UELEWA mdogo katika masuala ya kodi umetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi kuona ulipaji kodi ni mzigo

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
74b93ad9fa8deec1b6e308c21c8464c9.png

UELEWA mdogo katika masuala ya kodi umetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi kuona ulipaji kodi ni mzigo. Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mjini Arusha, Osa Elimu Mkuu wa TRA, Rose Mahendeka alisema wafanyabiashara na wananchi wanapaswa kufahamu kuwa kodi ndio chanzo kikuu cha mapato ya serikali. “Ni vema jamii ifahamu kuwa bila kodi huduma za kijamii haziwezi kupatikana, malipo ya mishahara, huduma za hospitali, barabara na madaraja, zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na kodi kutoka kwa wananchi wake”, alisema.

Pamoja na hayo osa elimu huyo alisema licha ya serikali kutumia misaada na mikopo kwa shughuli za kimaende- leo, lakini ingependa kutumia kodi kuondoka na mzigo wa riba zinazotokana na mikopo na pia kuepuka kuomba na kutegemea misaada. “Ni vyema wananchi wakaelewa kuwa suala la kulipa kodi sio la hiari, kodi ni tozo la lazima, kila mwananchi anapaswa kuichangia Serikali kwa kipato alichonacho”, alisema.
Awali akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alisema lengo la semina hiyo ni kujaribu kuondoa tofauti iliyopo kati ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo ambayo sehemu kubwa inachangiwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya wafanyabiashara.

“Ni matumaini yetu kuwa semina hii itasaidia kuwafanya wafanyabiashara na TRA kuwa maraki na pia kusaidia wafanyabiashara kufahamu haki zao na aina mbalimbali za kodi kutakakopelekea ulipaji wa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya nchi yetu”, alisema Bwana Ndunguru. Aliongeza kuwa wao ni wakala wanakusanya maduhuli ya serikali hivyo akasema wafanyabiashara na wananchi wanaweza kwenda katika benki hiyo kulipa maduhukli na kodi mbalimbali za serikali. Mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria semina hiyo, Rowland Phares alisema changamoto kubwa waipatayo ni uelewa mdogo juu ya taratibu, sheria na kanuni za TRA
 
View attachment 906913

Tatizo sio kulipa?? Tatizo ni pale Waziri anapotangaA mwisho wa kulipa madeni ni June 2019? Na TRA kukazimisha makusanyo kwa kufunga account za watu...kabla ya huo muda.
 
Back
Top Bottom