Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
Wadau tafadhali pitieni ufafanuzi kutoka CCM
*Kumekuwapo malumbano kwa baadhi ya watu kuhusu Mamlaka iliyotumia Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kufanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika Majimbo ya Kinondoni na Siha pasina kupitia mchakato wa Kura wa Kura ya Maoni.
Chama kinapenda kutoa ufafanuzi mdogo, kwamba uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi Mwezi Desemba 2017, Mjini Dodoma, umefanyika kwa mujibu wa Katiba, Kanuni ya Uchaguzi na Kanuni za Uteuzi wa Wagombea wa CCM katika Vyombo vya Dola.
Kanuni Za Uteuzi Wa Wagombea Wa CCM Kuingia Katika Vyombo Vya Dola (2010), Fungu la Tatu, Ibara ya 16 (2) Kanuni inasema, "Endapo, kwa sababu maalum, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itaona kuwa hakuna haja ya kuitisha kura za maoni, hususan katika uchaguzi mdogo, itakuwa na uwezo wa kuelekeza kwamba zoezi la kura za maoni lisifanyike."
Kanuni hii haina mabadiliko na inasomeka hivyo hivyo katika Kanuni hii toleo la 2005 Fungu la Pili Ibara ya 10(2)*
Imetolewa na,
*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*