#COVID19 Ufafanuzi: Muuguzi aliyemchoma chanjo Mhe. Rais Samia na viongozi wengine kutovaa mipira ya mikono (gloves)

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma.

#Jikinge, wakingeWengine
Chukua hatua
IMG-20210728-WA0043.jpg
Screenshot_20210728-153313_Drive.jpg


PIA SOMA:

- #COVID19 - Ikulu: Imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?
 
Exquisite....

At last people would well be informed!

#TujitokezeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#SiempreSSH
#JMTMilele
#KaziIendelee
 
Mi Tanzania huwaga sielewi wanatushauri tusikusanyike ila wao wanatukusanya 🤣🤣 mfano leo kwenye uzinduzi sikuona umuhimu wa kujaza watu kuja kushuhudia uzinduzi, ivi kulikua haiwezekani mh Raisi akapata chanjo yeye na mumewe au watu wachache mbele ya kamera the anatoa hutuba kuhamasisha watu wengine wafuatilie kupitia media
 
Ufafanuzi toka CDC!? Hongera kwa kuitambua CDC kwa sababu nyungu za mwendazake haziendani kabisa na CDC.
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma...
 
Wizara ya Afya Tanzania Askofu gwajima awajibishwe au aongee kwa hadhara kwamba ni salama amepotosha mamillioni ya watanzania watu wanaogopa chanjo sasa kuliko hata corona yenywe
Unakumbuka awamu ilopita ilisemwa nini juu ya maswala ya chanjo na matumizi ya barakoa?

Badala ya kumhusudu huyo jamaa ungeshauri hamasa na elimu itolewe zaidi wananchi wapate kuelewa na kuwatoa kwenye kule kuamini walikoaminishwa awali awamu ile na kufanya waelewe usahihi ni upi.

Yani kuna watu bado hawatilii maanani kabisa swala la kuchukua tahadhari zidi ya huo ugonjwa.

Hata wakivaa barakoa hawavai kwa usahihi, mtu anavaa barakoa lakini mdomo nje , Pia nje!
hawanawi mikono kwa usahihi , social distancing n.k
 
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma...
Hapa je
Screenshot_20210728-173039.jpg
 
Kuna contact diseases tena ikiwa mtu anatoa huduma kwa kugusa mtu zaidi ya mmoja ni hatari kwake na kwa anao wahudumia.
Examination gloves p/100 haifiki hata TZS 10000 .
Tuache kutafuta majibu ya kujiridhisha kwa mtu kuchukulia mazoea kwenye afya za watu .
@wizarayaafyatanzania
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom