Ufafanuzi kuhusu mafao ya kujitoa katika marekebisho ya sheria za mifuko; tumekwisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi kuhusu mafao ya kujitoa katika marekebisho ya sheria za mifuko; tumekwisha

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by rugumye, Aug 1, 2012.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  UFAFANUZI KUHUSU MAFAO YA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO.

  Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu mafao ya kujitoa:
   Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imesha sainiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.
   Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza kama si kuondoa kabisa kinga hii ya mfanyakazi anapofika uzeeni.
   Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kinyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.
   Pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini na zinginezo yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu
   Kwa mujibu wa marekebisho hayo mafao ya kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60).
   Tunawaomba Waajiri wa waelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameshastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nayo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika
   Tayari kumekuwa na hofu kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

  [FONT=&quot]
  [/FONT]

   Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini, ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote na kuelimisha Umma kwa ujumla.
   
 2. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu, umerudi lini Tanzania?
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  ****** yao, wakawapatie mafao bibi zao na babu zao kwa miaka hiyo 55, sie tunachotaka ni kumaliza kazi na kupewa chetu hizo habari za 55 sijui 60 wanazijua wao ambao wanakopeshana hela zetu.Ni mtanzania gani ana uhakika wa 55 na afterall wakikupa ukiwa 55 utazifanyia nini.

  Inatakiwa upewe chako ukiwa na nguvu za kutosha ili uweze kujiendeleza hata kwa kufungua biashara ya kukuwezesha kumudu maisha.Sasa ukiwa 55 hata huna akili za kufikiria tena.Mimi nasema serikali ishafanya mengi sana ya kuvumiika lakini kwa hili la mafao niko tayari kuandamana mpaka Msonga - Bagamoyo hata kama mkuu atakuwa huko kwa mapumziko
   
 4. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tumeshaliwa mkuu hao SSRA wanasema hatuna chetu.
   
 5. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hili ni popobawa ndugu, sijui kama tutatoka bila kuamka. amkeni kutoka usingizini. mchwa umemaliza kibubu penye kula kwa raha mstarehe ni kwenye mifuko ya jamii kwaani haina watetezi.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Msamehe bure tu
   
 7. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2016
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  kuna wale ambao ajira zao ni za mikataba eg 3 years then mkataba wake haukuwa renewed au kampuni imemaliza kazi eg ya ujenzi au kampuni imefunga shughuli zake nchini. Katika mazingira haya, muajiriwa anajikuta ajira imekoma na hana uhakika wa kupata ajira nyingine ambayo ataendeleza kuwekewa akiba. Kuna jamaa yangu, alikuwa shirika la umma na alikuwa mawanachama wa NSSF kwa miaka 12 lakini kapata kazi ya kudumu WHO na station yake ni Zambia and she is only 39 years old, anataka kuchukua akiba yake NSSF, je hatapata hadi atimize miaka 55 (16 years to come)?. Na huyu muajiriwa let's say ni only 45 years old. Je, asubiri kwa miaka 10 ndio alipwe chake? Nafikiri, labda wasilipwe wale wanaojitoa kwa hiari
   
 8. C

  Crazy genius Member

  #8
  Jun 7, 2016
  Joined: Apr 26, 2016
  Messages: 44
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 25
  Serikali ya mwendo kasi
   
Loading...