Ufafanuzi kuhusu Mshindi wa Kombe la Shirikisho la Azam na Qualification ya CAF confederation cup msimu ujao

B.4really

Senior Member
Jan 30, 2013
199
89
Wakuu salama?.
Nilikuwa nimekaa leo najiwazia ila sijapata majibu kuhusu hili swala, kama mnavyojua SIMBA SC ndio Mabingwa wa nchi msimu huu hivyo kulingana na kanuni zetu za TFF huyu tayari ndiyo mwakilishi wa Kombe la klabu bingwa Afrika msimu ujao.

Je ni vipi kama ikitokea Simba akamfunga Yanga hiyo Tar.12/07 na kutinga fainali na akabeba Kombe, Je ni nani Atakayeiwakilisha nchi kwenye kombe la shirikisho Afrika ikizingatiwa kwamba Mshindi wa Azam confederation ndio anatakiwa kuwa mwakilishi!?

Msaada wenu tafadhali wakuu.
 
Kwa kanuni za sasa, mwakilishi wa nchi kwenye mashindano ya shirikisho ya CAF atatokana na mashindano ya shirikisho yaani AZAM confederation.
Endapo itatokea mshindi wa kombe la AZAM atakua na nafasi nyingine ya kuiwakilisha nchi kwenye klabu bingwa, basi makamu wake (mshindi wa pili) kwenye kombe la Azam ndiye atakayepata nafasi hiyo ya kushiriki shirikisho.

Kwa sasa, hakuna namna yoyote ile mshiriki wa CAF confederation akatokana na ligi kuu labda pale tu ambapo nchi itatakiwa kuwakilishwa na timu mbili huko kwenye shirikisho (KMC walinufaika na huu utaratibu mwaka jana).
 
Kombe La Shirikisho Atawakilisha Makamu Bingwa Wa Kombe La Tff, Hivyo Kwa Hali Ilivyo Namungo Ataiwakilisha Nchi Kwani Yeye Ndo Ataingia Fainali Na Mnyama Simba, Wekundu Wa Msimbaz, Taifa Kubwa, Wanalunyas Wazee Wa Kidedea Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa Wazee Wa Vuvuzela, Timu Inayocheza Mpira Wa Kiwango Kilichothibitishwa Na Shirikisho La Mpira Wa Miguu Afrika Caf,
 
Wakuu salama?.
Nilikuwa nimekaa leo najiwazia ila sijapata majibu kuhusu hili swala, kama mnavyojua SIMBA SC ndio Mabingwa wa nchi msimu huu hivyo kulingana na kanuni zetu za Tff huyu tayari ndiyo mwakilishi wa Kombe la klab bingwa Africa msimu ujao.
Je ni vipi kama ikitokea Simba akamfunga Yanga hiyo Tar.12/07 na kutinga fainali na Akabeba Kombe,Je ni nani Atakayeiwakilishi nchi kwenye kombe la Shirikisho Africa ikizingatiwa kwamba Mshindi wa Azam confederation ndio anatakiwa kuwa mwakilishi!?
Msaada wenu tafadhali wakuu.

Anaenda Mshindi wa Pili kwenye Kombe la Shirikisho ( Mashindano husika)
 
Mwaka jana, alidhurumiwa LIPULI, na kupelekwa KMC. Mwaka huu, wataangalia tena namna ya kumchomeka Yanga!

Lipuli hakudhulumiwa, Kombe la AZAM confederation linatoa timu moja tu kwenda mashindano ya shirikisho barani Afrika, na mwaka jana alikwenda Azam Fc.
ikitokea kuna nafasi zaidi ya moja ya kupeleka timu kombe la shirikisho na klabu bingwa, basi wawakilishi wengine wote watatokana na ligi kuu.

Pamoja na mambo mengine, lengo la kanuni hii ni kulinda hadhi na ukuu (supremacy) ya ligi kuu.
 
Kwa kanuni za sasa, mwakilishi wa nchi kwenye mashindano ya shirikisho ya CAF atatokana na mashindano ya shirikisho yaani AZAM confederation.
Endapo itatokea mshindi wa kombe la AZAM atakua na nafasi nyingine ya kuiwakilisha nchi kwenye klabu bingwa, basi makamu wake (mshindi wa pili) kwenye kombe la Azam ndiye atakayepata nafasi hiyo ya kushiriki shirikisho.

Kwa sasa, hakuna namna yoyote ile mshiriki wa CAF confederation akatokana na ligi kuu kwa labda pale tu ambapo nchi itatakiwa kuwakilishwa na timu mbili huko kwenye shirikisho (KMC walinufaika na huu utaratibu mwaka jana).
Kwani ikitokea simba akajisemea mimi nataka kucheza kombe la shirikisho sitaki klabu bingwa atalazimishwa itakuwaje japo ni ngumu kuacha kushiki kombe la mabingwa ukacheza shirikisho??

Pia msiwe na wasi wasi mshindi wa FA ya bongo ni Yanga hata msiumize bichwa
 
Acha kuchanganya mambo wewe
Sidhani kama nachanganya. Mwaka jana, tulipata fursa ya kuwakirishwa na timu mbili mbili kwenye hayo mashindano. Ilikuwa ni bahati tu, baada ya Simba kufanya vizuri, msimu uliopita.
Simba, na Yanga, walituwakirisha Klabu bingwa, ikiwa ni mshindi wa kwanza na wa pili, wa VPL. Huko Azam, mshindi alikuwa Azam, mshindi wa pili alikuwa LIPULI. Hivi, hilo kombe la Azam, angelichukua Lipuli, na mshindi wa pili angekuwa ni AZAM, au YANGA, au SIMBA na wakati huo huo timu hizo huko VPL zipo nafasi ya 3- ,zingeikosa hiyo nafasi ya kutuwakirisha kwa tafsiri ya ushindi wa pili kombe la Azam?
 
Kwa muujibu wa sheria hawawezi kuwakilisha
 
Basi hujui kanuni na sheria za kupata mwakilishi
 
Mwaka jana, alidhurumiwa LIPULI, na kupelekwa KMC. Mwaka huu, wataangalia tena namna ya kumchomeka Yanga!
Yanga asipomfunga Simba hiyo tarehe 12 ajue hakuna muujiza unaoweza kufanyika kumbeba. Yanga ijibebe yenyewe isisubiri mbeleko.
 
Kwani ikitokea simba akajisemea mimi nataka kucheza kombe la shirikisho sitaki klabu bingwa atalazimishwa itakuwaje japo ni ngumu kuacha kushiki kombe la mabingwa ukacheza shirikisho??

Pia msiwe na wasi wasi mshindi wa FA ya bongo ni Yanga hata msiumize bichwa

Mkuu kinachofuatwa ni kanuni na sio ''fulani amependezewa na nini''.

Kila la heri kwa Yanga katika kuupata ubingwa wa FA (AZAM confederation cup)
 
naona mnaangaika tu na mihogo yenu sijui simba yanga namungo ila kiukweli atakae pangiwa na sahare aandike kaumia hilo kombe lazima liende Tanga tu nasahare ndio mabingwa
 
Back
Top Bottom