UDSM ni chuo dhaifu sana Afrika "Aibu kwa nchi"

Baadhi pia ya wanafunzi wa hapo recently wamekuwa wakijilinganisha na vyuo vya ndani kama UDOM mara SAUT,badala wajilinganishe na vyuo vya nje kama Makerere,Nairobi University,Kwazulu Natal na vingine..hii inaonyesha ni jinsi gani kimeporomoka
ko hao wa UDOM Unawapeleka wapi?
Sikiliza saizi Tanzania kila kitu ni siasa.Kwa hiyo kila mahali ni Siasa.DARUSO hugusi kama sio UvFisiem.sasa tegemea anguko kubwa zaidi maana kila kitu siasa mpira siasa,uchumi siasa,utalaam siasa tegemea anguko la kila sekta.
 
Suala sio UDSM.suala ni elimu yetu kwa ujumla.elimu imeporimoka kwa spidi ya bom.inayeyuka kama barafu kwenye maji.inanuka kama kinyesi.si vyuo vikuu wala vyuo vya kati.Serikali ya Ccm msingi wake ni ukosefu wa elimu.kuna mlima mzito sana.
Mtanzania anayetaka kuimarika kielimu aenye Nairobi UN au Kenyatta.Baada ya hapo ni south africa huko ndo kuna vyuo.Ila vyuo vingine na elimu yote ya Tanzania ni sawa na karatasi kavu karibu na moto,inateketa hata kama hujaitupia ndani ya moto.
 
Na wewe unajiita msomi wa chuo kikuu? hivi uko vyuoni siku hizi mnasomea ujinga? nani alikwambia kutukudisco ndiyo ubora wa chuo? Wewe ni msomi feki na wa hovyo kupata kutokea tangu Tanganyika ipate uhuru wake 9/12/1961.
Kwa kweli. Nashukuru kusikia ukinambia ukweli ninaoufahamu..
Nipo hapa kupata degree tu.. na nikishafanya mtihani nasahau
 
Udsm zamani kidogo miaka ya 2009 ndo kilikuwa tano bora kwenye ranking ya vyuo vikuu vya kusini kwa jangwa la sahara, hapo nakumbuka ilifuata SUA 22, ikafuata Mzumbe 39 na IFM 74,

Lakin tokea 2013 nimekuwa nafuatilia index hizo udsm inacheza 27+ hivi vingine kwenye 200+
Enzi za Prof Mathew Luhanga kurudi nyuma ndio lilikuwa li chuo kweli. Baada ya hapo ikawa ni siasa akina Mukandala, Bana, Bashiru, Maganda, ...
 
Kiujumla uwekezaji katika Elimu miaka hii umepungua Sana. Sera za wizara nazo hazioneshi jitihada zozote mpya. Tumebaki kuzubaa na Elimu bure. Ni siasa juu ya siasa
 
Mayala, hivi hujui kuwa UDSM miaka ya nyuma, mara moja kiliwahi kuwa nafasi ya tatu nyuma ya University of Cape Town na University of Alexandria?

Kuna wakati nimeenda pale, sikuridhishwa kabisa na kilichokuwa kikiendelea. Ikabidi nijivute hata kuzidi uwezo wangu, ili mtoto akasome Caoe Town maana UDSM siyo niliyokuwa nikiifahamu.

Nawashauri wazazi wenzangu, ukiona uwezo unaruhusu kidogo, jaribu kutafuta vyuo vya South Africa. South Africa, wanafunzi toka nchi za SADC, ada wanalipa kama wanafunzi raia wa South Africa. Kuna unafuu mkubwa sana wa ada ukilinganisha na kumpeleka Ulaya au America.
Thanks for this information.
 
Back
Top Bottom