Msulibasi
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,836
- 7,492
Kwa miaka mingi nimekuwa nikifuatilia namna Chadema inavyo jitangaza na kutafuta ufuasi. Katika jambo linalonipa maswali ni kutosikika kwa idara yake ya uenezi.
Sijafahamu vizuri kitengo cha uenezi kama kipo kwa jina jingine au hakipo na shughuli zake zimeelekezwa kwenye ngazi ipi. Ukifuatilia CCM kitengo cha uenezi miaka yote kinapewa nguvu na penda usipende, mwenezi wa CCM anafahamika katika ngazi ya taifa na MIKOA mikubwa.
Sijafahamu kama tatizo la Chadema ni muundo, mfumo wa utendaji au kumekuwa na waenezi dhaifu miaka yote.
Kuna baadhi ya majina kama Mtelemwa, Mushi, Makene sifahamu hawa ni maafisa habari au waenezi.
Kama kweli Chadema hawana hiyo ngazi ya uenezi basi muundo wao unawapunguzia nguvu ya kujiuza kwa wananchi. Ni vizuri Chadema wakatathmini muundo na nguvu wanayopaswa kuzipa idara zake .
Waenezi ni muhimu ngazi zote kuanzia taifa, Kanda, Mikoa , Wilaya, Tarafa na Kata. Si nafasi ya kupuuza.