2009 alikuwa wapi kutoa mchango wake?

  Hoja hii ni ya CCM yeye na Chama chake wameidandia kwamalengo ya kibinafsi na sio maslahi ya nchi.

  5. SUALA LA URAIA WA NCHI MBILI (DUALCITIZENSHIP)

  Mhe. Zitto anadai kwamba suala la uraia wa nchi mbili nisera ya CHADEMA.

  UFAFANUZI
  Suala la uraia wa nchi mbili limekuwa ni sera ya ChamaCha Mapinduzi na limesimamiwa na Serikali yake, hususan Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.

  Katika hotuba ya bajeti ya 2011/2012 iliyotolewa na Mhe.Bernard Membe Bungeni katika Bunge la Nne kikao cha 31 cha tarehe 22 Julai,2011 alisema:-

  “Ni dhamira ya Wizara yangu kuona suala la uraia wa nchimbili linazinduliwa sanjari na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

  Watanzania mnapaswa kujua jinsi Zitto Kabwe anavyoibahoja kwa manufaa binafsi alipowadanganya watanzania waishio nchini Marekani nadunia kwa ujumla akisema:-“CHADEMA inataka suala hili lifikie mwisho kwenyemjadala wa Katiba.”

  Huo ni uwongo mkubwa na uzushi, kwa kuwa dhamira hiyo niya Serikali ya CCM na ilishawasilishwa na Waziri mwenye dhamana Bungeni na yeyeakiwepo.

  6. HALI YA UCHUMI WA NCHI
  Amedai kuwa uchumi unaokuwa hivi sasa sio uchumi wawatanzania bali ni uchumi wa watu wachache kwenye sekta chache kama madini,mawasiliano na ujenzi; hivyo kupelekea watanzania wengi zaidi ya 15m kuishichini ya Tshs. 500 kwa siku, kutokuwa na uhakika wa kula na kukabiliwa namfumuko wa bei.

  UFAFANUZI
  Kwanza, takwimu zake sio za kitafiti kwani hazionyeshichanzo. Pili hazina ulinganisho wa haliya maisha ya wananchi wa nchi zinazotuzunguka ili uchungu alionao moyoniuonekane waziwazi kama ni kweli au ni uzushi.

  Mhe. Kabwe amepotosha kwa makusudi ya kulinda maslahibinafsi ya Urais wa 2015 kwa kuwa haiingii akilini kuwa Naibu Katibu Mkuu waChama takwimu hizo yeye hajazisoma.

  Kwa mujibu wa kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katikamwaka 2010 kilichotolewa na Wizara ya Fedha kukuwa kwa sekta ya kilimokumeongezeka kwa 4.2% mwaka 2010 tofauti na asilimia 3.2% mwaka 2009. Lakini katika taarifa yake anadai kuwa uchumiwa vijijini ambako ndiko kwenye kilimo umekuwa kwa asilimia moja tu (flatlining).

  Katika uchambuzi wake wa hali ngumu ya uchumi na mfumukowa bei kama angelinganisha na nchi jirani angegundua kuwa mfumuko wa bei kwaTanzania upo chini zaidi kwa asilimia 19 ukilinganisha na nchi zinazotuzungukaambao mfumuko ni mkubwa zaidi mfano Ethiopia ni 30%.

  Katika hali halisi ya maisha ya watanzania wa vijijinichakula chao hakitokani na pesa, wanakula vitu vingi ambavyo haviingii kwenyetakwimu za uchumi mfano, kuku, mayai, maziwa, mihogo, viazi vitamu, nyaman.k. Hivyo vinaliwa bila kuingia kwenye mzungukowa soko ndio maana hakuna mtanzania anayekufa njaa. Lakini nchi jirani wanakufa njaa nawanakimbia nchi zao kwa njaa. Mfumuko wabei ni tatizo la Dunia nzima sio Tanzania peke yake.

  Huyu ni mgombea Urais wa aina gani ambaye si mkweli kwanchi yake, hasomi takwimu na anaropoka mambo ya ndani ya nchi hovyo hovyoduniani.

  7. SUALA LA FURSA YA ELIMU
  Katika hotuba yake ameeleza kuwa “leo mtoto wa maskiniTanzania hapati elimu anayopata mtoto wa mwenye uwezo.” Na kwamba Tanzaniaijiandae kupokea bomu litakaloletwa na kundi kubwa la vijana wasio na elimuwala ujuzi.”
  UFAFANUZI
  Huo ni uwongo na uzushi unaolenga kutetea maslahibinafsi. Kwa kuwa katika uchambuzi wakeamejikita kwenye shule binafsi na sio shule za serikali ambazo zipo katikavijiji vyote Tanzania, vinatoa elimu huru, sawa na bila ubaguzi.

  Serikali ya Tanzania imetoa fursa ya Elimu kwa kilamtoto wa Tanzania tangu awali. Mpakaimefikia wakati hata mabinti wa kazi za ndani (house girls) hawapatikani wotewapo mashuleni.

  Kuthibitisha hilo mnamo tarehe 20/9/2010 Tanzaniailipata tuzo ya utekelezaji mzuri wa miradi ya Elimu katika ngazi za awali,elimu ya msingi na sekondari kutoka umoja wa mataifa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokea Tuzo hizoMjini New York.

  Hivi huyu Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA anakuwa wapiasiyaone haya mpaka kwenda kuwadanganya watanzania waishio Marekani huko hukoilikotolewa Tuzo?

  Serikali ya CCM imejenga Vyuo vya kutosha vinavyozalishawasomi wa kutosha na hata bomu tunalojiandaa kulikabili ni la vijana wasomiambao hawana ajira na sio vijana wasio na elimu kama anavyodai yeye.

  IMETOLEWANA TAWI LA CCM MAKAO MAKUUDODOMA 28/05/2012
   
 13. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ccm wanatapatapa tu wameshashikwa sehemu za siri
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,645
  Likes Received: 21,857
  Trophy Points: 280
  Kuhusu katiba mpya, Mwanasheria mkuu wa serikali na aliyekuwa Waziri wa sheria Kombani walitamka nini kwa nyazifa zao kuhusu katiba mpya? mbona chama wala serikali havikukana matamko yao wala kuwaadabisha? ni kwa vile ule ulikuwa ni msimamo wa chama chao.
  Ni kweli yanayojitokeza sasa ni shinikizo la Chadema na asasi zingine za kiraia na CCM ikawa haina pa kutokea.
   
 15. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 929
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Hata wao wenyewe CCM hawaamini wayasemayo kwa sasa.
  Nani asiyejua kuwa katiba mpya haikuwa kwenye ilani ya CCM?
  Nani asiyekumbuka kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria wa wakati huo (Kombani) walitoa tamko la kusema katiba mpya haitakiwi?
  Nani asiyekumbuka kuwa muswada wa kwanza ulipopelekwa bungeni ulikuwa wa kurekebisha katiba na si kuandika katiba mpya mpaka Chadema walipogoma?
  Nani asiyekumbuka kuwa hata baada ya kurekebisha muswada huo na kuleta mpya bungeni lakini ukiwa na mapungufu makubwa, Chadema waligoma tena na ndipo Jk akawaita Ikulu na kufumua kila kitu?
  Nani asiyekumbuka kuwa hata baada ya kupitishwa na kuwa sheria haikutumika na wala tume haikuteuliwa mpaka pale uliporudishwa bungeni na kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuruhusu tume kuteuliwa?

  Mambo mengine CCM waone aibu! Huku si kuiba agenda ya Chadema, ni kukwapua agenda kama kibaka.
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  zitto ni waziri kivuli na aliyejibu ni nani?
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  Aliyeandika hili tamko atakuwa ni yule mzinzi wa Iramba anasingizia tawi dogo la dodoma!
   
 18. Alonick Antony

  Alonick Antony Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM mtajibeba safari hii
   
 19. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  HATA KAMA CHAMA KINAKUFA SIO VIZURI KUVUA NGUO ZENU ZA NDANI AMBAZO NI CHAFU NAMNA HII MBELE ZA WATU TENA WATU WAZIMA JAMANI HIKI NI KINYAAAA SISI SOTE TUNAUJUA UKWELI

  ACHENI KUHARISHA HADHARANI CCM IMEKWISHA NA INAKWENDA ZAKE SASA MSIENDE NAYO NDIO MAANA MNAAMBIWA VUENI GAMBA VAENI GWANDA

  m4c kwa ukombozi wetu PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Well said.
   
Loading...