Ndugu wana JF
Nimepitia threads nyingi humu kuhusu swala la kupunguzwa kwa kiwango cha kodi ya wafanyakazi kutoka 11% hadi 9%. Kwa ujumla watu wengi wamepongeza hatua hiyo wakiwemo hata watu wa TUCTA, na wasomi mbalimbali. Sababu zinazotolewa ni kwamba punguzo hilo litamuongezea mfanyakazi kipato na kumpunguzia machungu ya maisha.
TUCTA wameenda mbali zaidi wakasema wamekua wakipigania swala hili kwa siku nyingi. Nia yangu hapa sio kubeza jitihada hizi, ila kinachonishangaza ni kwa jisnsi gani punguzo la 2% au shs 1,100 kwa watu wa mshahara chini ya 360,000 na punguzo la shs 3,800 kwa wale wenye mishahara inayozidi 360,000 utakavyomsaidia mfanyakazi kupunguza machungu ya maisha magumu.
Hivi kweli wafanyakazi walivyoshangilia pale uwanjani walijua punguzo hilo ni kati ya shs.1,100 hadi 3,800 tuu?. Kama ndivyo, basi kuna haja ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu mfumo wa kukokotoa PAYE ulivyo. Vile vile watu wa TUCTA wangeelekeza nguvu zaidi kupigania punguzo la kodi kwa makundi yote yalioko kwenye viwango tofauti vya mishahara, na kwakua kwa wale watu wa chini hata ukipunguza kwa asilimia 10% bado tuu punguzo hilo halitazidi 30,000 ni bora wangependekeza kiwango kile cha chini cha mshahara usiokatwa kodi (tax thresholds) kiongezwe kutoka 170,000 ya sasa walao kifike 400,000/=
Kwa wale wa kiwango cha juu kodi ya 30% kwa mshahara unaozidi 720,000 bado ni kubwa sana. Ikumbukwe kuwa mfanyakazi hawezi kukwepa kodi kama wanavyofanya wafanya biashara, pia ukiacha hiyo 30% anayolipa kama PAYE, pia anakutana na kodi ya VAT kila anaponunua bidhaa, 18%, pia kuna kodi nyingine nyingi (indirect taxes) anazokutana nazo sehemu mbalimbali.
Nia ya Mheshimiwa Raisi ya kuwapa unafuu wa maisha wafanyakazi haitafikiwa kama kweli unafuu huo unampa punguzo la kati ya 1,100 hadi 3,800 tuu kwa mwezi na hasa ukizingatia bei za bidhaa na huduma pia zimepanda, na pia shilingi yetu imeendelea kushuka thamani.
Kwa upande wa Zanzibar kima cha chini kimepanda kwa 100% kutoka laki 150,000 hadi 300,000.
Ingawaje sio mshahara mkubwa huo lakini hii ni step kubwa sana na yenye mashiko. Huku bara tungetegema kusikia pia mishahara ikipanda na sio tuu kuishia kwenye punguzo la kodi ambalo halitoshi hata kununua kilo moja ya nyama.
Naomba wahusika waliangalie swala hili kwa umakini mkubwa, kwani bado bunge la budget linaendelea ili waweze kulipatia ufumbuzi wenye mashiko.
Naomba kuwakilisha.