Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Habari great thinkers, nilikua na mpango wa kufungua Duka la urembo na vitenge dodoma wazoefu nelezeni sehemu gani zimechangamka kibiashara , bei za frame ili napokuja for market research my work can be easier.
 
Habari wana jamii,

Mimi ni mdada mwenye miaka 32, nimechoka na kazi za kuajiriwa nimefikiria nifanye kitu gani nikapata wazo la kufungua cosmetics shop lakini sina idea yeyote, kwahiyo naomba kwa mzoefu anisaidie kiasi cha mtaji cha chini ninachopaswa kuanzia,napia anisaidie nivitu gani ambavyo vinauzika zaidi na niwapi naweza kwenda kununua mzigo. Mimi naishi ubungo dar. Asanteni mbarikiwe.
 
Mimi nina wazo kama lako. Ila nikakosa muongozo. Tufahamiane ili tushauriane. Watu humu wanapita bila kujali
 
Mimi nina wazo kama lako. Ila nikakosa muongozo. Tufahamiane ili tushauriane. Watu humu wanapita bila kujali
Hajataka kufahamiana na mtu bali information kuhusu biashara ya cosmetics haswa kwa ambaye anaifanya au ana idea nayo, wewe unataka kunfahamu mtu au kupata idea ya cosmetic business? Acha usanii
 
Hajataka kufahamiana na mtu bali information kuhusu biashara ya cosmetics haswa kwa ambaye anaifanya au ana idea nayo, wewe unataka kunfahamu mtu au kupata idea ya cosmetic business? Acha usanii
Umewaza mbali sana ndugu yangu. Pengine nami nimekosea kuandika. Sina Maana ya kumtaka.
 
Hongera, ukianza na 1milioni si vibaya hata chini ya hapo kinachotakiwa fungua mlango ili ujue watu wanahitaji nini. Anza na pafyumu, lotions, brazilian hairs, shapoo.

Njia rahisi ya kujua mahitaji ni kufikiria kama kuna saloon za kike jirani zingehitaji vitu gani vya haraka haraka. Pia fikiria hasa akina dada ili wapendeze wanapendelea watoke vipi, e.g mikoba, viatu, bangili, hereni, mikufu-hivi utakuwa unaviongeza dukan kwako siku zijazo kadri ya uhitaji sio mwanzoni kwani ni gharama kubwa kiasi.

Kwa hapo Dar maduka ya jumla ya vipodozi nenda kariakoo ukifika kituo cha mafuta cha Big bon vuka barabara upande wa pili kuna gorofa linatazamana na hicho kituo, usifike msimbazi polisi station (sijashika jina la mtaa) nyuma ya hilo ghorofa kuna kabaraba kana maduka kibao. Zamani kidogo ilikuwa ni stand ya kushushia abiria wanaotokea mwenye na ubungo-sijaja Dar muda.

NB: Unaponunua au kuuza vipodozi:
  • Hakiki expire date
  • Uwe na vibali au jitahidi ukamilishe mchakato miezi michache ijayo kibali toka TFDA. Hii isikuzuie kufungua sasa lakini
  • Ujikite kujua vipodozi ambavyo nchini vimepigwa marufuku tusije tukakukosa JF kisa vipodozi haramu mfano Carolite, epiderm. Wengine wataongezea.

All the best
 
Nini ungependa kufahamishwa zaidi ili nisaidie mawazo kuliko kushusha lecture ya hata yale usiyotaka kuyafahamu kwani biashara hii ina mambo lukuki.

Cha msingi ni mtaji,location,soko na bidhaa husika zilizo kwenye soko kwa wakati husika
 
Jamani mm naomba ushauri nahitaji kwenda Mozambique kwa biashara za kutengeneza kucha,kupaka rangi pamoja na kubandika kope,naombeni ushauri wenu kama inalipa na sehemu gani inaweza kufaa
 
Wazo zuri ila ufahamu kabisa katika Mikoa yao sijui 11 au 9 vile wapi panalipa! Ila usije ukaenda Nangade cabo del gado asee! Biashara haitakua nzuri sababu hapo mkoa wa kaskazini wengi ni waumini wa dini yetu so biashara itayumba.. Nenda nampula, pemba, maputo etc.
 
Ww ni mwenyeji wa pande hizo
 
Njoo nkuuzie raba simple za kumetisha na jeans kwa bei poa kabixa ya sh 4500 kwa pc ukauze mtaani kuanzia 10,000 na zinatoka bila taabu
 
Habari wana jamvi,

Natarajia kufanya biashara hii ya duka la vipodozi kwa mkoa wa arusha, naomba kufahamu angalau kidogo kwa wenzangu wanao fanya biashara hii, mzigo huwa mnachukulia wapi, na changamoto zake pia zikoje.
 
Mzigo popote mkuu changamoto kubwa, bidhaa ni ya expire date hivo ni lazima ule hasara ya robo au hata nusu mtaji pindi kila ifikapo expire date.
 
Mzigo popote mkuu changamoto kubwa, bidhaa ni ya expire date hivo ni lazima ule hasara ya robo au hata nusu mtaji pindi kila ifikapo expire date.

Tatizo wafanyabiashara wagumu sana kama wavuvi. Mtu anajua bidhaa fulani itaexpire baada ya mwezi mmoja lkn utakuta anauza bei ile ile. Kwanini usifanye punguzo kwa bidhaa ambazo zimebaki mwezi mmoja kuisha matumizi? Hii itasaidia kurudisha fedha yako angalau kidogo. Km lotion inauzwa 10,000 unafanya hata 5,000.
 
Back
Top Bottom