Uelekeo wa tizamo huu wa Elimu yetu na Madhara yake hapo kesho...Tuanahitaji kujisahihisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uelekeo wa tizamo huu wa Elimu yetu na Madhara yake hapo kesho...Tuanahitaji kujisahihisha

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by jaxonwaziri, Apr 13, 2012.

 1. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Nimeamini, hatuna haja ya kupiga kelele sana na kuwanyooshea viongozi wa serikali ya nchi yetu vidole kwakuwa wao wanatoka katika 'pool' yetu watanzania tusio na upeo wa kuona mbali, kufikiri kwa kina na kupima kabla ya kutenda ama kushabikia. Kwa nini nasema hivi? Hebu fikiria yafuatayo:
  1. Siku za hivi karibuni, umegundua ni kwa kasi gani shule za binafsi zinaongezeka?
  2. Siku za karibuni umechunguza hali na hadhi ya shule za serikali na kasi ya kuongezeka kwake?
  3.Siku za hivi karibuni umechunguza na kukagua ubora wa elimu inayotolewa kwa shule za binafsi na serikali? Zinatofautiana? Zinashabiiana?
  4. Siku za hivi karibuni umejiuliza: Iwapo mitaala ya shule zetu nchini Tanzania inafanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya kiuchumi, kibiashara na kiteknolojia katika karne hii? How often? Mara ya mwisho hili kufanyika Tanzania ilikua lini?
  5. Hizi shule zinazoibuka kila siku (mushrooming schools) na ada wanazotoza, miaka mitano ijayo hali itakuaje?

  Ndugu zangu kuna mengi sana ya kujiuliza kwanye hii sekta ya elimu ila ninataka kuzungumzia neno moja tu nalo ni: Mabadiliko huanza na wewe na si kwa serikali. Nitakupa mfano halisi wa hili.
  Wengi wetu tumekuwa wepesi wa kushabikia kupeleka watoto katika shule binafsi ambapo si ajabu sana kusikia ada ya chekechea si chini ya Shilingi milioni moja za kitanzania kwa mwaka na mwaka mmoja una mihula mitatu bila kujihoji kwanza umakini wa hatua kama hizi. Wengi wetu imekua ni fasheni, ni namna ya kuonyesha kuwa hatuko nyuma, hatujaachwa nyuma n.k n.k n.k...! Tumekuwa tunachekelea pale shule za umma zilizopo mitaani kwetu zinapokuwa zinakosa waalimu,vitabu na madawati. Tumekuwa na kejeli sana pale shule hizi zinapohitaji michango kwa ajili ya kujikwamua kisa eti serikali imeshatangaza kuwa elimu ni bure...!

  Sasa angalia: Katika kila mzazi anaelipa ada ya Tsh. 1,000,000 + ngarama nyingine kama usafiri n.k, tungeungana na kukubali kuchangia shule zetu hizi kiasi cha Tshs 200,000 tu kwa mwaka ili kuboresha vyumba vya madarasa, madawati na vitabu, pia kuanzisha mifuko ya motisha kwa waalimu- mifuko ambayo itakua inasimamiwa na bodi za shule unadhani shule zetu hizi za umma zingekuwa wapi leo? Isitoshe hata kwa zile shule watu wengi wanapolipa mamilioni kama ada, wanapokuja katika mahafali ya shule hizi huwa wanachangishwa pia - over and above hayo mamilioni ya ada walizolipa!

  Uzuri wa shule hizi za umma ni kuwa zipo karibu na makazi yetu hivyo hata gharama za usafiri zitaweza kupungua. Pia hii itasaidia kupunguza kero za shule hizi za 'kiajabu ajabu' za binafsi, siku hizi kwakua shule binafsi ni biashara, watu hawaangalii tena kuwa shule zinajengwa wapi - unakuta mtu anaamua kugeuza nyumba iliyokuwa imepangwa kuwa makazi ya mtu kuwa eti shule, pembeni kuna gesti, kulia kuna baa na mbele kuna barabara. Hakuna viwanja vya michezo, mfumo wa maji safi na taka ni mkituko na bado wazazi wanang'ang'ana kulipa mamilioni kama mazuzu!

  Je, kama sisi watanzania tunafanya haya tunatoa wapi ujasiri wa kuikemea serikali kuwa ina - biased vipaumbele? Ama ina matumizi mabaya ya fedha za umma? What if tukichunguzana na kuchunguza hali hizi - hatutagundua kuwa huku ni kutumia vipato vyetu isivyo sahihi? Nina baadhi ya watu wameanza kulalalmika eti ada zinazotozwa na shule binafsi ni kubwa serikali iingilie kati, mlitumwa? Mbona watanzania hatutumii akili tulizopewa na Mungu?

  Wenzetu wa mijini hasa hasa wahindi walianza kuliona hili, wakawekeza kwenye shule zilizokuwa jirani na makazi yao. Matokeo yake zikawa nzuri zikaanza kung'aa, watanzania tunavyopenda vya bure na kudandia vilivyokwisha undwa tukaanza kung'ang'ania kupeleka watoto wetu katika shule hizo - mifano ipo katika shule za msingi zilizopo upanga na posta jijini dar es salaam. Kutokana na ufinyu wa nafasi watu wanafikia mahali wanatengeneza mazingira ya rushwa kwa kulazimisha kuhonga ili watoto wao wasome shule hizo!

  Wengi wetu tumesahau kuwa shule zote za serikali zilizowahi kuwika zilijengwa na kutunzwa na watu walioamua kujitolea - wageni, mashirika ya dini, makanisa, mashirika etc etc. Kuna tatizo gani sisi leo kuwekeza katika shule hizi zinazotuzunguka? Shule nyingi za sekondari zilizowahi kuwika leo zimebaki magofu, mfano mzuri Bagamoyo, Umbwe, Lyamungo, Moshi Technical, Old Moshi, Iyunga, Milambo, Tabora (Boys na Girls) n.k n.k n.k. Maabara zimekufa katika shule hizi, maktaba zimekufa, madarasa yamezeeka, mabweni nayo yanasikitisha. Cha ajabu tuna watu, tena wengi tu katika nchi hii wapo katika nafasi nzuri tu mahali mahali, walisoma katika shule hizi, wanaongoza kwa kupeleka watoto katika shule ambazo chekechea tu ada ni milioni. Hawajawahi hata kuthubutu kuchangia Tshs 500,000 kwa shule zilizochangia kuwafanya wawe pale walipo leo! What a shame! Are we cursed? Japo vitabu vya Tshs 200,000 hawajawahi kufikiri kupeleka!

  Cha ajabu sasa, watoto hawa hawa wakimaliza kidato cha sita wanarudi katika vyuo vya umma! Hapo ndipo unakuja kuona maajabu! Wanarudi katika mfumo ule ule walio-ukimbia miaka kadhaa iliyopita. Kituko zaidi, wanalilia mikopo kisa eti hawawezi tena kumudu ada ya chuo kikuu ambayo - kwa haraka haraka hakuna inayozidi Tshs. 3,500,000 kwa mwaka. Sasa wewe mtanzania, hebu fikiri, ungekuwa raia wa Uingereza halafu unaelezewa tabia hizi za 'mtanzania' ungemfikiriaje huyu 'mtanzania'? Bila shaka ungeweza kudhani ni 'kiumbe' mmoja wa ajabu sana, ama pengine sio binadamu huyu!

  Baada ya miaka kumi, watoto wetu tutawakabidhi aina gani za shule za umma? Sisi tulikabidhiwa zikiwa na hali nzuri, sisi tunazikabidhi vipi? Mitaala ya elimu ni ile ile tangu kipindi hicho hadi leo, kweli Tanzania itawendelea?

  Halafu, watanzania tunaonaje aibu kuhoji kwa nguvu zote kuwa na viongozi wa umma ambao wengi wao watoto wao hawasomi katika shule hizi? Una waziri wa Elimu ambaye mwanae hasomi katika shule ya umma? Hii inakuaje?

  Tunaandaa jamii ya aina gani ya miaka ya usoni ya nchi yetu?
   
Loading...