''Uende kunishtaki wakati nakulinda na jeshi langu?'' Tunavutia wawekezaji gani na kauli kama hizi?

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,964
Hotuba ya rais wakati akikabidhiwa ripoti ya pili ilikuwa ni attention ya vyombo vingi vya habari wadau mbalimbali na potential investors pia Rais anasisitiza juu ya kuvutia wawekezaji, kuwasamehe kodi za mwanzo na kusisitiza mara kwa mara mtendaji ndani ya serikali yake atakayeleta vikwazo kwa muwekezaji atamuondoa

Watu watasema tunajadili details zisizo na msingi kwenye hotuba ila kwa Investors anaye-contemplate juu ya kuja Tanzania attention yake inakuwa juu ya rais anavyodeal na wawekezaji waliopo nchini ndio anajua nchi hii ni rafiki ama sio rafiki na sio kusikiliza maneno anayomwambia rais akiwa anaongea nae

Kauli hiyo inatoa picha kuwa rais ni mbabe, asiyesikiliza reason ila akiktuhumu juu ya lolote unatakiwa ukiri na umlipe

Chukulia mfano huu
Umekodi shamba unapanda mahindi, makubaliano na mwenye shamba ni kuwa kila gunia 100 utakazovuna utamlipa gunia 2,
Mwenye shamba anakutuhumu unavuna mahindi mengi zaidi unamficha ili umpe gawio dogo, na kingine ni makubaliano ya gawio la kwanza hayapo fair, na amekuzuia kulima walakutoa mahindi

Mwenye shamba huyo anakuambia usithubutu kumshtaki kwa sababu una vifaa vyako shambani kwake...unatakiwa ukubali tuhuma zilivyo na na ulipe

Mwenye shamba kama huyo kama kuna mtu aliyekuwa anawaza kukodi shamba kwake ataenda kwake au atafikiria kukodi kwa mwingine na wenye shamba ni wengi?
 
Mnategemea wawekezaji?? Mtawekeza kwenye chuki na visasi.....miaka 10 mtaishia kujenga barabara na madaraja....ambayo ni kazi ya waziri 1 tu sio serikali nzima vingine vimesimama.....hadi uchumi umesimama!! Rahisi ni kipawa na kipaji sio kuokotana barabarani hata wenye ma fil yao........!!
 
Mnawapa watu nchi wenye ma file yao kuleee mlimani....?? Mnategemea wawekezaji?? Mtawekeza kwenye chuki na visasi.....miaka 10 mtaishia kujenga barabara na madaraja....ambayo ni kazi ya waziri 1 tu sio serikali nzima vingine vimesimama.....hadi uchumi umesimama!! Rahisi ni kipawa na kipaji sio kuokotana barabarani hata wenye ma fil yao........!!
Huogopi kuitwa mchochezi?

Kwa kuwa jamaa hataki kabisa kukosolewa.....

Na kwa kila anayemkosoa, kwake yeye anamuona mchochezi, siyo mzalendo na asiyeitakia mema nchi hii!

Hivi yule Mbunge wa Arusha mjini kilichomfanya asote rumande kwa miezi 4 si kauli yake tu kwa haya mambo yanayoendelea hapa nchini kwetu?
 
Hii dhana ya kusema tutafukuza wawekezaji ni dhana potofu au inapigiwa chapuo tu la kisiasa lakini haina mantiki yoyote.

Hii ni dhana inayotumiwa sana na makampuni ya kibeberu ili yafutiwe kodi au yapewe nafuu kubwa ya kodi.

Nchi yoyote yenye maliasili zinazotafutwa kwa ''udi na uvumba'' haiwezi kukosa wawekezaji.

Tanzania ina maliasili zinazotafutwa kwa 'udi na uvumba' katika masoko ya Ulaya na Marekani.

Huko Libya pamoja na vita vinavyoendelea lakini makampuni ya nchi za Magharibi yanapigana vikumbo ili kuwekeza pamoja na kwamba mazingira ya uwekezaji sio endelevu.

Nenda DRC ukaone jinsi ambavyo wawekezaji wanapigana vikumbo katika migodi pamoja na kwamba nchi iko vitani katika maeneo yenye madini.

Nguo nyingi katika masoko ya Ulaya zinatoka katika nchi za Bangladesh na Turkey ambako wawekezaji kutoka Ulaya wamewekeza pamoja na kuwa kuna vikundi vya kigaidi ambavyo ni active.

Nenda Iraq, nenda Egypt and the list goes on and on...
 
KITU NILICHOGUNDUA NI KUWA CCM BADO WANAUMIZWA NA KITENDO CHA LISSU KUWA RAIS WA WANASHERIA,WALIKUWA WANATAFUTA PA KUSHUSHIA HASIRA ZAO

Ila mimi bado nasubiri siku moja Lissu aongee kama rais wa chama cha wanasheria, lkn kila nikimsikiliza naona anaongea kama mwanaharakati wa sheria na akisimama kwa nafasi yake ya mwanasheria wa chama kikuu cha upinzani. Baadhi ya siku akiwa anaongea kwa kutenganisha hizo kofia zake mbili (kwa kuacha uchama) na kuongea kama raisi wa wanasheria itakua ni bora zaidi.
 
Hii dhana ya kusema tutafukuza wawekezaji ni dhana potofu au inapigiwa chapuo tu la kisiasa lakini haina mantiki yoyote.

Hii ni dhana inayotumiwa sana na makampuni ya kibeberu ili yafutiwe kodi au yapewe nafuu kubwa ya kodi.

Nchi yoyote yenye maliasili zinazotafutwa kwa ''udi na uvumba'' haiwezi kukosa wawekezaji.

Tanzania ina maliasili zinazotafutwa kwa 'udi na uvumba' katika masoko ya Ulaya na Marekani.

Huko Libya pamoja na vita vinavyoendelea lakini makampuni ya nchi za Magharibi yanapigana vikumbo ili kuwekeza pamoja na kwamba mazingira ya uwekezaji sio endelevu.

Nenda DRC ukaone jinsi ambavyo wawekezaji wanapigana vikumbo katika migodi pamoja na kwamba nchi iko vitani katika maeneo yenye madini.

Nguo nyingi katika masoko ya Ulaya zinatoka katika nchi za Bangladesh na Turkey ambako wawekezaji kutoka Ulaya wamewekeza pamoja na kuwa kuna vikundi vya kigaidi ambavyo ni active.

Nenda Iraq, nenda Egypt and the list goes on and on...
Kweli kabisa...pongezi kwako.@msemaji ukweli
 
Nchi zetu nyingi za kiafrika Tanzania ikiwa mojawapo zinaogelea katika dimbwi la umaskini huku zimefungwa nira za ukoloni mamboleo kwa kuwatumia vibaraka {baadhi ya viongozi wenye uchu wa ukwasi,madaraka}kutimiliza vitendo endelevu vya unyonyaji,ukandamizaji,wizi na uharamia wa rasilimali adhim.Ujambazi wa rasilimali umekuwa ukibatizwa majina mazuri ya kuvutia na kutia matumaini raia maskini waliokalia utajiri.
 
Ila mimi bado nasubiri siku moja Lissu aongee kama rais wa chama cha wanasheria, lkn kila nikimsikiliza naona anaongea kama mwanaharakati wa sheria na akisimama kwa nafasi yake ya mwanasheria wa chama kikuu cha upinzani. Baadhi ya siku akiwa anaongea kwa kutenganisha hizo kofia zake mbili (kwa kuacha uchama) na kuongea kama raisi wa wanasheria itakua ni bora zaidi.

Kweli mkuu.
 
Back
Top Bottom