UDSM walisema "hii serikali ya kisanii" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM walisema "hii serikali ya kisanii"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MyTanzania, Sep 30, 2008.

 1. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #1
  Sep 30, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa watU wote wanaoitakia mema nchi yetu tuipendayo,TANZANIA.
  Nakumbuka ilikuwa mwaka 2005 mgombea urais kupitia CCM,Bw. Jakaya Kikwete alipokuwa akipita kila mahali nchini kuhubiri sera zake kwa mtindo wa kutoa ahadi nyingi ambazo mpaka sasa utekelezaji wake umekuwa kitendawili.Bwana huyu aliwapa Watanzania waliochoka kuelea katika dimbwi la umaskini tumaini jipya kwa vibwagizo vyake vya kampeni vilivyobuniwa na mtaalam mmoja wa mambo ya siasa pale mlimani ambaye ni rafiki yake.
  Watanzania tuliambiwa "Ari mpya,Nguvu Mpya na Kasi MPya, Maisha bora kwa kila mtanzania,Tanzania yenye neema inawezekana".Maneno haya yamegeuka fimbo kwao maana watanzania wamegundua kuwa ilikuwa sanaa tu.
  Dalili zilianza kuonekana mapema baada ya Rais na Waziri wake mkuu kuanza kutofautiana nje nje kwenye vyombo vya habari.Rais akisema hivi,waziri mkuu anasema hivi.Mambo yalizidi kwenda mrama zaidi mwaka 2007 baada ya serikali kuanza kuinadi bajeti yake nchi nzima huku mawaziri wakizomewa.Kipindi hiki ndipo mambo mengi yalianza kufunuliwa kama BUZWAGI,EPA,RICHMOND and the like.
  Tunakumbuka list of shame ilivyotolewa na Bwana Slaa, mwanasheria wa Chadema Bwana Tundu Lissu na wengineo waliotajwa wengi walianza kuhamaki kwa kutishia kuwapeleka mahakamani lakini hadi leo hakuna hata mmoja aliyediriki kufanya hivyo.Walidhani bado tupo kipindi cha ukiritimba wa habari na kutishana na wakasahau kusoma alama za nyakati.
  Tunakumbuka kuwa kulitokea mgomo pale MLIMANI ambapo wanafunzi waliandika katika mabango yao kuwa "HII SERIKALI YA KISANII".Nadhani vijana wale waliona mbali sana.Waligundua sanaa ambayo watawala wa nchi hii wanaifanya.
  Waligundua sanaa ya RICHMOND na LOWASSA
  Waligundua sanaa ya EPA na CCM
  Waligundua sanaa ya TISCAN na KARAMAGI
  Waligundua sanaa ya RADAR na CHENGE
  Waligundua sanaa ya BUZWAGI na KARAMAGI
  Waligundua sanaa YA MUUNGWANA NA MAWAZIRI WAKE.
  Waligundua sanaa ya KAGODA na ROSTAM AZIZ
  Waligundua sanaa ya mabenki ya kitanzania yasiyowajibika kwa umma kwa kukubali pesa ya EPA ipitishiwe kwao.Nikitolea mfano CRDB Bank ni Public Limited Company,lakini ilikubali pesa za EPA zipitishwe katika bank yake bila kuhoji.Maana kama wangefuata vizuri provision za MONEY LAUNDERING ACT,wasingekubali kupokea pesa zile kwani zilikuwa na kila dalili za uchafu.
  Mwisho napenda kuwatia moyo wote mlio katika vita dhidi ya ufisadi,najua itafanikiwa japo mafisadi wamejijengea ngome.Tutaifanikisha kwakuwa MUNGU anapinga ufisadi na watawala wetu hawawezi kushindana na sauti ya MUNGU ambayo ni umma wa Watanzania.
  ALUTA CONTINUA
   
 2. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakupa tano kwanza.Hii ngoja nidownload kwenye hardcopy nigawe huku vijijini kyela.Nitaisoma kwa makini niwatafasirie kwa kilugha hawa akina mama ambao hawajui kusoma na kuandika.Takwimu za literacy zinaonyesha wenye umri wa kuzidi miaka 35 ni 70%.Nawatumia walimu wa primary na zile sekondari za kata.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Sep 30, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Umenishtua kidogo maana UDSM kubwa sana!

  Yes wanafunzi walisema hayo, lakini wengi wa waalimu wao(lecturers ndio waliompigia pande kikwete chini ya REDET!!, ndio waliompa huo usemi nguvu mpya , ari mpya, kasi mpya! japo waliiga toka nchi fulani.Na wakamwambia amalizie kusema maisha bora kwa kila mtanzania!

  So sio UDSM wote, damu changa waliisha ona mapema bomu lililopo kwenye serikali hii, wengi wa wazee walimpigia debe Kikwete.

  So title should read ''wanafunzi wa UDSM waliona mbali''

  we are now because of these so called wasomi!

  waberoya
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  [
  [/QUOTE]

  Yes Waberoya we are here because of these so called wasomi. I support you!???!!@#$!!
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mimi nakumbuka kipindi cha mchakato kumteua nilikuwa pale Morogoro kulikuwa na jamaa angu mmoja anaitwa Simbeye na wengine wengi walikuwa wanasoma Chuo cha Ualimu pale Morogoro walimshabikia sana nakumpenda Mkuu huyu Mungwana kwa kila namna mimi nikawa nawauliza nini cha maana mnacho mshabikia JK wakawa hawana jibu zaidi nikagundua kuwa walikuwa wanampenda anavyo tabasamu........
  Basi jamaa wakatoka pale Ualimu wapo kazini leo hii jamaa analia na kusaga meno maisha magumu analalamika sana mishahara ndo hivyo tena mazingira magumu ya kazi ....mimi nikamkumbusha unakumbuka sera ya chama?Maisha bora kwa kila MTZ ndo hayo sasa....umemchagua mwenyewe na ulisema anafaa kuwa kiongozi sasa anakupa adabu kesho ujifunze kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi kwa vile sura nzuri anatabasamu safi ukajua ndo kiongozi hapo ni wrong.....
  Ni kweli kabisa huyu JK watu wachache tulimbeza sana lakini ndo hivyo wananchi walimpenda kwa tabasamu lake safi wakamchagua kwa zaidi ya 70% leo hii wanajuta mitaani life limekuwa tough sana....
  Tuliambiwa jamaa atatengeneza ajira zaidi ya milioni 1 na maisha bora kwa kila Mtanzania leo hii wamekuja na style ingine eti maisha bora hayapatikani kwa kukaa vijiweni tufanye kazi kwa bidii......sasa mbona wakati wanakuja kuomba kura zetu hawakutuambia hivyo??wamesha pata sasa na wapo kwenye system wanakuja na gia ingine tena......
  Naona kuna haja ya kuteua mgembea mwingine kwa uchaguzi wa 2010 huyu jamaa hana cha kujivunia miundo mbinu toka amwachie Mkapa yeye mpaka leo hata barabara moja haijakamilika ambayo anaweza akajisifia kuwa amejenga barabara hiyo hapo Sam Mjoma mpaka leo hii sijui kama ipo kwenye kiwango hata 5km haifiki...huyu ndo waTZ waliomchagua kwa kuangalia sura sasa wao wenyewe ndo wanao umia wao aaaah wanatanua tu na miVX,hummer,Vogue n.k walalahoi wanapiga miayo tu.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Sep 30, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa:

  Nadhani kuchagua kiongozi yeyote, lazima tujue alifanya nini siku za nyuma apelekee leo hii tumchague?. kama wasomi ni vipofu namna hii? vipi kuhusu babu yangu huko tukuyu?


  waberoya
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ametumia miaka kumi akijiandaa kuwa rais, mlitarajia nini? Alichokuwa anakitaka yeye ni urais, si kuendeleza nchi
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The country is in one of the wrost economic crisis ever and something ought to be done.JK has failed the millions of Tanzaniana and please for God's sake wanafunzi wengi wa UDSM wametokea kona mbalimbali za TZ wana uwezo wa ku mobilize watu wawe poitically concious ili tuache kuwa vibaraka wa CCM.
  CCM needs to make history by doing what ANC has just done to Mbeki and by doing so it will show just how plotocally mature they are!
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  mradudia rudia mambo mno... sasa jipya hapo ni lipi?
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  [QUOTE mradudia rudia mambo mno... sasa jipya hapo ni lipi?[/QUOTE]

  wewe ulitaka jipya gani? hatuwezi kunyamazia ufisadi mpaka umma utakaposhinda.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mara nyingine kuirudia rudia point ndiko kunai drive home.

  Ulishasikia speech ya MLK "I have a Dream"? Ulishamsikia mara ngapi anasema "I have a Dream"?

  Ushasoma Agano la Kale? Ushaona repetitions zilivyojinyonga? Tazama story ya Ayubu kwa mfano.

  Ushasoma mashairi ya Andanenga? Ushaona mstari wa mwisho unavyojirudia?

  Ushasoma "Histories" ya Herodotus? Umeona repetition?

  Ushasoma "Mein Kampf" Umeona repetition iliyopo? What about Virgil, Juvenal and Homer? Chaucer's Canterbury Tales?

  Tatizo lisiwe kwamba watu wanarudia, je unaweza kubishia kile wanachorudia?
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tuna rudia rudia hilo mpaka likae vizuri vichwani mwetu ili 2010 hakuna wa kuja na kutudanganya tena. Unasikia kasheshe?
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #13
  Sep 30, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  hakuna jipya hadi hapo huyo muuza sura wenu atakapotuachia ikulu yetu ...tumuweke mtanzania mwenye akili na rekodi iliyotukuka ya utumishi kwa umma..

  hushangai siku hizi ile kauli mbiu .."kwa ari mpya ,nguvu mpya na kasi mpya"....na
  "maisha bora kwa kila mtanzania ,yanawezekana"..."tanzania yenye neema inawezekana"...zimegeuka TUSI KUTAMKWA ,MAHALI POPOTE MBELE YA RAIS....................HAZITUMII TENA,WALA WASAIDIZI WAKE KWENYE MIKUTANO YA HADHARA ANAYOKUWEPO HAWAZITUMII.....

  jakaya mrisho kikwete is literally..JANGALA MICHOSHO KIWETE!!!
   
 14. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2008
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  PM.
  Wewe si wakawaida
   
 15. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2008
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 543
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Pia sio wanaUDSM wote walisema: kama walikuwepo ni asilimia kidogo.

  wakati wa mchakato wa kumtafuta candidate katika CCM, Kikwete alijitabulishia kabla ya muda kichama kutolewa. na hilo lilifanyika nje ya Nkuruma Hall pale UDSM. nilikuwa pale nikisomaa na siku hiyo ninavyokumbuka, alikuwepo muhadhara uliohudhuliwa na Kagame na viongozi wengine toka ubalozi wa Cuba Zimbabwe, U.s Pakistani, Palestina n.k: uungwana alihudhuria kama Waziri wa Mambo ya Nje.

  Baada ya kujitangaza, wanachuo walianza kushangilia na kusukuma gari lake wakisema Rais, Rais, Rais.

  kama mnakumbuka hii sokomoko ilitaka kuleta zengwe.

  2. pia nakumbuka kipindi hicho nikiwa bado nasoma, wanachuo wengi wapatao 5000 toka UDSM walijazana Diamond Jubilee na wengine wakabaki nje kwa kukosa nafasi. wote walishangilia kuwa kwa mara ya kwanza PRODUCT YA UDMS ITATOA MBEGU YA RAIS BAADA YA KUKOSA VIONGOZI WAZALENDO. katika mkutano huo wa chama, malecturers wengi walikuwepo akiwepo hata Marehemu CHACHAGe, jambo linaloashiria kuwa walikuwa na matarajio mengi sana kwake.

  3. manaposema kuwa UDSM walijua ninasita kusema ni wote, mimi binafsi nilijua ila wenzangu tena majirani zangu walikubali hata ofa za T-shirt, ilikuwa inasikitisha. sasa kama hakuna maandamano yoyote ambayo yamehsisha idadi ya watu angalau 5000, ya kupinga hii serikali, then tunadhani bado hizo mbegu zinaishi.

  4. ni heri tukemee ili isijirudie kuliko kupamba ili tuonekane wema machoni pa jamii.
   
 16. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  In most cases watu wanaorudia rudia mambo wako shallow in thinking... guys with creativity hawarudii mambo obvious...

  Eid Mubaraka
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Well, naona upuuzi... lakini hakuna la kujifunza!!! expectation yangu nikiingia JF nisome mambo nilishayasoma...
   
 18. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakupa tano mkuu.Ila pamoja na udhaifu wake ameacha kumbukumbu nzuri kuhusu UDOM.Ni hilo tu kwa upande wangu naona ndilo la busara na nampa ushauri wa bure kipindi kimoja kinamtosha asiharibu zaidi.Wananchi wanaweza kumsamehe lakini aking'ang'ania kugombea tena kama alivyofanya Amani Karume atafuta hata hicho kifutia machozi.
  Karume anataka akumbukwe kwa kuvuruga muungano maana,anaona ndio karata yake ya mwisho ya kusimama kidete kutetea utaifa wa Zanzibar.
   
 19. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45

  Na ni hao hao walimu wa chuo cha Morogoro-kigurunyembe aka MOTCO waliomchagua JJ kuwa rais wao.Inamaana hicho chuo ingekuwa nchi walikuwa wamemchagua KIPOFU mwingine.Mimi naona shida siyo rais bali ni wapiga kura.Kwa level hii wewe unamchagua JJ kuwa rais halafu unamshaabikia muuza sura kuwa Rais kisha uanalalamika maisha kuwa magumu.Ulitarajia nini kipya???????
   
 20. o

  oldisgold Senior Member

  #20
  Mar 18, 2014
  Joined: Oct 2, 2013
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UDSM ni wazugani kila mtu analijua hilo
   
Loading...