Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,284
- 4,687
Jamani kwa kweli mambo ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam UDSM yanashangaza sana.Hii ni kutokana na jinsi utawala wa chuo hicho unavyowanyanyasa wahitimu kwa mambo na sababu za kipuuzi kabisa mabzo hata mwalimu mkuu wa shule ya msingi hawezi kufikiria.Huwezi kuamini kuwa Wahitmu wa mwaka wa masomo 2006 mpaka leo hii hawajaweza kupata degree certificates zao.Sababu hata hazijulikani ni kwanini.Wengi wao waeshindwa kutokea kwenye interviews za kazi kwa vile waajiri hawaamini kuwa mtu anaweza kugraduate akakaa mwaka mzima bila kuwa na cheti cha kuonesha kuwa kahitimu kweli.Kimbembe sasa hivi wanacho wahitimu wa mwaka wa masomo 2007 hasa wa vitivo vya sheria na elimu.Kwa kawaida udsm wao wanasema degree certifictaes ni baada ya mwaka 1 kwamba zinatoka Uingereza eti kuepuka kughushiwa!Mbona vyuo vingine vyeti hiyvo hupatikana baadsa y graduation tu?kwa vile udsm hawatoi vyeti mpaka baada ya mwaka basi hutoa transcripts.cha ajabu tangu graduation mwezi november 2007 wahitimu hawana hizo transcripts.matokeo yake wengi wamekosa ajira kabisa.Mbaya zaidi hakuna anayetoa jibu sahihi lini hizo transcrots zitatoka.mdogo wangu mmoja amezungushwa mpaka karibu achanganyikiwe,ni danadana tu,kakosa kazi sehemu 3 mfululizo kwani waajiri hawataki kupokea "provisonal results",wanataka transcripts au cheti.Ukiritimba na usanii huu UDSM mnataka na/au mnawatakia nini jamani kwa wahitimu?