UDSM: Ukweli Ni Huu

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
UKWELI KUHUSU YA MATUKIO YA VURUGU YA 17 NA 22 FEBRUARI NA 11 APRILI 2008 KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

UTANGULIZI:

Tarehe 15 Aprili 2008 Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilitoa taarifa kwa umma juu ya kusimamishwa masomo kwa wanafunzi mbalimbali. Jumla ya wanafunzi 16 wamesimamishwa kwa makosa ya kufanya na kuwa vinara wa vurugu za tarehe 17 na 22 – februari 2008. jumla ya wanafunzi 4 wamesimamishwa kwa kosa la kufanya vurugu tarehe 11 Aprili 2008.

Tukio la 17 na 22, februari 2008.

Mnamo tarehe 17 na 22 – februari – 2008 kulitokea vurugu zilizofanywa na wanafunzi wa Chuo hicho katika Hosteli za Mabibo (17 februari 2008) na Hosteli za Kampasi kuu (22 februari 2008).

A: CHIMBUKO LA VURUGU ZA 17 FEBRUARI 2008, HOSTEL ZA MABIBO.

Kwa muda mrefu wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamekuwa wanakabiliwa na matatizo mengi sana kama vile ukosefu wa maji, kukatika kwa umeme kwa muda mrefu, ubovu wa lifti, upungufu wa Hosteli, vyumba vichache vya madarasa, vyoo vibofu hasa vya kukalia, vyumba kuvuja maji, n.k.

Licha ya ubovu huo wanafunzi wa Chui hiki wamekuwa wavumilivu kwa miaka mingi sana. Kuzoea shida na maisha waliyotoka wanaona kuwa ni sehemu ya maisha ya Mtanzania. Wale wachache wanaosimamia kidete na kusema bila woga hupata misukosuko kutoka katika Utawala wa Rwekaza Mkandala.

Tarehe 17 Februari 20008 maji yalikuwa yamekatika katika Hosteli za Mabibo kwa siku nzima. Licha ya viongozi wa Daruso kuwasilisha matatizo hayo kwa USAB Manager na Mawarden ufumbuzi haukupatikana. Hata gari la maji lilileta maji kidogo na kuyamimina katika matenki ya wanafunzi kuchotea maji. Lakini ilikuja kujulikana kuwa kulikuwa na maji ya Dawasco yalikuwa yamejaa hadi juu katika tenki kubwa la kuhifadhia maji katika Hosteli hizo na kuyasambaza katika vyoo, bafu na matenki ya wanafunzi kuchotea maji. Lakini mafundi na mawardeni walisema kuwa pampu na bomba la kusukuma maji katika matenki ya wanafunzi kuchotea ilikuwa imeharibika.

Baadaye tulijiuliza kwa nini magari ya maji yasichukue maji katika hicho kisima na kuyamimina katika matenki ya wanafunzi kuchotea maji badala ya kuyatoa umbali mrefu?

Tuligundua kuwa kumbe mwenye kampuni hiyo ya kuleta maji katika Hosteli hizo wakati wa dharura alikuwa amekula dili na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo ili kuweza kutengeneza “udharura” ili alete maji na hivyo kujipatia fedha kwa kuwaumiza wanafunzi. Pia tuligundua kuwa alikuwa akiingia na maji kisha anamimina kidogo kisha anaondoka na kugeuza na kuja kuyaminina tena, hivyo katika msafara mmoja alikuwa anatengeneza misafara miwili. Ufisadi huu wa wazi kabisa uliwakera wanafunzi wakazi wa Hosteli hiyo ya Mabibo.

Majira ya usiku ya tarehe 17 feburari 2008 ndipo fujo zilianza ambapo wanafunzi walianza kuimba nyimbo na kuandamana kuzunguka katika Hosteli hizo, na hatimaye walikwenda katika makazi za Mawadeni na kuyaharibu. Baada ya vurugu hizo tu maji yalianza kutoka kwa wingi sana.

B: TUKIO LA 22 FEBRUARI 2008 – MAIN CAMPUS

Tukio hilo lilianzia katika Hall 2 – Main Campus. Baada ya wanafunzi wakazi wa Hall 2 kukusanyika kusikiliza majibu ya matatizo yao ya kukosekana kwa lifti.

Kwa muda mrefu Chuo kikuu cha Dar kilitoa ahadi ya kufunga lifti na kukarabati Hall 2 kipindi cha likizo. Hata hivyo hadi chuo kinafunguliwa na hadi semesta ya pili kuanza hakuna lifti iliyokuwa imefungwa. Hivyo wanafunzi walikuwa wakipandisha maji kutoka chini hadi ghorofa ya kumi. Hali hii iliwachosha. Hadi hivi sasa lifti bado haijafungwa.

Licha ya uongozi wa Daruso kupitia kwa mwenyekiti wa Hall 2 na waziri wa Malazi kufatilia kero hiyo utawala ulibakia kutoa ahadi za matumaini kwa wakazi hao. Hivyo Daruso ilianza kuonekana kana kwamba wanashirikiana na utawala wa chuo kuwatuliza wanfunzi kwa ahadi hewa za matumaini.

Hivyo wakazi wa Hall 2 waliamua kuunda uongozi wao utakaokwenda kufatilia kero zao kwa Deputy Vice Chancellor – PFA, Porfesa Yunus Mgaya. Walimchagua mwenyekiti wao aliyeitwa Dominick Deogratius wa mwaka wa kwanza. BA Education, FASS.

Waliandika barua mbalimbali ambazo zilikuwa wakijibiwa na Profesa Yunus Mgaya.
Mnamo tarehe 22 februari 2008, ijumaa majira ya saa mbili usiku wakazi wa Hall 2 walikuwa wamekusanyika ili kusikiliza majibu ya mwenyekiti wao kutoka kwa Profesa Yunus Mgaya. Majibu hayo yalisema kuwa lifti itafungwa ndani ya wiki kumi na nne hivyo wawe watulivu.

Ahadi hiyo iliwapa furaha na kuona kuwa kumbe utawala wa Chuo ukitishiwa unatekeleza vitu ndani ya muda maalum, kwani ni siku chache ambapo wanafunzi hao waliazimia kuwa na mgomo wa kulala nje kwa muda wa siku saba.

Pia hali hiyo ilikuwa ni ushindi dhidi ya Daruso kwani wanafunzi waliweza kufanikisha na kutatua matatizo yao pasipo utawala wa serikali ya wanafunzi Daruso.

Hapo ndipo kero ya maji ilipokuwa imewajia akilini mwao, kwani kwa muda wa siku tatu mfululizo maji yalikuwa yamekatika katika Main Campus na hivyo kulikuwa kuna hali mbaya sana, harufu za vyoo zikukuwa kila mahali. Wanafunzi wa kike walisumbuka sana.

Hivyo wanafunzi walianza kuimba kuwa wanataka maji, wanataka maji huku wakipiga makofi, hali ilipelekea kupata wafuasi wengi kutoka Hall 1 na 5 kwani Chuo kizima kilikuwa hakina maji. Lengo lao lilikuwa ni moja.

Hata hivyo kulikuwa kuna sababu zingine ambazo zilisababisha na kutoa tahadhira kwa wanafunzi hao:

1. wanafunzi walijua kuwa Utawala wa Chuo unapotishiwa matatizo yao yanaisha. Walirejea siku chache ambapo wanafunzi walitishia kufunga barabara ya Mandela hadi matuta yawekwe na matuta yaliwekwa katika barabara hiyo kuingilia Hosteli za Mabibo.
2. walijua kuwa wanafunzi wa Mabibo walipogoma na kufanya vurugu sasa hivi wanapata maji mengi sana.
3. Ongezeko la ada kutoka Milioni moja hadi Milioni mbili ziliwafanya wanafunzi waaangalie huduma wanazopata na ada inayotaka kutozwa na Chuo.
4. walikuwa na nia ya kuwaiga wenzao wa Mabibo.

Hivyo vurugu zilianza ambapo hakuna mtu maalumu ambaye alikuwa akiziongoza. Wazo liliotolewa na wazo lililoafikiwa na wengi wanafunzi walilitekeleza. Viongozi wa Daruso walionekana kama wasaliti. Hivyo walibaki kwa nyuma na kujichanganya na wanafunzi. Kazi yao ilikuwa ni kuzuia maafa zaidi yasitokee.

Vurugu zilianza katika Hall2 kupitia Hall one, kisha kwenda katika makazi ya Makamu Mkuu wa Chuo, profesa Rwekaza Mkandala ndipo wanafunzi waliimba nyimbo za kumambia aache ufisadi, na wakavunja geti la makazi yake, kisha walirudi hadi UDASA baada ya kupata fununu kuwa Rwekaza yupo UDASA Club ankunywa, walifika UDASA na kuvunja geti lakini hawakumkuta. Waliondoka hadi katika ofisi za USAB Manager wakavunja vioo, kisha walielekea hadi Hall seven ambapo waliwatoa walokuwa vyumbani na kuhesabika kama wasaliti. Ilikuwa imetimia saa sita ndipo wanafunzi walitoa wazo la kwenda Swimming Pool kuoga kisha waende wakalale kwani waliamini kuwa ujumbe utatakuwa umefika. Kwani maji yalikuwa yalikuwa yamekatika.

Walipofika swmminig walisukuma geti na kufunguka, hapo ndipo mauti yalimkuta mwenyekiti wao wa Hall 2 baada ya kuruka katika kina kirefu cha Swimming Pool ila kuogelea.

TUKIO LA 11 APRILI 2008 LA UCHAGUZI.

Sababu za vurugu za tukio la tarehe 11 Aprili 2008 zilianza baada ya utawala wa chuo hicho kutoa tamko kwa wanafunzi juu ya kuhahirishwa kwa uchaguzi wa Urais wa Serikali ya wanafunzi (DARUSO) kutokana na kuwepo kwa rufaa nyingi na kujiuzulu kwa wajumbe wa Bodi ya Rufaa.

Hali hiyo ya utawala wa Chuo hicho kuingilia uhuru na demokrasia ya Serikali ya wanafunzi (DARUSO) iliamsha hasira kubwa miongoni mwa wanafunzi na hatimaye kuwafanya kukusanyika katika eneo la Revolutonary Square na baadaye katika ukumbi wa Nkrumah.vurugu hizo kama zinavyoitwa zilianza saa nne asubuhi hadi saa saba mchana.

Tarehe 11 Aprili 2008, ijumaa mgombea wa Urais ambaye inasemekana hatakiwi na utawala wa chuo hicho Bw. Odong Silas Kefa Odwar alipewa barua ya kumtaka kudhibitisha uhalali wake wa kuwepo chuoni kwa kuleta vyeti halali. Tarehe 12 Aprili 2008, jumamosi wafuasi watano wa Odong Odwar walipewa barua za kusimamishwa masomo

HALI HALISI:

wengi wa wanafunzi waliosimamishwa na wale wanaokisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya upinzania hasa Cahdema, na huwa hawana woga katika kutetea maslahi ya wanafunzi wa Chuo hicho.

Ni wazi kuwa Odong Odwar ambaye ni mgombea wa Urais hatakiwi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na anakubalika kwa kuwa na msimamo wa kutetea wanafunzi.

Makamu mkuu wa Chuo Profesa Rwekaza mkandala anafanya kila awezalo kuua demokrasia na uhuru wa kusema. Baada ya Waziri mkuu kuongea kwa uwazi katika Channel Ten tarehe 14 Aprili 2008 kwenye kipindi cha Jenerali Ulimwengu, siku ya Jumatano tarehe 16 Aprili 2008 alisimamishwa masomo na kuunganishwa katika watu kumi na sita waliofanya vurugu za tarehe 17 na 22 februari 2008.

Pia, anajaribu kudanganya umma kwa kuunganisha watu aliowasimamisha kwa kutetea maslahi ya wanafunzi na kuwaunganisha na watu 5 waliokamatwa wanavuta bangi ambao tayari polisi walishasema hawana hatia, pia hawakupewa barua ya kusimamishwa masomo, ili kuwafanya wale waliosimamishwa kwa kutetea maslahi ya wanafunzi waonekane kama wahalifu, wavuta bangi, n.k mbele ya macho ya wanajamii.

Ni wazi kuwa Chuo kilishindwa kutatua matatizo ya wanafunzi kwa wakati mwafaka. Wanafunzi hao wamekuwa wakiishi katika matatizo hayo kwa muda mrefu hadi hivi sasa. Wakati wanafunzi hao wakiona na kushuhudia nchi ikitafunwa na mafisadi wao wanazidi kutaabika na matatizo yanayowapata wanafunzi hao.

Chuo kikuu kinapaswa kuwa kielelezo cha demokrasia ya kweli na siyo kuingilia uchaguzi wa ndani wa Serikali za wanafunzi kwani ni kitendo cha aibu. Wakati vyuo kama Harvard, Capetown zinajenga demokrasia ya kweli Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaharibu demokrasia na uhuru wa kweli miongoni mwa umma wa wanafunzi.

Pia ijulikane kuwa Kamati ya uchunguzi ilianza kupoteza mwelekeo wake baada ya kuanza kulalamikiwa na wanafunzi kuwa kamati haikuwa huru na wazi kwa mwanafunzi yoyote aliyekuwa na mapendekezo ya kujenga, pia maswali yaliyokuwa wanafunzi yalikuwa ni katika kujua vyama vyao vya kisiasa badala ya maswali ya kuulizwa maswali ya msingi. Pia kamati haikuwa na uwakilishi wa Serikali ya wanafunzi DARUSO.
NINI KIFANYIKE?

1. Utawala wa Chuo hicho kiwarudishe mara moja wanafunzi hao waendelee na masomo na hawapaswi kupelekwa mahakamani. Kwani ni wazi wanahukumiwa kwa kosa ambalo kiini chake ni Utawala wa Chuo.

2. Vilevile kuwasimamisha wanafunzi hao siyo suluhisho la kutatua matatizo, bali yale yote yaliyokuwa madai ya wanafunzi yanapaswa yatatuliwe kwanza.

3. Ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ni vyema ikawekwa wazi kwa umma wote wa watanzania na wanafunzi kwa ujumla waweze kufahamu ripoti hiyo imetoa mapendekezo gani, kwani ni wazi kuwa kamati hiyo ilitumia pesa za walipa kodi wa watanzania. Hivyo ni haki ya watanzania kujua yaliyomo katika ripoti hiyo na isibaki kuwa siri kama wanavyofanya Utawala wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

4.
 
4. Serikali na uongozi wa chuo vikome kabisa kutumia FFU kupiga wanafunzi ambao hawafanyi fujo kama hawa waliokuwa wanaandamana kwa amani hapo chuoni!
 
......
Majira ya usiku ya tarehe 17 feburari 2008 ndipo fujo zilianza ambapo wanafunzi walianza kuimba nyimbo na kuandamana kuzunguka katika Hosteli hizo, na hatimaye walikwenda katika makazi za Mawadeni na kuyaharibu. Baada ya vurugu hizo tu maji yalianza kutoka kwa wingi sana.

.......ndipo wanafunzi waliimba nyimbo za kumambia aache ufisadi, na wakavunja geti la makazi yake, kisha walirudi hadi UDASA baada ya kupata fununu kuwa Rwekaza yupo UDASA Club ankunywa, walifika UDASA na kuvunja geti lakini hawakumkuta. Waliondoka hadi katika ofisi za USAB Manager wakavunja vioo, kisha walielekea hadi Hall seven ambapo waliwatoa walokuwa vyumbani na kuhesabika kama wasaliti. Ilikuwa imetimia saa sita ndipo wanafunzi walitoa wazo la kwenda Swimming Pool kuoga kisha waende wakalale kwani waliamini kuwa ujumbe utatakuwa umefika. Kwani maji yalikuwa yalikuwa yamekatika.
...........

Poleni sana kwa hayo matatizo ya kusingiziwa.
Lakini kwanini mvunje mageti na vioo n.k.??? Huoni na nyie mnakuwa VIJIFISADI vyetu? Je maji yakishatoka kwenye mabweni yenu nani ataweka hivyo VIOO na mageti mliyovunja?? Je nasie wa Kimara tukikosa maji tukavunje jengo IKULU?? Kuandamana ni haki ya kila raia, lakini si kuvunja mali ambayo si yako pekee!!
 
UDSM kuna matatizo nasio chuo makini kunahitajika mapinduzi ya kimufumo na kiutawala

Kwanza maprof feki wote wapigwe chini maamuzi ya KINAZI NAZI yaishe ,harafu waje kwenye mfumo wa elimu nao waupige chini

Harfu uone uchumi utakavyopaa
 
Paparazi:

Nimesoma maelezo yenu (sijui kama wewe ni moja ya wanafunzi au la). Na haya hapa ndio maoni yangu nikiwa pia ni mshika dau wa UDSM:

i) Ni hivi, moja ya agenda kubwa kabisa hapa JF ni kujaribu kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria na kusimika ustaraabu katika maisha ya kawaida na hasa mambo ya uongozi wa kisiasa. Sasa nyie, kupitia hili tamko lenu, mnakiri kwa kalamu na midomo yenu kuwa mlifanya fujo ikiwemo kuharibu makazi ya mawadeni wenu mnamo tarehe 17 Februari (aya ya 9 ya taarifa uliyobandika hapa). Katika aya ya 25 ya taarifa yako umeeleza tena kwamba mliendelea na vurugu "hadi katika makazi ya Makamu Mkuu wa Chuo.... na wanafunzi wakavunja geti la makazi yake".. kisha wakaendelea na vurugu hadi club maarufu ya UDASA. Sasa moja kwa moja hapa, bila kujali sababu za kufanya hizo vurugu, ni kwamba mmevunja sheria, tena pia mlikosa ustaraabu kwenda kuvunja makazi ya watu na kuwasumbua watu wengine ambao hawahusika na mambo yenu kwa njia yeyote ile. Ukumbuke kuwa huko kwenye makazi kungeweza kuwa na akina mama wajawazito, watoto wadogo, n., nyie hamkujali hayo yote.

Kwa maelezo yako, haya ningeuomba utawala wa chuo na vyombo vya usalama viharakishe uchunguzi wa kuwatambua wanafunzi wote waliohusika na unyama huu ili wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo. Hapa JF tupo serious sana na kuhakikisha kuwa utawala wa sheria unafuatwa na kudumishwa na kwamba ustaraabu unapatikana katika kila nyanja ya maisha. Tunataka tudumishe utamaduni wa kuheshima sheria kwa namna zote na kwa watu wote bila kujali hali yao maisha, wawe ni wanaume, wanawake, viongozi, wanafunzi, n.k. Tunatoa wito kwa vijana wetu waliopo vyuoni waache kujiona wao kuwa ni watu muhimu sana na wa kipekee katika jamii yetu kiasi cha kujichukulia sheria mikononi mwao. Wanaweza kugoma na kuandamana bila kuharibu mali za chuo na wananchi wengine ambazo zimepatikana kwa jasho kubwa.

ii) Tunaendelea kulaani sana kitendo cha uongozi wa chuo kuingilia uchaguzi wa wanafunzi. Tunakitaka chuo kiache kuwaona wanafunzi kama watoto wadogo kiasi cha kuwaamulia mambo yao. Tunataka serikali ya wanafunzi DARUSO iachwe iendeshe mambo yao kwa uhuru na uwajibikaji bila kuingiliwa na utawala wa chuo au ule wa serikali.

iii) Katika vyuo vingi duniani ni jambo la kawaida kwa wanafunzi kuunga mkono vyama mbalimbali vya siasa. Tumeona hata katika uchaguzi unaoendelea huko America wagombea wamekuwa wakifanya kampeni zao katika maeneo ya chuo na wanafunzi wamekuwa huru kuunga mkono mgombea yeyote wanayemtaka. Ajabu ni kwamba kwetu wanafunzi wamekuwa wakibanwa wasionyeshe mapenzi yao ya kisiasa waziwazi hasa pale wanapokuwa wanaunga mkono vyama vya upinzani. Hata hivyo,wale waoamua kuonyesha mapenzi yao kwa chama tawala huachwa wafanye hivyo bila bughudha na wakati mwingine kuwezeshwa kukamilisha mapenzi yao ya kisiasa kwa kupewa usafiri wa mabasi kwenda kuhudhuria sherehe mbalimbali mjini. Tunataka wanafunzi waachwe huru kuonyesha mapenzi yao ya kisiasa kwa vyama na wanasiasa wanaowataka. Hakuna ubaya kwa makada wa vyama mbalimbali kugombea uongozi wa DARUSO madamu wamefuata sheria na taratibu za chuo na uchaguzi huo. By the way, uongozi wa DARUSO ni fursa ya kipekee kabisa kwa vijana wetu kuweka katika vitendo nadharia za uongozi wanazosoma madarasani na kupambanua vipaji vya kiuongozi kwa wale waliojaliwa kuwa navyo.

Kwa kifupi, tunawataka wasomi wetu waliopo katika vyuo vyetu vya elimu ya juu, walimu, wanafunzi na watawala, wafuate sheria na ustaraabu wa kisomi katika kupambana na changamoto zinazowakabili.
 
Poleni sana na matatizo, pamoja na kwamba mlivunja sheria, hii ndo mifumo yetu tunayofanya kazi nayo hapa Tanzania, jitahidini kufuata sheria pamoja na kuwa haki yenu itachelewa lakini itapatina badala ya kuaribu mali na kukiingiza chuo hasara.
 
Mwl 100/100
Lakini kunakitu nataka kufahamu ,kuna wanafunzi wanashitakiwa kwa kufanya mapenzi sasa mimi nikienda kusoma pale na mke wangu harafu tukawa tunapeana mapenzi moto moto ,mabusu ni kosa kwa bylaws za udsm.
Ama wanaosoma udsm wote ni under 18 ,mimi kwa kweli hapo sijaelewa.
 
Shule kubwa sana hii Kitila.

Imebidi nisome mara mbili mbili. Ngoja emotions ziwekwe pembeni for now ili hekima itawale.
 
Kuandamana Ni Haki Pale Unaporuhusiwa Kuandamana

Wewe mtu unatia hasira lakini iko siku....................unaleta mawazo ya kijinga namna hii? Nilisikia unajita mchambuzi ndiy uchambuzi wenyewe huu ?
 
profesa rwekaza mukandala ..ndio mshauri wa jakaya kikwete ..hapo unaweza kuona aina ya mawazo ambayo yanaongoza nchi yetu!!
 
Hivi hamjui kuwa Pro. Rwekaza ni cader mzuri wa CCM, nashangaa hata alipotoa zile kura za maoni watu wanzisherekea huyu ni cader anawajibika moja kwa moja katika ibara ya 15:1, kila anachofanya lazima kiwe kwa ajiri ya manufaa ya CCM kwanza nchi baadae.
 
if ur are a critical analyst utagundua kwamba wanafunzi hawa bado hawajamtambua adui ni nani...na kiukweli hata mgomo wa sasa si wa kurudisha wenzao, bali ni kushinikiza chuo kifungwe ili wajipange upya kwa mitihani na kifedha, nina ushahidi na hili!!1
 
Hivi tumesahau yaliyotokea ufaransa miaka ya sitini? Yaliyotokea marekani miaka ya sitini na sabini dhidi ya vita vya Vietnam? Yaliyotokea Korea ya Kusini miaka ya tisini? Kabla ya kudai kuwa hawa wanafunzi wajiheshimu inabidi sisi tulio watu wazima tuonyeshe mfano kwa kuwaheshimu na kuyapa uzito unaostahili maoni yao na kero yao. Tukifanya hivyo, nao wataona hamna haja ya kufanya hizo fujo. Vitisho vya kuwasimamisha shule, kuwapeleka mahakamani na kuwaitia FFU havitasaidia kitu pasipo kuwa na heshima ya kweli. Hawa wataondoka na watakaokuja watafanya hayahaya. Solution ya matatizo yote haya iko mikononi mwa utawala na uongozi wa chuo. Washuke kutoka kwenye hizo ivory towers, wajiunge na wanafunzi wao katika mapambano ya kutafuta haki sawa kwa WOTE!
 
na kwa kuwakumbusha tu ni kuwa wazungu hawajengi mtaro, ila wanaziba pale maji yanapotoka.
kwa hiyo kuwasimamisha masomo wanafunzi au kuwaitia FFU ni sawa na kujenga mtaro.
ila kama watakaa chini na kusikiliza wanachokitaka then wakubaliane itakuwa ni sawa na kuziba maji yanapotoka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom