Ufafanuzi kuhusu kero kubwa Soko la Mabibo (Mahakama ya Ndizi)

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
349
500
Boniface Jacob

Mstahiki Meya Ubungo

Nawasalimu wote katika Jina la Bwana! pamoja na Salaam ningependa leo 14 April 2020 nitolee Ufafanuzi juu ya kero Kubwa Iliyopo katika Soko la Mabibo.

Kwa Vipindi tofauti nimekuwa nikitafutwa na vyombo vya habari kuhusu malalamiko ya watumiaji wa soko, wafanyabiashara na Kero zilizopo katika soko la Mabibo. Malalamiko, kero Sugu na kubwa katika Soko letu la Mabibo zimekuwa.

1. Matope na Kufurika Maji wakati wa Mvua (hasa wakati huu wa Masika)
2. Kukosekana kwa miundombinu mizuri ya soko kama mabanda ya kisasa, barabara za kuingia na kutoka, sakafu sehemu za kutandikia mazao na huduma nyinginezo.
3. Uchafu Uliokithiri katika soko hilo.

Ikumbukwe Soko la mahakama ya ndizi, Mabibo lilihamia pale kutokea Buguruni Mwaka 2002 November

Viongozi wa Serikali wakati huo walitoa Amri na Maelekezo ya Soko la ndizi kuhamia pale lilipo leo.

Kwa kipindi chote hicho cha Miaka 18, Mapato ya Soko yamekuwa yakigawanywa kwa wadau wa Soko KIWANDA na MANISPAA (Kinondoni wakati huo)

Lakini Kwa Bahati Mbaya Taarifa za Mapato hayo zilikuwa zinaonyesha soko linaingiza kiasi cha Millioni 17 tu kwa Mwezi na 184 kwa Mwaka.

Wakati huohuo Manispaa zilikuwa zinapokea Millioni 4 tu baada ya kuambiwa kuwa pesa zingine zinaenda kwenye uendeshaji wa soko na kinachobakia kinaenda KIWANDANI.

Baada ya kuanzishwa kwa Manispaa ya Ubungo Mwaka 2016 November. Soko la Mabibo lilichukuliwa kama moja ya Chanzo kikubwa cha Mapato na Manispaa ya Ubungo iliyopelekea kubadili Mfumo wa ukusanyaji Pesa katika soko la Mabibo.

Ambapo Kwa Mafanikio Makubwa Miezi hiyo Manispaa ilifanikiwa Kukusanya kiasi cha Tsh Millioni 100 kwa Mwezi na Makisio ya Billioni 1.2 kwa Mwaka na hata wakati Mavuno si Mazuri soko limekuwa linaingiza si Chini ya Millioni 65 kwa Mwezi.

katika Kufaidika na Mapato hayo Manispaa iliandaa Mkataba wa kugawana faida Baada ya Uendeshaji (MOU) ambapo kiwanda lilikuwa kinapata zaidi ya Millioni 20 kwa Mwezi kutoka ile waliokuwa Wanasema wanapokea ya Millioni 4 kwa Mwezi.

Pamoja na Mafanikio Makubwa hayo yaliyojitokeza,bado KIWANDA CHA URAFIKI kama wamiliki wa Eneo walianzisha Madai Mapya ya kutaka Eneo lao na Kwamba hawataki SOKO eneo hilo na Kugomea kusaini Ule Mkataba wa Kugawana Mapato kati yao na Manispaa ya Ubungo.

Kiwanda cha Urafiki kikafufua Madai yao Mahakamani ya tangu Miaka ya 2000 huko nyuma na kupata Dalali wa Mahakama YONO AUCTIONEERS Waje kuwaondoa Wafanyabiashara wote katika Eneo lao la Sokoni hapo Mabibo.

Kwa Masikitiko Baada ya Kutokea Hali hiyo Viongozi wote wa Serikali kuanzia WILAYA Mpaka MKOANI hawakuwa Upande wa Manispaa kuwa Soko la Mabibo liendelee kubakia pale, Bali Viongozi wa serikali waliungana na Kiwanda kutaka Wafanya Biashara wote wa sokoni watoke waende pasipo Julikana.

( Katika Ufafanuzi huu Nimeambatanisha Video ya tarehe 10 January 2018 Mkuu wa Mkoa na wilaya wakiwa Sokoni kutoa Miezi Miwili Wafanya Biashara wawe wameondoka Katika Soko la Mabibo) na Video hii ndiyo inaonyesha Msimamo wa Serikali wa kutokulitambua Soko la Mabibo.(Chanzo cha Tatizo)

Kwa Mujibu wa Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Serikali Ulikuwa Soko la Mabibo liwe limefungwa Kufikia Mwezi April 2018.

Mimi kama Mstahiki Meya na Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa tulianzisha Harakati za Kuhakikisha Soko linabakia palepale Mabibo na Wafanya Biashara zaidi ya 2000 Wanaendelea kufanya Biashara zao tuliyapinga Maelekezo ya Viongozi hao walioyatoa kwa Muda wa Miezi Miwili Soko liwe limefungwa.

Tulimtafuta Waziri wa TAMISEMI na Baadae Rais Magufuli ambao Wote Baada ya Kuwapa hoja kuwa wasiangalie tuh kuwa Ubungo ni Manispaa ya Wapinzani Bali.

1. Ajira za watu wanaenda Kupoteza sokoni pale,
2. Juu ya Kiwanda Kukodisha Ofisi za Mabasi ya Mkoani katika Maeneo ya Kiwanda cha Urafiki na Ufisadi Mkubwa wa Mikataba yao ya upangishaji,
3. Uwepo wa Kituo cha Mafuta Lake Oil lakini watu hapohapo hawataki pawe na Soko lenye Manufaa Makubwa kwa Wananchi kuliko
4. Kwamba Kiwanda Cha Urafiki ni Kiwanda Cha Ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Uchina, kwa Maana hiyo hata eneo la Soko ni la Serikali pia.

Pamoja na Msaada Kutoka Juu wa Waziri wa TAMISEMI kuagizwa aje Kusitisha Operesheni ya kuwaondoa wafanya Biashara wa Soko la Mabibo.

Bado Manispaa ya Ubungo haijapata Ruhusa Rasmi ta kuendelea Kutumia eneo hilo kama Soko halali la Manispaa ya Ubungo, ili kuruhusu Uwekezaji Mkubwa na Ukarabati wa soko la Mabibo ambapo Manispaa ya Ubungo kwa muda wa miaka 3 mfululizo imekuwa ikitenga zaidi ya Billioni 1 katika kukarabati na kutengeneza masoko yake.

Lakini kwasababu ya kukosekana kwa mkataba baina ya Manispaa na kiwanda, sheria inakataza kutumia kiasi kikubwa cha fedha kabla ya hati ya kukabidhiwa eneo la Soko la Mabibo au Kuwepo kwa Mkataba na Manispaa ya Ubungona Kiwanda cha Urafiki.

Kinyume chake,kuwekeza Pesa kubwa sehemu ambayo bado hatuna hati ya kukabidhiwa na Mkataba na wanaodai kumiliki eneo hilo,inaweza kugeuka kuwa haraka kubwa Kwa Manispaa na hata sheria inatukaza.

Kwa sasa kitu pekee ambacho Manispaa tunachoweza kufanya ni marekebisho madogo madogo tuh ya Miundombinu na Ujenzi wa Choo kwa Sababu ya Kukosekana Hatima ya nani amiliki wa eneo la soko la Mabibo Ndizi

MWISHO
Mimi na viongozi Wenzangu wa kamati ya fedha tunaitaka Serikali kuu (TAMISEMI) kuharakisha utatuzi wa sintofahamu ya Umiliki na Uwepo wa Soko la Ndizi Mabibo ili kuruhusu Manispaa kutoa huduma za Kisasa na Kuwekeza Pesa Nyingi ili kukomesha Matatizo yanayojitokeza mara kwa mara na Kuwasababishia Wananchi Usumbufu Usio na lazima,Kwa Sababu Soko la Mabibo ni la Pili kwa ukubwa hapa Dar es Salaam.

CORONA IPO CORONA INAUA, JIKINGE NA CORONA


IMG-20200414-WA0070.jpg
IMG-20200414-WA0068.jpg
IMG-20200414-WA0069.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom