UDSM wakaribia kuwa RAIA wa Tanzania

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mchakato wa kugawa vitambulisho vya Uraia wa Tanzania umeshika kasi ambapo zoezi la kuchukua alama za vidole kieletroniki limefanyika jana UDSM. Hiyo ni hatua ya mwisho kuelekea kugawiwa kwa vitambulisho hivyo kwa 'raia' rasmi wa Tanzania. Zoezi hilo liliwahusisha wafanyakazi wa UDSM ambao walishajaza fomu za kuomba vitambulisho hivyo miezi michache iliyopita.

Kwani,ambao hatapata vitambulisho hivi hatakuwa raia wa Tanzania? Just curious
 
Na wanafunzi je wamepata? isije ikatokea kuwa ni tekniki ya wakubwa huko mbeleni bila kitambulisho hupigi kura, na wanafunzi hawajapata vitambulisho bado
 
Sisi wa Mtwara na Lindi hatuchukui vitambulisho maana tunatarajia kuanzisha Jamhuri ya Watu wa Kusini mwa Tanzania.

Tuko kwenye mazungumzo na watu wa mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Katavi ili nao wajiunge na jamhuri yetu!!

So vitambulisho vyenu gawaneni hukohuko
 
Mbeya na Katavi ujinga huo hawana.
 
Back
Top Bottom