UDSM ndiyo chuo pekee Tanzania kati ya vyuo vikuu 50 vinavyoongoza kwa ubora Afrika

I'm very disappointed by the UDSM Management kuchapisha habari kama hiyo kwenye tovuti yao manake habari cheap kama hii walitakiwa kuwaachia watu wa mitandaoni!! Hivi wanaona fahari gani kuwa nafasi ya 42 wakati University of Nairobi wapo 13, huku Makerere wakiwa nafasi ya 14?! Hivi ni jambo la kuonea fahari hilo?! Ina maana uongozi wa UDSM unaona mshindani wao ni akina SUA, Mzumbe, na UDOM na sio hao ambao wametupiga gap la kufa mtu? Tena ikiwa UDSM Mkongwe ambae over 90% ya wafanya maamuzi wametoka hapo, wanajiona fahari ipi hata kwa Tanzania kuwa 42 huku SUA wakiwa 51?

Ukisikia siasa kwenye taasisi za elimu, ndo hii sasa!!
Wewe utakuwa mkufunzi wa chuo fulani na hapa unaonyesha chuki yako ya wazi juu ya chuo kikuu cha dar es salaam
 
Wavuti inayofanya tafiti na kutoa orodha ya vyuo vinavyoongoza kwa ubora duniani 'webometrics' imekitaja chuo kikuu cha dar es salaam 'udsm' kuwa ndio chuo pekee kutokea Tanzania kuwepo kwenye orodha ya vyuo vikuu 50 vinavyoongoza kwa ubora barani Afrika.

Kwa mujibu wa rank za vyuo vikuu iliyotolewa na wavuti ya webometrics mwezi july mwaka huu 2021, udsm kimeshika nafasi ya 42 kwa ubora barani Afrika, nafasi ya 1911 kwa ubora duniani na nafasi ya kwanza kwa ubora kati ya vyuo vikuu 51 nchini Tanzania.

Viwango vya ubora vya sasa vilivyotolewa na webometrics vinaonyesha kuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam 'udsm' kimepata maendeleo makubwa ukilinganisha na viwango vilivyotolewa mwezi january mwaka huu ambapo kilitajwa kushika nafasi ya 1971 ulimwenguni.

Aidha, webometrics imeendelea kukitaja 'udsm' kushikilia na kudumisha msimamo wake wa kuwa chuo kikuu cha kwanza kwa ubora nchini Tanzania.

Utafiti huu unapatikana katika wavuti ya webometrics kupitia kiunganishi hapa chini:

View attachment 1948231
Okay. Sisi wa SUZA tukaushe tu
 
Wewe soma ukimaliza njoo omba kazi Ndipo atasema afadhali ningekwenda VETA.
 
Leta data kuthibitisha hoja yako acha uchonganishi
Si yule Prof.Kabudi aliyewahi kusema kuwa anamshukuru Magufuli kwa kumtoa jalalani.Mtu ni Prof.anafundisha UDSM lkn anasema eti alikuwa jalalani.Mara oh!!, mhe.mungu ah!, mheshimiwa Magufuli.
 
Hilo halina ubishi, hicho ndiyo huwa selection ya kwanza kwa kila mhitimu wa A-level ila wanapokataliwa ndiyo huwa wanageuka wapinzani. Udsm ndiyo chuo bora Tanzania
Wakati namaliza A-level interest yangu ilikuwa ni kusoma Kilimo na UDSM hakukuwa na Kilimo,sasa ndoto ya kusoma UDSM ingekujaje??.
 
Back
Top Bottom