UDSM: Rais Magufuli kuzindua Maktaba ya kisasa,kuzungumza na Taifa

Mkuu acha Uwongo wako bhana na sijawahi kupotea hapa Jamvini JamiiForums labda Wewe ndiyo ulikuwa umepotea. Haya nakupa Masaa yangu ambayo lazima tu unipate humu na ikitokea sipo katika haya Masaa ninayokuwekea hapa basi jua kuwa nimepatwa na dharula moja kubwa ili Mimi na JamiiForums ni damu damu daima na ukitaka tugombane niambie nisiwepo hapa.

Saa 3 Kamili asubuhi hadi Saa 6 Kamili mchana ( nakuwepo JamiiForums )
Saa 8 Kamili mchana hadi Saa 10 Kamili jioni / Saa 10 Kamili jioni hadi Saa 12 Kamili jioni ( nakuwepo JamiiForums )
Saa 4 Kamili usiku hadi Saa 6 Kamili usiku / Saa 4 Kamili usiku hadi Saa 7 Kamili usiku ( nakuwepo JamiiForums )


Kila la kheri Mkuu na tupo pamoja!
Muda wote huo unakuwa JF huna kazi za kufanya?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dr. John Pombe Magufuli,kesho tarehe 27/11/2018,anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa na Kituo cha Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM.

Taarifa zilizotolewa na Mamlaka za UDSM zinadokeza kuwa Maktaba hiyo ya kisasa na Kituo cha Kichina vinavyozinduliwa kesho vipo kwenye eneo la mita za mraba 20,000. Katika Maktaba hiyo,pamoja na mambo mengine, kuna sehemu za kujisomea,sehemu za kuhifadhi vitabu,ofisi za wafanyakazi na ukumbi wa kisasa wa mihadhara na mikutano.

Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli ndiye aliyeweka jiwe la msingi katika ujenzi huo uliofanywa na Kampuni ya Kichina ya Jiangsu Jiangdu. Kupitia ufunguzi huo,Rais Magufuli anatazamiwa kuongea na Taifa kutokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anachokitaja kama akipendacho na kukiheshimu.

Hapa kazi tu!
Mkuu kwani hii habari ni ya Ki Siasa mpaka uilete kwenye hili Jukwaa ?
 
Hapana! Lazima aseme kidogo maana usikute jengo hilo limejengwa kwa bilioni 9 badala ya gharama halisi ya bilioni 2.
Nyie lumpen mliozoea kudanganywa kuwa hostel za udsm zilijengwa kwa 10 bil na mkaamini na kushangilia
 
Back
Top Bottom