Ufafanuzi kuhusu demokrasia: Dhana (myths), upotoshaji na uhalisia wake

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
36,570
44,227
1. Nchi kuwa na ufalme haimaanishi kutokuwa na demokrasia.

Kuna kitu kinaitwa constitutional monarchy/ufalme wa katiba ambao unadhibitiwa na katiba huu unaweza kuwa utawala wa kidemokrasia kabisa kama U.K, Denmark na Sweden. Kuna absolute monarchy/ ufalme mtimilifu, huu ni ufalme ambao haudhibitiwi na katiba na mfalme anaweza kuamua jambo lolote bila kufungwa na katiba hizi ni falme za Saudi Arabia, Oman, Swaziland, Abu dhabi.

Jamii zote duniani kwa wakati fulani zilikuwa chini ya wafalme, emperors, machifu, watemi au mabwana wa kivita. Autocracy/uimla ni mfumo default wa binadamu wote na kuna wakati ulizifaa jamii na kuzifanya kuu sana hivyo hata wakati ulipoindolewa kuna baadhi ya jamii waliona ni vyema kuendelea kuzihifadhi historia zake na wengine kama Ufaransa waliamua kuondoa na historia yake kabisa.

2. Ukomo wa vipindi vya uongozi sio kigezo muhimu cha demokrasia. Kuwepo kwa ukomo wa vipindi vya urais, uwaziri mkuu, ubunge n.k wa miaka 4, 5, n.k haimaanishi ndio kuwepo kwa demokrasia. Ujerumani haina ukomo wa Kansela wake ila ni demokrasia imara sana. Kitu kinacholeta shida hasa kwa nchi za Africa ni watawala waliopo madarakani kutaka kuondosha ukomo wa vipindi vya utawala kwa manufaa yao binafsi (kucheza na katiba).

3. Kuwepo na vyama vingi au vyama tofauti kubadilishana madaraka sio kiashiria muhimu cha demokrasia iliyokomaa. Jambo muhimu ni mchakato, taasisi imara na uhuru wa watu katika kufanya maamuzi ya chama gani kiwepo madarakani. Botswana ni mojawapo ya demokrasia iliyopiga hatua nzuri chini ya chama kimoja tangu uhuru. Chaguzi zinafanyika kwa haki na uhuru tangu nchi hiyo ipate uhuru, BDP imekuwa ikishinda bila hila nyingi na viongozi wanawajibika sana kwa raia wake.

4. Ni kweli nchi za kidemokrasia haziwezi kufanana kwa asilimia hata tisini ila demokrasia ina misingi yake ambayo ni ya duniani kote /"Universal". Baadhi ya hiyo misingi ni utawala wa sheria, uhuru wa mihimili, uhuru wa vyombo vya habari, uchaguzi huru na wa haki, kuheshimu haki za binadamu n.k.

5. Demokrasia sio kamilifu/perfect kwa 100% ila ndio mfumo bora zaidi kwa binadamu waliostaarabika.Demokrasia ni kazi inayoendelea kuboreshwa kila siku/"work in progress".
 
Ukitazama kwa makini utagundua hakuna ubaya kwa nchi kuongozwa kifalme, kwasababu ukiachia mbali uwepo wa malkia anayekuwepo bila kupigiwa kura na kupewa mahitaji yote toka kwa kodi za wananchi.

Ni bora hilo kuliko huku kwetu ambapo viongozi wanaopatikana kwa wizi wa kura, wanapewa mahitaji yote toka kwa kodi za wananchi ambao hawakuwachagua, viongozi walioshindwa kukuza uchumi mpk tunaenda kuomba kwa malkia.

sisi ndio tuna matatizo zaidi ya wale wanaotawaliwa kifalme, kwao wanaishi wakijua malkia ni fulani full stop.
 
Kaja kutafuta aibu hapa jukwaani
Huyu jamaa mimi ana nishangaza sana linapo fika swala la demokrasia huwa ana wasema sana viongozi wa upande wa mashariki kuwa sio waumini wa demokrasia ila wa upande wa magharibi ni waumini wa demokrasia kaja kuwa tetea hapa tawala za kifalme za kiuaji za magharibi na kuzivika joho la demokrasia Ila falme za uarabuni kazi kataa . Nataka aniambe ni wananchi wangapi waliwapigia kura familia ya kina Elizabeth kuwa hiyo familia ndio inapaswa kuitawala Uingereza na familia nyingine hapaswi kufanya hivyo ?
 
Badala ya kufura na kupayuka tu ungejibu kwa hoja ewe mkomununisti uchwara wa bongo .
Endelea kutetea matawala mauaji ya kidikteta ya magharibi huku ukiya vika majoho ya tawala za kidemokrasia hizo ndizo kazi za vibaraka hata wakati wa ukoloni.
 
Raia wa U.K wanaweza kumkosoa au hata kumtakana malkia au mfalme wa Uingereza bila kuguswa hata na kidole. Raia wa Saudi Arabia kama Jamal Khashoggi hata wakiwa nje ya nchi wakijaribu kufanya hivyo hawewezi kuendelea "kusavaivu".
Tumia kichwa kufikiri kwa upana, sio kufugia nywele tu.
Huyu jamaa mimi ana nishangaza sana linapo fika swala la demokrasia huwa ana wasema sana viongozi wa upande wa mashariki kuwa sio waumini wa demokrasia ila wa upande wa magharibi ni waumini wa demokrasia kaja kuwa tetea hapa tawala za kifalme za kiuaji za magharibi na kuzivika joho la demokrasia Ila falme za uarabuni kazi kataa . Nataka aniambe ni wananchi wangapi waliwapigia kura familia ya kina Elizabeth kuwa hiyo familia ndio inapaswa kuitawala Uingereza na familia nyingine hapaswi kufanya hivyo ?
 
Wewe mkomunisti acha kutukana marehemu na jikite kujadili mada.
Ukomunisti wangu haunizui mimi kutoa mchango tofauti na kile alicho andika mtoa mada anaye jifanya kuibadilisha nyeupe kuwa nyeusi . Kwa kujifanya kuupaka rangi utawala wa kiuaji wa kidikteta kuwa utawala wa nuru wa kidemokrasia kisa tu ni upande wa magharibi.
 
Raia wa U.K wanaweza kumkosoa au hata kumtakana malkia au mfalme wa Uingereza bila kuguswa hata na kidole. Raia wa Saudi Arabia kama Jamal Khashoggi hata wakiwa nje ya nchi wakijaribu kufanya hivyo hawewezi kuendelea "kusavaivu".
Tumia kichwa kufikiri kwa upana, sio kufugia nywele tu.
Jibu swali : Wananchi wangapi waliipigia kura familia ya kidikteta ya kina Elizabeth wa pili kuwa hiyo familia pekee ndio Ina mamlaka pekee ya kutawala UK ? nasubiri jibu
 
Kama unataka tawala za kidemokrasia kutoka Asia hiz hapa.
Taiwan, Japan, Korea Kusini, India, Singapore na Philippines.
Ukomunisti wangu haunizui mimi kutoa mchango tofauti na kile alicho andika mtoa mada anaye jifanya kuibadilisha nyeupe kuwa nyeusi . Kwa kujifanya kuupaka rangi utawala wa kiuaji wa kidikteta kuwa utawala wa nuru wa kidemokrasia kisa tu ni upande wa magharibi.
 
Poor angry little man.
Jibu swali : Wananchi wangapi waliipigia kura familia ya kidikteta ya kina Elizabeth wa pili kuwa hiyo familia pekee ndio Ina mamlaka pekee ya kutawala UK ? nasubiri jibu
 
Raia wa U.K wanaweza kumkosoa au hata kumtakana malkia au mfalme wa Uingereza bila kuguswa hata na kidole. Raia wa Saudi Arabia kama Jamal Khashoggi hata wakiwa nje ya nchi wakijaribu kufanya hivyo hawewezi kuendelea "kusavaivu".
Tumia kichwa kufikiri kwa upana, sio kufugia nywele tu.
Usisahau pia hao madikteta wapumbavu waliua Babu na Bibi zako Tanganyika, Zimbabwe, SA , Kenya na nchi lukuki endelea kulamba makalio yao na kuwa tetea maana hio ndio kazi ya vibaraka na chawa hata wakati wa ukoloni walikuwa Wana fanya hivyo .
 
WANA CCM NA UTAWALA WAO WA URAIS WA KIFALME / DIKTEKTA

Mwalimu Nyerere muasisi wa CCM ananukuliws kusema rais wa Tanzania ana madaraka ya kifalme na anaweza kugeuka dictator wakati wowote maana katiba imempa uwezo huo akikusudia

Sasa Tuiangazie taifa lenye historia ndefu ya misuguano baina ya mfalme na bunge pia baina ya raia na mfalme kuhusu masuala mbalimbali kama tozo (hii hubuniwa na mfalme), kodi hizi hupitishwa kwa mswada wa mfalme kuuleta bungeni ujadiliwe, kutangaza vita ya kijeshi, masuala ya mfalme kuwa juu ya sheria kwa vile anaamini ni mteuliwa wa Mungu n.k

Siku za karibu viongozi wa CCM na wale wa serikali wote wamekuwa wakithibitisha kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa rais wa tanzania ana mamlaka makubwa mithili ya mfalme. Tunasikia rais amefanya hili, ameelekeza likafanyiwe kazi, ametoa hela ya mbolea, amejenga vituo vya afya, amekataza shughulu za kisiasa baada ya uchaguzi ilihali katiba inaruhusu mikusanyiko ya kisiasa kwa kweli kivuli cha rais ni kirefu kinachofunika kila kitu nchini Tanzania.



Charles I begins his 11 years of personal rule​

10th March 2019
It was today in 1629 that Charles I dissolved his third parliament and began his eleven years of Personal Rule – when he governed alone and refused to call a parliament. He had been king for almost four years, and had clashed with his parliament from the very beginning of his rule.

In the medieval period it was usual that the king ruled his kingdom personally, with assistance from a council which likely included representatives of the most powerful families, senior members of the church, and civil servants. Edward I was the first king to call a parliament as he wanted to ensure that the changes he wished to make to laws and taxation were acceptable to the people of England. It was costly and time consuming to call a parliament, so they were summoned sparingly and dissolved by the king once the specific task had been completed and the king would continue governing the country himself. From the fourteenth to the sixteenth centuries, the power of parliament grew and it became accepted that only a parliament could impose new or greater taxes.

Charles’s father James I believed in the divine right of kings – that as monarch, the only authority above him was God and therefore he should be able to govern without answering to a parliament. However, James was often very short of money and so was forced to summon parliaments frequently in order to raise funds through taxes. When parliament was sitting, they often insisted that the king agree to various laws and policies before they would agree to support the increased taxation.

With this history and his own strong belief that the king’s powers could not be challenged, when parliament began to criticise Charles I more harshly, he decided to rule without them. This was feasible, but only if he made peace with France and Spain, as without parliament he could never raise enough funds to continue waging war.

As the years passed, and with Charles unable to raise taxes the traditional way through parliament, the king and his advisors were forced to utilise increasingly complex ways to raise enough money to successfully run the country. One of the most unpopular of these was a ship money levy. Usually only applied to coastal counties during wartime, Charles extended it inland, claiming it fell under his royal prerogative. It raised him significant amounts of extra money.

It was when Charles tried to bring the Church of Scotland more in line with the Church of England that his Personal Rule came to an end. The Scots resented Charles’s interference and opposed the changes – this eventually escalated into the Bishop’s War, when Scotland invaded England in 1639. Charles needed money to pay troops to fight the Scots and finally had to call a parliament. This parliament lasted less than a month before Charles dissolved it, but by now he was out of options and out of money.

Forced to recall parliament a few months later, they demanded enormous concessions from the king – in particular, passing an Act that meant parliament could not be dissolved without the consent of its members. They did not want to risk another eleven years of Charles governing alone.

Unsurprisingly, Charles was unhappy with the demands. The breakdown between the king and parliament eventually led to the First English Civil War in 1642, with Charles leaving London to raise his army and regain by force the authority he believed to be his God given right.

6ae7810cef1654a0a4305e75f52626c9.png


Image: Charles I (1600-1649) with M. de St Antoine, by Anthony van Dyck, 1633. RCIN 405322. Royal Collection Trust / © Her Majesty Queen Elizabeth II 2019

Source : Charles I begins his 11 years of personal rule - News


The Trial of Charles I (1649)​




Source : Historia Civilis

In January 1649, after years of civil war, King Charles I stood trial in a specially convened English court on charges of treason, murder, and other high crimes against his people. Not only did the revolutionary tribunal find him guilty and order his death, but its masters then abolished monarchy itself and embarked on a bold (though short-lived) republican experiment. The event was a landmark in legal history. The trial and execution of King Charles marked a watershed in English politics and political theory and thus also affected subsequent developments in those parts of the world colonized by the British.
 
Kama unataka tawala za kidemokrasia kutoka Asia hiz hapa.
Taiwan, Japan, Korea Kusini, India, Singapore na Philippines.
Singapore si hao wapumbavu wenzako U.S.A waliipachika jina la tawala ya dikteta chini ya Lee Kuan Yew na CIA kutaka kuipindua 1965 , hao Taiwan unajua Kuomitang walicho wafanya huko kisiwan, Ufilipino wazalisha madikteta yaliyo kope kwa U.S.A, Korea Kusini unajua Park Chung Hee alipachikwa jina gani na magharibi, Kashmir wanaujua udikteta wa India vizuri, hao Japan wauondoe utawala kwanza wa kidikteta wa kifalme ndio uje uwaweke kwenye hilo kundi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom