ufafanuzi juu ya kusomea sheria

Bengazuu

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
1,029
1,235
wakuu nilikua naomba ufafanuzi juu ya swala hili 'mimi nataka nije kusomea sheria lakini kuna mtu kaniambia kama ukisomea sheria kazi lazima ujitafutie na sio kuajiliwa na serikali' je' kuna ukweli wowote kuhusu hili nisaidieni wakuu maana naipenda sana sheria.
 
kwanza nikupongeza kwa kutamani kusoma,sheria.cha kwanza ujiulize unataka kusoma sheria kwa ajili ya nini,kama lengo lako ni kusoma ili kuajiriwa,kuna hatari ya wewe kukata tamaa ya maisha baadaye,hasa kama ukisoma halafu usipate ajira. Lakini kama unasoma kwa ajili ya kuongeza ufahamu na namna ya kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha,yaan uwe na elimu ya sheria kama hazina yako ya maisha,hii itakusaidaia sana kwan, wakati mwingine watu wanasoma sheria na hawafanyikazi ya kisheria kama huamini uliza utambiwa wengi wanafundisha,ni wafanyabiashara na pamoja na degree yao ya sheria.
la mhimu hapa nikuangalia unataka sheria ikusaidia nini.
ajira zipo serikalini na sekta binafsi lakini za moja kwa moja kama unavyodhani. Hata kaada nyingine wamesoma na hawajapata kazi lakini huwezi kusema kwakuwa umesoma sheria utapata ajira mara moja,kuwa hakimu au jaji utajifunza hukohuko wakati wa masomo yako ya sheria,yaani sifa zipi zinamfaa mtu kuwa hakimu au jaji,chamsingi ni nia na usikate tamaa,wengi wanasema sheria ni ngumu,ukweli nikwamba hakuna kitu rahis duniani kama huna nia.
 
wakuu nilikua naomba ufafanuzi juu ya swala hili 'mimi nataka nije kusomea sheria lakini kuna mtu kaniambia kama ukisomea sheria kazi lazima ujitafutie na sio kuajiliwa na serikali' je' kuna ukweli wowote kuhusu hili nisaidieni wakuu maana naipenda sana sheria.
My dear, unataka nini katika maisha yako? Ndoto zako na malengo yako ni yapi? Unadhani ndani ya moyo wako unafurahia kusomea sheria? Unataka kusomea sheria ili iweje?
Hayo ni maswali unayopaswa kujijibu ndani ya moyo wako, ni vizuri kupata ushauri mbalimbali kutoka kwa watu lakini its you heart that will make decision.
Ukifikiria swala la kupata kazi kila course utaikosoa, sheria ni nzuri endapo moyo wako utakuruhusu.
 
Back
Top Bottom