UDSM: Rais Kikwete atunukiwa PhD ya heshima katika sheria

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,025
Mimi ni mmoja wa wahitimu, tuko hapa Mlimani City, kwa mujibu wa kitabu cha majina ya wahitimu ukurasa wa 74 unaonyesha kuwa JK atalamba PhD ya Heshima kwenye Sheria wakati Museveni atapata ya fasihi.

Kaazi kweli kweli
 
Kwa mbele pale yupo Utoh na Luhanjo, wamekataza kabisa watu wasiingie na camera, kuna ulinzi mkali usio wa lazima!

Nitaendelea kuwajuza muda utakapofika lakini mpaka sasa hatujaanza bado wako kwenye seherehe za miaka hamsini huko Nkrumah Hall pale Campus!
 
Ni aibu mtu katoka kuzomewa kwa kushindwa kuendesha nchi halafu mna mpa PhD ya misifa nyingine tena
 
Ni aibu mtu katoka kuzomewa kwa kushindwa kuendesha nchi halafu mna mpa PhD ya misifa nyingine tena

Kama zingekua zinasaidia katika kuendesha nchi isingekua tatizo ila sasa hazina maana yoyote na wanapeana kirahisi sana wakati watu tunasugua kichwa, naona kalazimisha apewe hio PhD baada ya UDASA kuigomea!
 
Kwa mbele pale yupo Utoh na Luhanjo, wamekataza kabisa watu wasiingie na camera, kuna ulinzi mkali usio wa lazima!

Nitaendelea kuwajuza muda utakapofika lakini mpaka sasa hatujaanza bado wako kwenye seherehe za miaka hamsini huko Nkrumah Hall pale Campus!

Endelea kutujuza mkuu na nikupongeze kwa kutunukiwa kwa juhudi zako na sio zile za "Kisogoni"
 
Shule hataki kwenda kazi kuendekeza Ufisadi, zomeazomea mwisho wake watakuja kumwagia maji ya ukoko
 
Endelea kutujuza mkuu na nikupongeza kwa kutunukiwa kwa juhudi zako na sio zile za "Kisogoni"

Asante sana Mpwa, niko na mdingi na mimaza mijitu mizima, I wish ningekuwa na damu mbichi mbichi hapa tungegoma wasimpe
 
Hongera sana mh Jakaya.
Unastahili kabisa kutokana na kazi yako nzuri unayoifanya
 
Hawa jamaa sijui vichwa vyao vina vitu gani? yaani walisema ratiba inaanza saa nane kamili hivyo tuwepo ukumbini saa hizo, sasa vitabu vya majina vinaonyesha kitu tofauti eti wanaanza saa tisa na nusu, tumekaa humu ndani kama sijui nini vile, they are so disorganized.
 
Hawa jamaa sijui vichwa vyao vina vitu gani?

Yaani walisema ratiba inaanza saa nane kamili hivyo tuwepo ukumbini saa hizo, sasa vitabu vya majina vinaonyesha kitu tofauti eti wanaanza saa tisa na nusu, tumekaa humu ndani kama sijui nini vile, they are so disorganized.

REJAO naona umeingia shift ya mchana leo! Wenzio wanaingia shift ya saa ngapi leo?
 
Ya Dr. Magufuli alikaa darasani na kuihangaikia, hivi tunaelekea wapi!?
 
REJAO naona umeingia shift ya mchana leo! Wenzio wanaingia shift ya saa ngapi leo?
Nakutafuta ulipo..kama upo ndani hapa lazima nikubebe. Huwezi kuwa unatoa habari za kipuuzi kama hizi hapa JF
 
hivi wakina shivji nao ilikuweje tena na hili li-PhD uchwara la jk?
hata sielewi,au kalazimisha afu iweje?

yani kuna malimbukeni hii nchi acha
 
Naona kama vile wanataka walete siasa tena hapa, sioni la maana, heri ningeendelea na kazi zangu nyingine! Nimesoma kwa tabu bado hata leo napo nipate tabu! Sielewi logic iko wapi! Joho peke yake nimelipa a total of 47,000Tsh.
 
Ya Dr. Magufuli alikaa darasani na kuihangaikia, hivi tunaelekea wapi!?

Kwenye kitabu kuna Jina la Eliezer Feleshi, anapata PhD ya sheria, huyu amesoma sasa sijui ndio Feleshi yule yule au labda ni majina tu!
 
Hongera sana mh Jakaya.
Unastahili kabisa kutokana na kazi yako nzuri unayoifanya

nisaidie ktk hili mkuu...
iv iz digrii ni kama nguo flan iv, unaweza vishwa na kuvuliwa au inakuwaje???
nakumbuka MUGABE kavuliwa zote na Waingereza...
 
Back
Top Bottom