Ufafanuzi; Huduma za mabenki bongo nyingi zina mpango wa dhuluma kwa wateja wake; Wizara ya fedha wapo kimya kulisemea!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Nitaeleza kwa kifupi;

Ukizunguka benki zote, utaratibu wa kufungua akaunti unafanana,
  1. Wanahitaji jina kwa maana ya kitambulisho chako
  2. picha yako
  3. finger print basi
  4. wakijitahidi sana, wanaomba barua toka serikali ya mtaa!
Baada ya hapo Mteja huwa anapewa CARD/Check ikiwa na maana unaruhusiwa kuweka pesa ukiamini iko mikono salama!

Swali; Kwanini benki nyingi hawatoi mikataba kwa wateja wao? nini lengo lao kama siyo dhuluma?

Umewahi kujiuliza maswali haya!
  1. Pesa zako zikidukuliwa zikapotea ki-elektroniki nani atakulipa?
  2. Ukifika ndani ya jengo la benki ikatokea Ambushi majambazi yakapola benki na pesa zako huja- deposits utamdai nani?
  3. Benki yako ikifilisiwa pesa zako utalipwaje kwa utaratibu gani? n.k
Rejea matukio kadhaa ya wateja walio lizwa kwa scenario kama hizi; Usiombe yakukute;

Nanukuu

Mteja 1.
"Nilikuwa na pesa zangu 38 mil kwenye akaunti, bank imefilisiwa, Nimeambiwa nitalipwa 150,000/={laki na nusu) kila mwezi hadi deni liishe

Mteja 2; " Nimefuatilia pesa zangu benki ya ****** naambiwa benki imefilisiwa, wakaniambia niende B.O.T , nimefika huko wanasema watatoa laki na nusu, akaunti ilikuwa ina million 280, Nina watoto wanne nataka nikawalipie Ada! naambiwa benki imefilisiwa!

Mambo kama hayo yalipaswa kuwekwa kwenye mkataba punde tu anapofungua akaunti; kuwepo mkataba tena kwa lugha ya kiswahili ili Mteja abaki na nakala;

Na sheria za fedha B.O.T ziwekwe wazi, wanapoifilisi benki X walipe pesa za wateja immediately!

(kufilisika kwa benki siyo kufilisika kwa Mteja, Wizara ya fedha/B.O.T wekeni wazi utaratibu wa kulipwa pesa kwa matukio kama hayo, utaratibu wa sasa kwakweli umejaa dhuluma)
 
Nondo kama hizi zilizotushawishi kuja JF zimeadimika sanaaa humu.
Mkuu wewe ni true Great Thinker
 
BOT wanachangia hii dhulma, kwa nini hawaweki bayana sheria kuhusu mambo kama haya...

Wao wanaifilisi Bank, halafu ukienda kwao wanakupa laki na nusu tu.

TATIZO NI BOT
 
Mm niliuelewa sana ule mjadala wa kwa nn bank ukimaliza kulipa PERSONAL LOAN hawakurudishii LOAN INSURANCE?
 
Nitaeleza kwa kifupi;

Ukizunguka benki zote, utaratibu wa kufungua akaunti unafanana,
  1. Wanahitaji jina kwa maana ya kitambulisho chako
  2. picha yako
  3. finger print basi
  4. wakijitahidi sana, wanaomba barua toka serikali ya mtaa!
Baada ya hapo Mteja huwa anapewa CARD/Check ikiwa na maana unaruhusiwa kuweka pesa ukiamini iko mikono salama!

Swali; Kwanini benki nyingi hawatoi mikataba kwa wateja wao? nini lengo lao kama siyo dhuluma?

Umewahi kujiuliza maswali haya!
  1. Pesa zako zikidukuliwa zikapotea ki-elektroniki nani atakulipa?
  2. Ukifika ndani ya jengo la benki ikatokea Ambushi majambazi yakapola benki na pesa zako huja- deposits utamdai nani?
  3. Benki yako ikifilisiwa pesa zako utalipwaje kwa utaratibu gani? n.k
Rejea matukio kadhaa ya wateja walio lizwa kwa scenario kama hizi; Usiombe yakukute;

Nanukuu

Mteja 1.
"Nilikuwa na pesa zangu 38 mil kwenye akaunti, bank imefilisiwa, Nimeambiwa nitalipwa 150,000/={laki na nusu) kila mwezi hadi deni liishe

Mteja 2; " Nimefuatilia pesa zangu benki ya ****** naambiwa benki imefilisiwa, wakaniambia niende B.O.T , nimefika huko wanasema watatoa laki na nusu, akaunti ilikuwa ina million 280, Nina watoto wanne nataka nikawalipie Ada! naambiwa benki imefilisiwa!

Mambo kama hayo yalipaswa kuwekwa kwenye mkataba punde tu anapofungua akaunti; kuwepo mkataba tena kwa lugha ya kiswahili ili Mteja abaki na nakala;

Na sheria za fedha B.O.T ziwekwe wazi, wanapoifilisi benki X walipe pesa za wateja immediately!

(kufilisika kwa benki siyo kufilisika kwa Mteja, Wizara ya fedha/B.O.T wekeni wazi utaratibu wa kulipwa pesa kwa matukio kama hayo, utaratibu wa sasa kwakweli umejaa dhuluma)
Mkuu upo sawa, ila ungeweza kutaka nchi kadhaa kwa uzoefu wako ambazo sheria za nchi zao zinamtaka mwenye benk ampe mkataba mteja.
 
Naunga mkono hoja bank zinatuibia sana wateja wake yani kuna makato ya ajabu ajabu hayo bank yani bora pesa zangu nifukie chini siyo kuacha bank
 
Mbaya KABISA ni wakati ukikopa kwao. Wanakwambia riba yao ni asilimi 21 tu. Lakini ukifanya mrejesho (kwa mfano kwa miaka mitatu) unakuta kiasi utakachokuwa umelipa kama RIBA KINAZIDI ASILIMIA 40 !!! Jambo la pili:-Kama mkopo wako ni wa miaka mitatu na baada ya kulipa kwa mwaka mmoja, ukipata pesa ukawaambia unataka kumaliza kulipa mkopo wote HAWAPUNGUZI ILE RIBA AMBAYO ingepaswa kupungua kwa ile miaka miwili iliyobaki. Wanakulazimisha kulipa kiasi chote kilicho kwenye jaduweli lao la ulipaji. NI WIZI MTUPU !!
 
Mm niliuelewa sana ule mjadala wa kwa nn bank ukimaliza kulipa PERSONAL LOAN hawakurudishii LOAN INSURANCE?
Mkuu kwani kwenye magari mwaka ukiisha bila kupata ajali wanakurudishia? Kuna insurance yoyote ambayo mtu huwa anarudishiwa?
 
Pia kuna wizi mdogo mdogo wa kila siku - ukiuliza salio, unalipia. Kwa wale mliobahatika kutembea nchi za watu - ni nchi gani nyingine kuna utaratibu huu wa kumkata mteja pesa kwa kuuliza salio? Mimi sijawahi kuona hiki kitu nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom