Udukuzi juu ya udukuzi: Mwendelezo wa vita baridi kati ya Marekani na Urusi

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
11,852
22,008
Mwaka 2016 ndio tunauacha Rasmi, mwaka 2016 una mengi ya kukumbukwa yaliyoifurahisha na kuihuzunisha dunia. Mambo ambayo yatabaki kichwani mwa watu ni Vita vya mahasimu wanaooneshana ubabe nchini Syria ambavyo vimesababisha vifo vya watu wengi huku mataifa makubwa yakiendelea kuoneshana umwamba wa nani zaidi katika masuala ya teknolojia ya silaha za kisasa huku raia wasio na hatia wakiendelea kupoteza maisha.

Suala la pili litakalokumbukwa na Dunia ni Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya, suala la tatu litakalokumbukwa ni Donald Trump kushinda kiti cha Urais wa Marekani kinyume na matarajio ya wengi, suala la nne la kukumbukwa ni suala la kuuawa kwa Balozi wa Urusi nchini Uturuki na Mwisho ni Uamuzi wa Rais Obama kuwafukuza maafisa 35 wa Ubalozi wa Urusi nchini Marekani kwa kuwatuhumu kwamba walidukua Uchaguzi mkuu wa Taifa hilo na kumuwezesha Trump Kushinda urais wa Marekani.

Hayo yaliyotajwa ni baadhi ya Matukio yaliyotikisa siasa za Dunia japo nimetaja machache kati ya mengi yalliyotokea:

Makala yangu itajikita kuelezea uhasama uliopo kati ya Marekani na Urusi, Uhasama ambao huwa hauishi bali hutulia kwa Mda. Uhasama huu ulianza mapema baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia mwaka 1955s. uhasama huu ulipewa jina la Vita Baridi (COLD WAR) uhasama huu ulijikita katika utawala wa kisiasa, utawala wa Maeneo Maalumu kiusalama, Utawala wa kimtazamo au itikadi (capitalism versus Socialism) na Mwisho ni Uhasama kiusalama.

Vita baridi ilianza Rasmi mwaka 1960s na ilikuja kuhitimishwa rasmi Mwaka 1990s baada ya umoja wa kisosholist wa kisoviet kusambaratika chini ya Utawala wa Michail Gorbachoev ambaye alisaini mkataba wa kuwaruhusu NATO kuendelea kujitanua mashariki mwa Ulaya na Asia na kuua Umoja wa Jeshi la kujihami la mashariki mwa Ulaya (WARSAW PACT) na kufa kabisa kipindi cha Boris Yeltisin ambapo licha ya Boris Yeltisin kuhitimisha kifo cha umoja wa kisosholist wa kisoviest atakumbukwa kwa kumleta Mbabe wa siasa za kisasa na rais wa sasa wa Urusi bwana Vladimir Putin.

Uhasama wa mataifa haya Mawili Ulihitimishwa mwaka 1990s kwa upande wa kushindana kiitikadi na Mitazamo ya Kisiasa ambapo Marekani na wafuasi wake walishinda vita baridi hiyo na kuufanya Ubepari kuwa ndio mfumo uliotawala uchumi na siasa za Dunia na kuufanya usosholist au Ujamaa kufika tamati japo kuna baadhi ya Nchi hadi leo zina chembe chembe ya Ujamaa Mfano China, Vietnam, Urusi, Bolivia, Venezuela, Cuba na Ufilipino.

Uhasama wa mataifa haya ulihama kutoka katika utawala wa maeneo maalumu kiitikadi, kimtazamo, kisiasa na kiuchumi na kujikita katika uhasama wa Teknolojia katika masuala ya Silaha na Kiuchumi.

Uhasama huu uliohamia katika Teknolojia ya Silaha ulienda sambamba na uhasama wa Umiliki wa Maeneo nyeti kiusalama mfano licha ya kusambaratika kwa USSR lakini maeneo ya kimbinu na kiusalama ya Urusi yalihusisha pia kuzikalia nchi nyingine kama Georgia, Kazakhstan, Latvia, Lithuania,Crimea, Ukraine, Slovakia, Serbia na maeneo mengine mengi yanayopatikana Mashariki mwa Ulaya na Asia. Na Marekani iliendelea kuwa na maeneo ya Kimbinu kwa Washirika wake kama vile Ufaransa na Uingereza na baadhi ya nchi huko latin Amerika.

Uhasama wa Kimbinu na kiusalama ulitawaliwa zaidi na oparesheni na oganaizesheini ya kijasusi, katika nchi zilizoendelea sehemu za Ubalozi hutumika kama kificho cha majasusi ambao hufanya kazi zao kwa kujificha katika balozi.

Uhasama huu ni kati ya shirika la ujasusi la Mambo ya nje ya nchi la Marekani (CIA) na lile shilika la Ujasusi la mambo ya nje la Urusi (FSB). Haya ni mashirika ya ujasusi ambayo huwekwa maeneo yote ya kimbinu ili kujiimalisha kiusalama dhidi ya Adui lakini pia hufanya kazi za udukuzi ili kuibiana siri mbali mbali zinazohusiana na Masuala ya Kiuchumi, Technolojia, siri za kiusalama na siri za kijasusi.

Alhamisi ya Tarehe 29 mwezi wa 12 mwaka 2016 Marekani ilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 35 na kufunga vituo vya kijasusi
Itaendelea...
 
vya Urusi mjini Washington ambapo vilikuepo kwa makubaliano ya Kidiplomasia. Idadi hii ya wanadiplomasia 35 kufukuzwa ni kubwa zaidi tokea mwaka 2001 ambapo wanadiplomasia zaidi ya 50 walifukuzwa baada ya Urusi kumkamata bwana Robert Philip Hanssen ajent wa FBI aliyekamatwa akidukua nchini Urusi ambapo marekani iliwafukuza wanadiplomasia hawa ili kushinikiza kuachiwa kwa Bwana Robert Philip Hansen aliyekamatwa akifanya kazi za kijasusi jijini Moscow, Wanadiplomasia hawa 35 wamefukuzwa kwa madai ya kwamba walihusika kudukua uchaguzi wa Taifa hilo na Kumwezesha Rais Mteule wa Marekani kushinda uchaguzi bwana Donald Trump.

Hatua hii ilizusha mgogoro wa kijasusi baina ya Marekani na Urusi na endapo Urusi ikijibu mapigo inaweza kuvifunga vituo vyote vya shilika la ujasusi la marekani (CIA) Katika maeneo yote ya kimbinu kama vile Georgia, Kazakhstan, Lithuania, Latvia, Crimea, Ukraine, Slovakia, Slovenia, Bulgaria na maeneo mengine mengi yanayopatikana mashariki mwa Ulaya na Asia.

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema wazi hawezi kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani mpaka pale Rais Mteule atakapoapishwa tarehe 20 january 2017 na kuona kama ataidhisha vikwazo basi nao watajibu ikumbukwe itakuwa ni wiki tatu tu toka sasa rais mteule wa Marekani atakapoapishwa, Trump ameomba kukutana na maafisa usalama wa Juu wa Marekani wiki ijayo ili kujadiliana nao baadhi ya mambo ya kiusalama yanayoihusu nchi hiyo sasa sijui kama na suala la Kufukuzwa kwa wanadiplomasia wa Urusi nchini humo litagusiwa.

Uhasama huu wa kidiplomasia haujaanza leo, kumekuwa na mtiririko wa matukio mbalimbali yanayozihusu nchi hizi katika kufukuziana wanadiplomasia. Ifuatayo ni mikasa ambayo ilipelekea mataifa haya kuwekeana vikwazo vya kidiplomasia.

Mwaka 2013 Marekani iliwafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi katika kujibu mapigo baada ya Askari polisi wa Urusi kumvamia na kumkamata mwanadiplomasia wa Marekani nje ya ubalozi wa Mrekani jijini Moscow.

Polisi wa Moscow walisema walimkamata mwanadiplomasia huyo baada ya kukataa kuonyesha kitambulisho wakati anaingia katika Ubalozi wa Marekani jijini Moscow hivyo polisi walihisi ni jasusi wa CIA, Marekani iliiomba Urusi kumwachia Mwanadiplomasia huyo kwa kuthibitsha ya Kwamba ni MMoja wa staff wa Ubalozini lakini Urusi iliendelea kumshikiria Mwanadiplomasia huyo hivyo Marekani ikajibu mapigo kwa kuwafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi nchini Marekani.

Mwaka 2010 raia 10 wa Urusi walishtakiwa kwa kufanya kazi kama maajenti wa siri wa Urusi nchini Marekani (sleeper Agent), maajenti hawa walirudishwa nchini Urusi baada ya Kukiri katika mahakama ya shirikisho katika jiji la Manhattan, maajenti 10 wa Urusi waliachiwa katika makubaliano ya kuwaachia wafungwa 4 wa kimarekani waliokuwa wamefungwa nchini Urusi ambapo watatu kati yao walikuwa na makosa ya Uhaini.

Mwaka 2001 Marekani iliwafukuza wanadiplomasia 50 wa Urusi nchini Marekani Baada ya Urusi kumshikilia Jasusi wa shilika la FBI ambaye alikuwa akifanya kazi za kijasusi nchini Urusi katika jiji la Moscow ambapo alifanya kazi za kijasusi zaidi ya miaka 15, mwaka 2001 alikamatwa na Urusi baada ya Kumhisi kwamba ni jasusi, walipompa mateso makali alikubali kuwa yeye ni Jasusi wa Marekani hivyo basi Urusi ikamuahidi kumuachia endapo angetoa Ushirikiano, Jasusi huyo aliyejulikana kwa jina la Robert Philip Hansen alikubali kuisaliti marekani na kuipa Urusi siri za Marekani. Marekani iliiomba Urusi kumrudisha nchini Marekani bwana Hansen lakini Urusi ilikataa kumsalimisha katika kujibu mapigo Marekani iliwafukuza wanadiplomasia zaidi ya 50 wa Urusi nchini humo.

Mwaka 1994 baada ya kukamatwa kwa jasusi wa CIA bwana Aldrich H. Ames ambaye alikuwa double agent aliyeyafanyia kazi mataifa yote mawili yaani Marekani na Urusi. Marekani iliamua kumfukuza mwanadiplomasia wa Urusi aliyejulikana kwa jina la Aleksandr Lyskenko kwa madai kwamba bwana Ames alikuwa akimkabidhi bwana Lyskenko siri mbalimbali za Marekani na kuzipeleka nchini Urusi.
Itaendelea
 
Hivi hii dhana iliyo jengeka ya kudai eti Marekani ilishinda vita baridi - madai haya yana ukweli gani zaidi ya propaganda za MSM.

Ukweli ni kwamba Reagan ambaye alikuwa Rais wa Merikani kwa wakati huo ndiye alinyanyua simu na kumpigia Gobarchev kwamba nchi zao zisitishe uhasama baina yao kwa njia ya mazungumzo, na hicho ndicho kilicho jili, watu wanakwepa kusema ukweli huo badala yake masaa yote wanazuga walimwengu kwa adithi za kufikirika za Alinacha!!

Tukija Urusi yenyewe ni Gorbachev ndiye aliamua nchi zilizo kuwa zinahunda shirikisho la USSR zisitishe kuwa nchi moja, kila nchi ijetegemee wabaki kuwa kama a loose assosiation - ukweli ndio huo lakini watu wanakuja humu na skewed story kupotosha wasomaji.

Gorbachev alifikia uhamuzi wa kufanya marekebisho katika nchi zilizo kuwa zinahuda USSR baada ya kuona nchi hizo zilikuwa zinaitegemea sana Russian Federation bila ya wao kujishughulisha sana, hilo ndilo lilikuwa ni lengo la Gorbachev i.e kupunguza utegemezi wa nchi hizo.

Kuhusu Warsaw Pact, lengo la kuanzisha shirikisho hilo la kijeshi lilikuwa ni ku counter NATO, kumbuka NATO ilianzishwa 1949 kama sikosei wakati Warsaw Pact ilianzishwa 1956 i.e miaka saba baadae, sasa kama NATO na Warsaw Pact walikubaliana kuachana na vita baridi kulikuwa na haja gani kuendelea na ushirika wa kijeshi wa nchi zilizo hunda NATO na ushirika wa nchi za Warsaw Pact - uhuni tu wa Merikani na ajenda zake za siri ndiyo ulikuja kukihuka makubaliano, badala ya kudis-band NATO wakaimarisha na kujitanua kuelekea East wakiwa na lengo ka kuizingira Urusi - kinyume kabisa ya makubaliano ya Reagan na Gorbachev - akili za Viongozi wengi katika Serikali ya Marekani zimejaa ndoto za kuisambaratisha Urusi - kiwe kiangazi au masika, wako obsessed na Urusi kama nini sijui? Marekani ikiendekeza ujinga wake huo na kujaribu kuishambulia Urusi kwa kuishtukiza watapewa fundisho la mwaka.
 
Hensen huyo double agent
Kama sikosei alikamatwa na wamarekani wenyewe baada ya kugundulika anaspy CIA na taarifa anazipeleka kwa KGB....yaani ulichoandika kifanye vice versa
 
Hensen huyo double agent
Kama sikosei alikamatwa na wamarekani wenyewe baada ya kugundulika anaspy CIA na taarifa anazipeleka kwa KGB....yaani ulichoandika kifanye vice versa
Mbona na wewe ni kama huna uhakika?
 
Hensen huyo double agent
Kama sikosei alikamatwa na wamarekani wenyewe baada ya kugundulika anaspy CIA na taarifa anazipeleka kwa KGB....yaani ulichoandika kifanye vice versa

Cha kujiuliza nani alimkamata jasusi wa mwenzake kwanza? Hapo ndio utapata picha kamili.
 
Sehemu ya 3
Inaendelea:
Hivyo basi anatakiwa kurudi Urusi lakini baadaye baada ya kuingia uongozi wa Bill Clinton bwana Lyskenko alisamehewa kwa makubaliano mataifa hayo mawili kuendeleza urafiki wa kidiplomasia.

Mwaka 1986 Rais wa Marekani Ronald Reagan aliwafukuza wanadiplomasia 55 wa Urusi baada ya kuwahisi Warusi wanaiba siri za Marekani, vivyo hivyo Urusi ikawazuia wafanyakazi wa muungano wa Kisoviet sosholist republic zaidi ya 260 waliokuwa wanafanya kazi katika ubalozi wa marekani kuacha kufanya kazi mara moja. Hii ndio idadi kubwa zaidi ya Wanadiplomasia wa Urusi kuwahi kufukuzwa nchini Marekani.
Mgogoro ulianza baada ya Gennadi F. Zakharov aliyekuwa mfanyakazi wa kisoviet katika makao makuu ya Umoja wa mataifa (United Nation) kukamatwa kwa madai ya Udukuzi wa Siri muhimu za Jeshi la Marekani. Urusi walijibu mapigo kwa kumkamata Nicholas S. Daniloff ambaye walimtuhumu juu ya ukusanyaji wa taarifa muhimu za Urusi na kuzituma nchini marekani. Kwa historia hii inaonyesha wazi ya Kwamba vita baridi katika mataifa haya inaendelea na haijawahi kusimama.

Uhasimu wa mataifa haya utamalizika pale ambapo taifa moja litakubali kuwa Mfuasi wa Taifa lingine au kama ikitokea Vita ya tatu ya Dunia na Taifa moja likapoteza nguvu kiuchumi, kiteknolojia na kisiasa kwa kupigwa katika vita hiyo.
Urusi na Marekani ndio mataifa yenye ushindani mkubwa katika teknolojia ya silaha na shughuli za kijasusi.
Mwisho,
Asanteni na shukrani
 
Back
Top Bottom