Uelewe mfumo wa 3-4-3 anaotumia Antonio Conte

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,553
37,710
Wana JF,

Imekuwa gumzo duniani kuhusu mfumo huu wa 3 - 4 - 3. Mfumo huu si mpya bali ulikuwepo na makocha wengi wanauelewa ila huwa hawapendi kuutumia sababu unahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo ufuatao:

3-4-3.jpg

Mabeki 3
Hawa mabeki 3 lazima wawe warefu na wepesi, wawe na uzoefu na uwezo mkubwa mno wa kucheza mipira hasa ya juu. Kwenye timu ya Chelsea mabeki hawa watatu ni

X3 (Azpilicueta X5 (David Luis) X2 (Gary Cahil)

Viungo 4
X4 (Ngolo Kante) X8 (Nemanja Matic) X7 (Victor Moses) X6 (Alonso)

Viungo hawa 4 wamegawanyika sehemu kuu mbili - 1. Viungo wa kati; 2. viungo wa pembeni.
Viungo wa Kati yaani X4 (Ngolo Kante) na X8 yaani (Nemanja Matic)
Hawa watakuwa na majukumu makubwa ya ukabaji na kuhakikisha wanamiliki mpira ili kuipa timu uwezo wa kwenda mbele kushambulia - X4 atakuwa nyuma kidogo kuhakikisha Ulinzi unaimarishwa na X8 atakuwa mbele kupeleka mashambulizi - hawa watacheza kwa uelewano kwamba kama X4 atakwenda mbele kuongeza mashambuzi basi X8 atarudi kuweka cover nyuma. Mfano ni ile game ya Man U - like goli alilofunga X4 (Ngolo Kante) ni uhakikishio wa ushirikiano wao kwenye kiungo cha Chelsea.

Viungo wa Pembeni yaani X6 (Alonso) na X7 (Super Victor Moses).

X7 (Victor Moses) ni kama amezaliwa upya, pongezi kubwa na Conte kumwezesha Moses kufikia kwenye ubora wake, Huyu atakuwa na majukumu ya Ulinzi upande wa Kulia, atahakikisha anasaidiana kwa kiasi na X2 kuhakikisha eneo lote la kulia ni salama, kama timu haina mpira basi X7 atarudi nyumba upande wa kulia kuhakikisha wapinzani hawapiti kirahsi kufanya maangamizi. Ubora wa mfumo huu utategemea uwezo wa X7 kupanda na kushuka - yaani awe na mapafu ya mbwa kwani kama itatokea akichoka tu ama hayupo kwenye ubora wake basi timu inaweza kupitwa kirahisi mno kupitia upande huu. So far X7 amefanya kazi kubwa mno.

X6 (Alonso); Huyu jamaa ni jembe, yupo kwenye ubora wake timilifu, kazi ya X6 ni kama ya X7 kuhakikisha ulinzi sehemu ya kushoto akisaidiana na X3. Kama timu haina mpira basi X3 atashuka zaidi kuweka cover upande wake huo wa kushoto, na kama timu ina mpira basi atapanda mbele kuongeza mashambulizi.

Washambuliaji yaani X11 (Pedro) X10 (Costa); X9 (Hazard)

X11 (Pedro); kazi yake ni kukimbiza upande huo wa kushoto, wakati timu haina mpira anaweza kushuka hadi eneo la kati kuhakikisha mpira unapatikana kwa haraka, X11 kwenye mfumo huu lazima awe mwenye mbio na kasi na uwezo kwa kuwapita ma-defenders wa timu pinzani walau wawili ama watatu - hili X11 (Pendro) analiweza saana, kukuhakikishia hilo angalia goli alilofunga kwenye game ya Tonteham - aliwageuza mabeki 2 kabla hawajarudi sawa kujua nini kimetokea mpira ulikuwa unaninginia wavuni.

X10 (Costa) Finisher, anatakiwa awe na nguvu za Kichwa, miguu - kuhakikisha anamalizia cross toka kushoto ama kulia - kwa hili X10 (Costa) kalifanya vizuri na mpaka sasa ana magori 10

X9 ( Hazaaaaaard) Huyu na wewe utamalizia - sitaki kusema sana.

Ubora wa huu mfumo huu:

1. Washambuliaji yaani X11, X10 na X9 mara kwa mara watakuwa mbele hasa pembeni kuwasumbua sumbua mabeki, as resulsts mabeki wanaweza kujikuta wakifanya makosa ama kugokoa.

2. Viungo hawa 4 wanaweza kuongeza upana aka kufungua uwanja

3. Viungo na washambuliaji wanaweza kubadilishana nafasi hasa za pembeni hii kuwapa kazi kubwa mabeki kukabiliana nao. Hapa tumeshaona jinsi Hazard, anavyo switch postions na Pedro ama hata Costa

4. Ulinzi unakuwa madhubuti saha hasa katikati - mmeona jinsi David Luis na Cahil wanavyopiga kazi.

Udhaifu wa mfumo huu:

1. Wachezaji wa kiungo wanaweza kutengeneza gap (nafasi) katikati yao, hasa X7 na X6 wanapocheza nje ya sehemu yao, nafasi kubwa kati yao inaweza kusababisha timu pinzani kuitumia na kuwaadhibu mara moja.

2. Viungo lazima wapande mbele wa uangalifu mkubwa hasa wakati wa ushambuliaji, kama wakijisahau ama kupoteza mpira basi nafasi kubwa itakuwepo kati yao na mabeki, na hii nafasi itatumika na timu pinzani kuwaadhibu aka Counter attack.

Mfumo huu unahitaji nidhamu ya hali juu, kosa moja la mchezaji linaweza kuadhibu timu wakati wowote ule na ndiyo maana makocha wengi hawapendi sana kutumia mfumo huu kwa kuogopa human errors za wachezaji!!

Mambo Makuu 4 aliyoyafanya Antonio Conte kabla ya kuanza kuutumia mfumo huu:

1. Alihakikisha ana mabeki wazuri (Athletic defenders) wanaoweza kucheza mipira ya juu na chini wa ustadi mkubwa.
Hapa anawatengeneza vizuri (shaping) kina Luis, Cahil na Azpilicueta.

2. Nidhamu kwa wachezaji wote hasa wa Kiungo unahitajika sana ili kupunguza uwezekano wa kupigwa counter attack, Hapa alimwongeza Ngolo konte na kumrudisha Matic kwenye ubora wake.

3. Wachezaji wa pembeni wenye uwezo mkubwa wa kuwapita mabeki walau wawili ama watatu (Ability to dribble) nakupiga crosses ndani. Hapa alimkuta Hazard, William, Pedro akasema safi sana, akamtengeneza Moses ambaye alikuwepo kwa mkopo kila mwaka sababu makocha waliopita hawakuweza kujua nini ubora wake.

4. Mwisho kabisa ni kuhakikisha mawasiliano mazuri mno kati ya Mabeki na Viungo - hapa ndipo kwenye siri ya mafanikio.

Jumuisho.

Je unafikiri Mkwasa sasa ni muda wa kutumia mfumo huu??? je tunao wachezaji wenye uweo huu nchini kwa sifa nilizozitoa hapo juu??

Tujadili kwa hoja!!! namalizia kutoa hongera kwa Conte kuteta starehe siku za weekend kwa washabiki wa Chelsea.
 
Wana JF,

Imekuwa gumzo duniani kuhusu mfumo huu wa 3 - 4 - 3. Mfumo huu si mpya bali ulikuwepo na makocha wengi wanauelewa ila huwa hawapendi kuutumia sababu unahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo ufuatao:

3-4-3.jpg

Mabeki 3
Hawa mabeki 3 lazima wawe warefu na wepesi, wawe na uzoefu na uwezo mkubwa mno wa kucheza mipira hasa ya juu. Kwenye timu ya Chelsea mabeki hawa watatu ni
Big up sana Mkuu. I wish JF ingekuwa na watu wengi kama wewe.
 
Na mfumo huo waligongwa 3 na washika bunduki
Walikuwa hawajaanza kuutumia huu mfumo. In fact walihamia kwenye hii mbinu baada ya kutandikwa tatu na wameshinda mechi 7 mfululizo since then.

3-4-3 mara nyingi imekuwa inageuka kuwa 5-3-2 hasa pale wanapokuwa wanashambuliwa. Upeo wa Conte umesaidia saana maana yeye anakuwa kama mchezaji wa 13 wa Chelsea. Anausoma mchezo mwanzo mwisho na anawapigia kelele akina Alonso na Moses wakimbie faster kurudi nyuma kusaidia ile beki 3 team ikishakuwa under siege.

System hii ni ngumu na inahitaji practice ya kutosha. Everton walijaribu kuiiga walipocheza na Chelsea na matokeo yake wakalambwa goli za kutosha. Ninajua Man City watacheza 3-4-3 weekend hii ili kumatch wanachofanya Chelsea na mwisho wa siku individual brilliance itawin ile game.
 
west ham united ndiyo kiboko yenu nyie wacheza blues....wagonga nyundo hawapendagi ujinga wenu
 
Binafs ndo mfumo nnaoutumia kwenye game, napiga mbaya kabisa!
Kasoro zake ni ;kucheza na timu inayo defence
Kucheza na timu inayopiga sana pasi mbele,
Ukutane na forwad zenye speed
 
Kikosi kilekile kila match subir trh 3, wenzenu wamerotate na wachezaj 37.
Mkuu hii si hoja, Chelsea ina kikosi kikubwa mno, alichofanya Conte so far ni kuchagua first 11 ya kuuanza huu mfumo mpya, huwezi kubadili mfumo kisha hapo hapo ukaanza ku rotate wachezaji ukifanya hivyo utakosa kila kitu. Mfumo huo wameutumia mechi 7 sasa, wamefunga magoli zaidi ya 15 na kuruhusu moja tu lile la Tonteham. Kwa Sasa unaweza kuona Conte kaanza kuwapa dakika chache chache wachezaji wengine Ivanovic, Oscar na Wailliam. Conte ana uzoefu mkubwa na mfumo huu kwani aliutumia akiwa Juventus na baadaye kwenye timu ya Taifa ya Italy.
 
Unahis kwa kikosi cha Chelsea hasa Mabeki wanaweza wakastahimili kwa muda gan huu mfumo?
 
Unahis kwa kikosi cha Chelsea hasa Mabeki wanaweza wakastahimili kwa muda gan huu mfumo?
Bado mabeki wa Chelsea si wa kubeza hata kidogo kwani ndiyo hao hao waliowapa chelsea ubingwa mwaka juzi, ubora wa Luis, Terry, Cahil. Ivanovic, Azipilicueta, Alonso na Bwana mdogo Zuma si wa kuhoji, kilichokosekana chelsea mwaka jana ilikuwa ni weakness kwenye benchi la ufumdi. Mabeki 7 , you can't ask for more!!
 
Mkuu hii si hoja, Chelsea ina kikosi kikubwa mno, alichofanya Conte so far ni kuchagua first 11 ya kuuanza huu mfumo mpya, huwezi kubadili mfumo kisha hapo hapo ukaanza ku rotate wachezaji ukifanya hivyo utakosa kila kitu. Mfumo huo wameutumia mechi 7 sasa, wamefunga magoli zaidi ya 15 na kuruhusu moja tu lile la Tonteham. Kwa Sasa unaweza kuona Conte kaanza kuwapa dakika chache chache wachezaji wengine Ivanovic, Oscar na Wailliam. Conte ana uzoefu mkubwa na mfumo huu kwani aliutumia akiwa Juventus na baadaye kwenye timu ya Taifa ya Italy.
Nimependa majibu haya mazuri kama die hard fan wa Chelsea, big up
 
Bado mabeki wa Chelsea si wa kubeza hata kidogo kwani ndiyo hao hao waliowapa chelsea ubingwa mwaka juzi, ubora wa Luis, Terry, Cahil. Ivanovic, Azipilicueta, Alonso na Bwana mdogo Zuma si wa kuhoji, kilichokosekana chelsea mwaka jana ilikuwa ni weakness kwenye benchi la ufumdi. Mabeki 7 , you can't ask for more!!
FUSO , you speak my words!! Thanks
 
Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom