Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Aug 3, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Kipenga cha kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UWT kimepulizwa na wa kwanza kukimbilia fomu ni Mwenyekiti wa sasa Mhe. Sofia Simba akijiaminisha atapata kwa mteremko wa kupita bila kupingwa maana CCM inatawaliwa na nidhamu ya woga kwa jina la "utii", lakini hali haikuwa hivyo kwani Mhe. Mama Anne Kilango Malecela ametia timu kumpinga Mama Simba ambae "she is good for nothing"!. Mama Kilango ni just an opportunist mpiga kelele kila anapoongea as if ana uchungu wa kweli na anachopigia kelele!.

  Ila kumlinganisha na mama Simba, Kilango ni mpiganaji wa kweli kwani baada ya kubebwa pale mwanzoni, sasa amejibeba na kubebeka zaudi wakati Simba yeye ni kubebwa tuu mwanzo mwisho!.

  Leo kuna binti kijana, msomi wa haja ambaye yuko very bright upstairs kwa jina la Bi. Mayrose Kavura Majinge, naye atatupa karata yake!. Huyu ni "very promising" kuibadili UWT toka hapo ilipo na kuipaisha to next level!.

  Sasa subirini tushuhudie sarakasi za kama CCM inaendelea kuchagua "good for nothing" na kuisindikiza rasmi kaburini, au wana CCM wata opt for "oportunistic" ili kuendeleza ulaji na kupeana au this time watachagua "promising leadership" kujaribu kuiokoa CCM ambayo imeshaonyesha dalili zote za mkao wa kifo?!.

  Kwa vile sio siri, its open secret kuwa members wengi wa jf ni washabiki wa CDM, wakiwa na matumaini kuwa 2015 its their time, wajue kuwa wapiga kura wengi zaidi Tanzania ni wanawake, I doubt kama BAWACHA does realy exist!, hivyo majaaliwa ya Chadema kushinda uchaguzi wa 2015, itategemea kura za wanawake hivyo ni nani anashinda uchaguzi wa UWT!. Akirudi Mama Simba au Mama Kilango, ushindi wa Chadema ni dhahiri, ila akishinda Mayrose Kavura!, amini msiamini, ikulu mtaishia kuisikia tuu!.
  Mark my words!.

  Pasco!.

  NB. Kwa vile mimi namshabikia EL ateuliwe CCM, na kwa CDM nausupport move ya ZZK, bado nasisitiza sina chama!. Ila wale mnao amini mimi ni gamba, endeleeni kuamini hivyo kwa sababu kuwa mwana CCM sio dhambi wala kuishabikia CCM sio kosa!.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco, ningeomba utuwekea profile ya huyo mwanamama Bi. Mayrose Kavura Majinge, wengi hatumfahamu kiasi cha kubaki tunajiuliza ni nani haswaaa hadi awe tumaini jipya kwa UWT?
  [​IMG]
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mwanamke na nasema hivi:
  Sitaipigia kura ccm hata kwa dawa.
  na waalimu wengi ni wanawake na hivi
  mlivyowazalilisha nao watahama kwenye hicho chama chenu
  .
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Tunaomba CV yake? But I doubt wanyeviti wote wa UWT waliotangulia huwa ni wake/hawara wa vigogo wa CCM. Je na MayRose ni hawara/mke wa kigogo wa CCM?

  Naomba tukumbushane Wenyeviti wa UWT waliotangulia
  1 Marehemu Sophia Kawawa
  2. Anna Abdallah Msekwa
  3. Sophia Simba
  4.............
  5................
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Pasco, ndo huyu unayenpigia debe? Mbona amechoka sana jamani. Hebu tuwekee cv yake maana wife wangu ni mpiga kura huko UWT naweza kumshawishi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  huu u-mburura wa pasco ni wa kiwango cha juu sana
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Naamini Bi. Maryrose ni kiwango na siyo mkiritimba!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wa Ukenyenge, sina CV yake rasmi ila ni msomi mwenye masters. Sifa yake kuu ni kitabu fulani alichoandika kuhusu vita dhidi ya umasikini!.

  Huyu Mayrose she is real good ambaye anaweza kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CCM kwa ku invoke changes from within!.

  Kwa vile huyu ni mdada wa ukweli, bado anaamini a dying CCM can be revived kupitia UWC!. Kumbe bado hajajua, uwongo, fitna na majungu ni mtaji mkubwa wa ushindi kwenye uchaguzi wowote wa ndani ya CCM.

  Huyu Mayrose ana tatizo moja kibwa, she is too genuine hivyo kuwa too good kwa CCM, I hope baada ya uchaguzi huu wa UWT, she'll realize she is in a wrong party, anapoteza bure time, money na her very promising potentials to try reviveing a dying CCM!.

  I wish her all the best!.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mamndenyi, very unfortunately waalimu sio wanasiasa!, hawa ni watu wa wito hivyo ni wa kupelekwa pelekwa tuu!.

  Umesema kwa vile waalimu wengi ni wanawake, na kwa vile wamedhalilishwa hivyo watajitoa CCM?!. Hivi kumbe waalimu wengi ni CCM?!. Mimi nilifikiri waalimu ni just professionals hivyo have nothing to do with CCM!.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Vote For Sofia Simba.Naamini atafaa sana hasa kwa sera yake ya kuwataka kinamama kuwanyima unyumba waume zao wanaounga mkono CDM.
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wewe unajulikana kuwa ni mfuasi Sugu wa CCM uliyepewa kazi maalum ya kuleta chokochoko ndani ya CDM.Mgombea urais ndani ya CDM hakuhusu kwa sababu lengo lako kuu ni kuangamiza CDM.
  Kukusaidia soma link ifuatayo:

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa.html
   
 12. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,228
  Trophy Points: 280
  Huwa unatafuta sifa na umaarufu kwa kujipendekeza ili uendelee kupata tenda.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sophia Simba na Anna Kilango Malecela wote kama alivyokuwa mtangulizi wao Anna Abdalah wametumia "urembo" wao kufika hapo walipo kupitia kwa vigogo wa CCM akina KK, JSM na PM( kabla yake RMK).

  UWT ilikuwa inahitaji watu kama AshaRose Migiro, Prof Anna Tibaijuka au hata mama Getrude Mongella ambao hadharani wanaheshimika sana. Labda nikuulize swali dogo Pasco; kambi za akina Lowassa, Membe, Sitta zina akina nani kwenye nafasi hii nyeti?
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nasikia pia safari hii ni zamu ya mwanamke Mzanzibar kushika nafasi hii. Akina Amina Salum Ali, ..., wajiandae.
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu mkeo yupo kwenye UMOJA WA WANAWAKE WA CCM!
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  eeeti huna chama mbona umeonyesha kuwa wewe ni chama gani??
   
 17. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Yap. Tumegawana, mimi CDM mwenzangu CCM kuepuka risk ya kuweka mayai yote kwenye kikapu kimoja
   
 18. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hivi huu umoja kwanini usibadilishwe jina UWT iwe UWCCM
   
 19. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Huyu ni kichwa kinachoitajika katika nchi hii.
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kauli mbiu ya mama Simba inataka viti maalum kwa wanawake kuwa na ukomo (miaka 10) jambo hili ni miongoni mwa agenda itakayomwangusha ingawa ina maslahi kwa taifa letu.

  wapo wanaotaka viti maalum viondolewe kabisa lakini tuweka utaratibu wa kila chama kusimamisha wagombea wawili kwa kila jimbo ( mwanaume na mwanamke) ili wananchi wachague wanayemtaka. Kila chama kikitoa wagombea wawili wa jinsia tofauti inaongeza idadi ya wanawake bungeni.

  kuna wanaoamini kwamba kwa mtindo wa sasa wa kuteua mgombea mmoja kwa kila chama ni mfumo utakaondelea kutoa fursa ndogo kwa wanawake kupita kutokana na mazingira ikiwemo Rushwa na mfumo dume.
   
Loading...