Uenyekiti wa chama,kasi ya Magufuli,kupwaya kwa Mashinji na hatari upinzani nchini

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Vipo viashiria vingi vyenye kuonesha mdodororo wa siasa za upinzani nchini muda mfupi tu mara baada ya Mh Magufuli kuwa raisi wa jamuhuri ya muungano.

Tumeshuhudia mikakati pamoja na style zakisiasa zilizoukuza upinzani nchini zikigonga mwamba licha ya juhudi kubwa zilizokua zikifanywa na viongozi wa upinzani.

Mkuu alishasema si vema akatokea mtu akakwamisha serikali kutimiza ahadi zake hivyo anaetaka kufanya siasa za majukwaa asubiri 2020 ama kama atataka atumie bunge au vikao vya baraza la madiwani.

Sote tunajua kwamba upinzani nchini ulijengwa kwa mfumo wakiharakati hasa maandamano na operation mbalimbali kama operation sangara na move 4change ambazo kwa ujumla ulifanya upizani ukakua kwa kasi nchini.

Lakini sasa vyote vinatakiwa visubiri mpaka 2020 ili kupisha serikali iweze kutekeleza ilani ya uchaguzi jambo ambalo limeonesha dalili za waziwazi za mdororo wa upinzani nchini.

Lakini pia utendaji kazi uliotukuka wa raisi Magufuli umekua chanzo cha ya wapinzani kupoteza muelekeo kwani ile kete ya ufisadi serikali ya mh Magufuli inaishugulikia kwa ufanisi mkubwa.

Matumizi ya pesa za uma na utumishi wa uma sasa umekua ni kada yenye nidhamu ya hali juu jambo ambalo limeweza kurudisha imani iliopotea muda mrefu kwa wananchi kwenye serikali yao.

Licha ya dalili zote hizi mbaya juu ya mwenendo mbovu wa upinzani lakini kunaonekana kupwaya kwa uongozi hasa kwenye chama kikuu cha upinzani ambacho kwa muda sasa weledi wa katibu mkuu hasa kwenye masuala yakisiasa umekua ukitiliwa shaka.

Harakati zakumng'oa naibu spika kwenye bunge la bajeti lililopita lililokua likizungumzwa huku wakifahamu kabisa kwamba hawana akidi yakutosha kutekeleza zoezi hilo ni ishara kwamba kuna upungufu wakiueledi kwenye safu ya uongozi jambo ambalo ni hatari sana kwenye utawala makini wa Mh Magufuli.

Kete ya mwisho ni kesho ambapo Magufuli anakwenda kukabidhiwa chama na hapa tutarijie mdororo zaidi kuongezeka upande wa upinzani kwani Maguli atakwenda kurudisha imani ya watanzania kwa chama kikongwe cha CCM.

Kwa ukimya uliopo sasa kwa wapinzani inaonesha wameshakubali yaishe kwani kwa sasa hata ukitizama ile kasi ya Mh Zitto kabwe yakufanya siasa zamitandao imekua ikipungua siku hadi siku.

Kwa ujumla wapinzani wanatakiwa wachukue hatua zamakusudi ili kuokoa kufa kwa vyama vyao.
 
Haya eeh hebu tujaribu labda tutapita, haya eeh trafiki huyo . Yuko wapi, yule. Yuko wapi yuleeee
 
Haya eeh hebu tujaribu labda tutapita, haya eeh trafiki huyo . Yuko wapi, yule. Yuko wapi yuleeee
Hapiti mtu mzee Magu amekaba kila mahali na kama upinzani wasipojipanga vuzuri huwenda wakaathirika sana kipindi hiki cha utawa avwa gavufuli
 
Kwa mikakati hiyo yote yanawezekana kinaweza kufa au kuishi hivyo ni uzi tu huo co msahafu
 
Kwa mikakati hiyo yote yanawezekana kinaweza kufa au kuishi hivyo ni uzi tu huo co msahafu
Tusingependa upinzani ufe ila kwa uongozi wa katibu mkuu mashinji lazima utakua na gharama kubwa kwa CDM ambayo kwa sasa ndio upinzani wenyewe
 
kimsingi katibu mkuu bwana mashinji amepwaya mno,wakati ni sasa na kama kusipochukuliwa hatua mapema huenda chadema ikashuka kisiasa, huu ndio ukweli na lazima usemwe
 
Back
Top Bottom