Uenyekiti CHADEMA ni sawa na tunda la mti wa katikati pale Eden, ukiligusa tu unatupwa nje ya Bustani kama Zitto, Sumaye na Mwambe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,604
141,421
Kiukweli kitendawili cha nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA ni kigumu sana kukitegua.

Kwanini Mwenyekiti yuko madarakani kwa zaidi ya miaka 20, ndilo swali kuu!

Je, ni demokrasia, ubabe au udikteta?

Kwanini kila aliyetamani kuwa Mwenyekiti wa Chadema leo hii hayuko katika chama hicho chenye makao yake mtaa wa Ufipa?

Alianza Wangwe, akaja Zitto na kisha wamefuatia Mzee Sumaye na kinara wa Siasa za kusini Cecil Mwambe.

Binafsi naifananisha nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na tunda la mti wa katikati ambalo Mungu alimwambia Adam wa kwanza asilile.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Nilisema hili mapema sana! Jf wakawa wanafuta michango yangu kuiondoa hum jf ili wana jf wasiisome, walizani wa wasiisome, nilijua una mtu wanamfurahisha ila hawakuzingatia nilichokisema!

labda nikumbushie kwa ufupi.
Nilisema , siasa nibiashara nzuri sana ukiipatia na nikatolea mfano kwa chadema kuwa nikibubu cha mbowee kupiga pesa, ndo maana anaona akiondoka pale masrahi yake na watu wake yataharibika na si masrahi ya chama.

nikatoa tahadhari ya chama kupukutika kwa kuwa viongozi waandamizi wa chama pamoja na wabunge walichoka kuchangishwa bila masrahi ya chama.
wanachama wamekuwa wakishuhudia matumizi ya fedha hovyo kwa baadhi ya watu ndani ya chama.
lakini pia wanachama na wabunge wameshuhudia teuzi za viongozi kwa lengo la ukaribu na mwenyekiti na kamati yke

Sasa chama kinaisha kwahoja rahisi eti WASALITI!!! mara wananunuliwa wanashawishiwa bila kuchunguza tatizo.
Narudia kuwaambia tatizo ni mbowe na mapato ya chama wataisha wte na watakao baki niwale wanaotafuna pesa tu.

CHADEMA amka fukuza mbowe na genge lake muokoe chama.
Ule msemo wa mbowe tuvushe umebadirika umekuwa mbowe tumalize.
 
Masanjaone, Unge edit kwanza hizo hisia zako.

Kwani CAG huwa hafanyi ukaguzi CDM? haya madai yenu ya kitoto Mbowe anaiba but hamuwezi kuthibitisha popote ikiwemo mahakamani hamchoki kuimba kila siku? mara Mbowe anawaweka ndugu zake, unataka kusema Mbowe ana ndugu mikoa yote Tz?.. na kama ana kundi lake tuambie na kundi jingine ni la wakina nani?

Habari ya chama kupukutika nayo story tu, coz wote wanaokimbia wakati huu wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi, sasa wewe hii sababu yako sijui umeitoa wapi, au huwa husikilizi vyombo vya habari?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist.

Hapajatokea mgombea mwenye ushawishi kumshinda Mbowe hasa wakati hii tulionao chini ya utawala wa awamu ya tano, wote tunaona wanavyohangaika na Mbowe, kuanzia kuharibu mali zake (mashamba, billicanas) mpaka kumsweka ndani hovyo kwa kesi za kutengeneza.

Walifikia hatua ya kutaka kumuua kwa risasi Mungu akamponya, bahati mbaya akafariki mtoto wa watu Mungu amlaze pema. Kwenye mazingira kama haya Mbowe atashinda sana, mpaka achoke mwenyewe.

Huyo Zitto alinyimwa uwenyekiti wakati ule alikuwa anafanya vikao vya siri na Kikwete, watu wakajua, then mtu wa aina hiyo ndio apewe uenyekiti wa CHADEMA?

Mwambe, huyo bado mchanga, alijaribu akashindwa, na CHADEMA wangekuwa wajinga kama wangempa uenyekiti wa chama, kuthibitisha asivyo mvumilivu leo keshakimbilia CCM.

Wote uliowaorodhesha hapo walipigiwa kura wakashindwa, wajumbe wanajitambua, wanajua wapi wanataka kuelekea kama chama chini ya mwenyekiti Mbowe.

Sasa kama hiyo sio demokrasia sijui kwako ni nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
..hata ccm huwezi kum-challenge mwenyekiti wa chama taifa aliyeko madarakani.

..John Shibuda alitimka CCM baada ya kufanyiwa figusu alipoonyesha nia ya kugombea Uenyekiti.

..Cecil Mwambe hakuwa tayari kumpiku Freeman Mbowe. He had a chance, chama kilimpitisha, lakini hakuwa amejijenga kwa wanachama wa CDM
 
johnthebaptist,
Ulishawahi jiuliza kwa nini ccm wanang'ang'ania kututawala leo zaidi ya miaka 50 na wanatishia amani itatoweka wakishindwa?

Na lini kulikuwa na ushindani wa nafasi ya mwenyekiti wa ccm taifa ? Kama Membe tu katamani kugombea urais kaitwa kuhojiwa,vipi akichukua na kurejesha fomu?
 
Membe chukua form Urais 2020 kwa CCM; hakuna kipengele chochote kile ndani ya katiba ya CCM kitakachokuzuia.
 
johnthebaptist,
Sumaye kagombea uwenyekiti wa kanda tu akiwa mgombea pekee kachemka...!! Aibu kubwa!!

Sasa mlitaka CHADEMA wampe kura hewa kisa alishakuwaga Waziri Mkuu?
 
Uzuri ulioje

Tunasubiria Sumaye na Mwambe

1. Wagombee Urais huko ccm,

2. Wasipopitishwa ccm tuone, watalalama?

3. Wasipopitishwa ccm watajiondoa ccm
 
Kinachoshangaza ni kwamba wenye chama chao wanaamini hakuna mwenye uwezo wa kukiua chama chao halafu ukifika wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wanakuambia bila Mbowe hakuna CHADEMA

Sasa kama chama ni mtu mmoja tu si hata teja anaweza kuiua CHADEMA!
 
Chacha na Zitto je?!

..I dont think Chacha was a serious candidate.

..Zitto angeweza kuwa mwenyekiti, lakini alikuwa hajajijenga ktk chama, na alikosa subira.

..Cecil Mwambe alipigiwa kura na akashindwa kwa hiyo huwezi kumlaumu Mbowe au chama.

..lakini Cecil kuhama chama namna hii unadhani alistahili IMANI ya wanachadema?
 
Kwa sababu uwenyekiti sio lazima chadema tu na wamerudi ccm basi wagombee uenyekiti hapo ccm .Au unaonaje boss?

Nakuunga mkono. Kwa kuwa tayari wamerudi walikotoka wachukue fomu za kugombea na nafasi ya Mwenyeki wa CCM Taifa kama wao wanaume kweli!!!
 
Back
Top Bottom