Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,298
- 45,586
1. Nchi kuwa na ufalme haimaanishi kutokuwa na demokrasia.
Kuna kitu kinaitwa constitutional monarchy/ufalme wa katiba ambao unadhibitiwa na katiba huu unaweza kuwa utawala wa kidemokrasia kabisa kama U.K, Denmark na Sweden. Kuna absolute monarchy/ ufalme mtimilifu, huu ni ufalme ambao haudhibitiwi na katiba na mfalme anaweza kuamua jambo lolote bila kufungwa na katiba hizi ni falme za Saudi Arabia, Oman, Swaziland, Abu dhabi.
Jamii zote duniani kwa wakati fulani zilikuwa chini ya wafalme, emperors, machifu, watemi au mabwana wa kivita. Autocracy/uimla ni mfumo default wa binadamu wote na kuna wakati ulizifaa jamii na kuzifanya kuu sana hivyo hata wakati ulipoindolewa kuna baadhi ya jamii waliona ni vyema kuendelea kuzihifadhi historia zake na wengine kama Ufaransa waliamua kuondoa na historia yake kabisa.
2. Ukomo wa vipindi vya uongozi sio kigezo muhimu cha demokrasia. Kuwepo kwa ukomo wa vipindi vya urais, uwaziri mkuu, ubunge n.k wa miaka 4, 5, n.k haimaanishi ndio kuwepo kwa demokrasia. Ujerumani haina ukomo wa Kansela wake ila ni demokrasia imara sana. Kitu kinacholeta shida hasa kwa nchi za Africa ni watawala waliopo madarakani kutaka kuondosha ukomo wa vipindi vya utawala kwa manufaa yao binafsi (kucheza na katiba).
3. Kuwepo na vyama vingi au vyama tofauti kubadilishana madaraka sio kiashiria muhimu cha demokrasia iliyokomaa. Jambo muhimu ni mchakato, taasisi imara na uhuru wa watu katika kufanya maamuzi ya chama gani kiwepo madarakani. Botswana ni mojawapo ya demokrasia iliyopiga hatua nzuri chini ya chama kimoja tangu uhuru. Chaguzi zinafanyika kwa haki na uhuru tangu nchi hiyo ipate uhuru, BDP imekuwa ikishinda bila hila nyingi na viongozi wanawajibika sana kwa raia wake.
4. Ni kweli nchi za kidemokrasia haziwezi kufanana kwa asilimia hata tisini ila demokrasia ina misingi yake ambayo ni ya duniani kote /"Universal". Baadhi ya hiyo misingi ni utawala wa sheria, uhuru wa mihimili, uhuru wa vyombo vya habari, uchaguzi huru na wa haki, kuheshimu haki za binadamu n.k.
5. Demokrasia sio kamilifu/perfect kwa 100% ila ndio mfumo bora zaidi kwa binadamu waliostaarabika.Demokrasia ni kazi inayoendelea kuboreshwa kila siku/"work in progress".