Ufafanuzi tafadhali: Je, hii ni ngozi halisi ya chui?

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,024
24,374
Wajuzi wa mambo tafadhali, hebu kwa wanaoelewa na kujua watufafanulie na kutujuza hili jambo!

Katika ufunguzi wa tamasha la utamaduni Rais Samia Suluhu alivishwa vazi la kabila la wachaga lenye rangi za chui na Chief(Mangi) Marealle ambaye nae pia alikuwa amevaa vazi la aina hiyo!

Sasa je yale mavazi ni kweli yametengenezwa kwa ngozi halisi ya chui au ni nakshi tu. Na kama ni ngozi halisi ya chui, hao chui wanapatikanaje na kwa utaratibu gani maana tunajua chui ni miongoni mwa nyara za taifa.

Wenye historia au namna halisi ya utengenezaji wa hilo vazi tafadhali watujuze!

IMG_8862.jpg
 
Ni halisi kabisa, sema hizo Ni za mamangi wa zamani wamerithishana kabla Sheria za kuzuia uwindaji wa hao leopards kuundwa
 
Ni halisi kabisa,sema hizo Ni za mamangi wa zamani wamerithishana kabla Sheria za kuzuia uwindaji wa hao leopards kuundwa

Kama ni za zamani si zingekuwa zimepoteza ubora mkuu na kunyonyoka manyoya...maana ngozi aliyoivaa Mangi miaka ya 50 huko sidhani kama muonekano wake ungekuwa kama zilivyokuwa leo hii!

Mfano vazi walilomvisha Hangaya, je ile ni ngozi ya chui iliyochunwa miaka ya 50 au 60 huko?
 
Pengine labda Kuna namna wanazitunza zisiharibike au Kuna utaratibu wanaofuata kwenye mamlaka husika kupewa vibali vya kuwinda kwa masharti wanayowajua wao!

Au labda chui wanaojifia huko porini wanaomba vibali wanachuna ngozi

Mi sijui nawaza tu
 
Kwani chui ni immortal kuwa hawafi na ngozi zao kupatikana? Sasa kama tamasha limeandaliwa na wizara ya serikali u adhani wanakosa pa kupata ngozi ya chui?

Kwanini hujashangaa "wachaga" wametoa zawadi ya ngamia ilihali sio moja ya wanyama wanaowafuga. Na hata kihistoria hawajawahi kuwafuga?
 
Ngamia upareni wapo...!!
 
Kama ni za zamani si zingekuwa zimepoteza ubora mkuu na kunyonyoka manyoya...maana ngozi aliyoivaa Mangi miaka ya 50 huko sidhani kama muonekano wake ungekuwa kama zilivyokuwa leo hii!

Mfano vazi walilomvisha Hangaya, je ile ni ngozi ya chui iliyochunwa miaka ya 50 au 60 huko?
Chui wanauzwa, wenda wamenunua

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom