UDSM wamenifungia matokeo yangu sababu nina deni la ada.

Apparent

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
220
110
Najua wenye mamlaka au wanaohusika na Utawala wa UDSM mnapita mitaa hii.

Je mwisho wake ni nini?
Hadi muda huu naandika sijui kama nina sup na sijui nini kinaendelea kwenye akaunti yangu ya ARIS.
Kisa nadaiwa 500,000TZS.

Je hamtambui kuwa duniani kuna masikini kama mimi?.
Nashauri mngenibana wakati wa kuchukua cheti ila sasahivi siwezi kupata pesa ninayodaiwa.

Vyuma vimekaza naomba muwe na utu,wengi nikiwaambia hili tatizo hawaamini kama kweli nadaiwa na wanachukilia kirahisi na wengine wanaomba taarifa zangu wakiona ni kweli wana lala mbele au wanaingia mitini.

UDSM naomba nisaidiwe ili niweze kuona matokeo yangu,kuna dalili mwaka wa tatu nitaendelea kuusikia kwenye vyombo vya habari na watu waliofanikiwa kuhitimu.
 
Sijaona kosa la Udsm hapo. WEWE ANDIKA UZI KUOMBA MSAADA WA KUCHANGIWA PESA na sio blah blah .
 
Hiki kitu hakuna....hauwezi fanya mtihani bila kulipa ada lamili....ID ya kufanyia mtihani uliipataje?

Utaratibu wa UDSM ni kwamba lipa direct cost na ada, upewe id ndio utakua unaruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na chuo
 
Mkuu anzisha uzi utoe details kamili hata kwa PM watu wakusaidie
Hiyo laki 5 kwa humu JF watu wakichang buku 1 moja na ndugu zako wakichanga utalipa deni lote
Huo uzi nimewahi kuanzisha ila niliishia kutoa taarifa zangu lakini sikusaidiwa.
 
Hiki kitu hakuna....hauwezi fanya mtihani bila kulipa ada lamili....ID ya kufanyia mtihani uliipataje?

Utaratibu wa UDSM ni kwamba lipa direct cost na ada, upewe id ndio utakua unaruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na chuo
Kwa wote wenye matatizo ya kiuchumi wanajua inakuwaje,ni ngumu kwa tajiri kama wewe kujua kuwa kuna kitu kinaitwa Conditional Registration.
 
Hiki kitu hakuna....hauwezi fanya mtihani bila kulipa ada lamili....ID ya kufanyia mtihani uliipataje?

Utaratibu wa UDSM ni kwamba lipa direct cost na ada, upewe id ndio utakua unaruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na chuo
Una uhakika mimi nina uhakika mtu anapewa kitambulisho na kufanya UE kwa usajili wa muda,mimi ni mmoja kati ya waliosaidiwa.
 
Back
Top Bottom