Geofrey_GAMS
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 496
- 228
Uko maeneo gani mkuu?
Niko Cabodelgado babu!! Unauzoefu wowote unisaidie?uko maeneo gani mkuu
Capo delgado hivi ipo wapi
Niko Cabodelgado babu!! Unauzoefu wowote unisaidie?
Biashara yoyote, ianza kutokana na mtaji wako ila kiukweli biashara ya vipodozi unahitajika uwe na mtaji mkubwa kidogo ili uwe japo na kila aina ya kipodozi, lakini pia ni vyema ujue ni aina gani ya kipodozi vinatoka sana!
Pale Kariakoo, wanapo nunua vipodozi vya jumla ili kwenda kuviuza rejareja mtaani, taratibu ukizoea na wakikuzoea utapata na vile vipodozi vilivyopigwa marufuku, ambavyo kikweli ndio vinafaida kubwa ukienda kuuza dukani kwako!
Swala la lesni zake, kwa maduka ya rejareja hilo silijui lipo vipi, nadhani watakuja wanaojua zaidi watakupa majawabu!
Fanya hivi;-
Nenda Kariakoo, kuna eneo linaitwa Sabasaba lipo oppst na fuel station ya bigbon ukivuka ukiuvuka mtaa wa msimbazi (ulizia maduka ya mama mmoja anaitwa Sharifa) yeye ni importer mkubwa sana wa vipodozi nchini!
Na ni Muislam safi mcha Mungu!
Usipomkuta yeye, basi vijana wake wapo...waulize chochote watakupa msaaada unaoutakankama ni aina gani ya vipodozi vya kuanza navyo kuvinunua kwa bisahara yako, na ni sh ngapi at least uanze nayo!
Pale Sabasaba, kuna maduka mengi sana, ila nimekuelekeza kwa huyo mdada kwakua yeye au vijana wake hawata take advantage ya ugeni wako wa biashara ili wakuuzie vipodozi ambavyo haviuziki sana au wakulalie bei ila kwa kadiri siku zinaenda utazidi kuyajua maduka mengi, na utafahamiana na watu wengi na mbinu nyingi!
Mwisho, nikutakie kila la kheri kwa biashara yako mpya unayotaka kuianza, ila kuwa mwangalifu na expire date at all time!
kudos to you, big boss.