Udsm na mauaji ya vibaka kila kukicha........chui nae atishia maisha.au ndio matukio ya miaka 50!!!!

MASAMBI

Member
Feb 4, 2011
19
3
hapa UDSM imekuwa kawaida wanafunzi kuwaua vibaka wanaposhikwa wakiiba mali zao, mfano ni tukio la juzi ijumaa tarehe mosi julai pale hall five (5) wanafunzi walimwua kibaka licha ya juhudi za auxilliary police kutaka kumwokoa wakashindwa na nguvu na kundi la wanafunzi waliokuwa na hasira. Isitoshe wiki tatut zilizopita mauaji kama haya yalitokea pale mabibo hosteli,ilikuwa asubuhi saa tatu hivi kibaka aliingia hostel na kunyemelea wanafunzi wanapoingia bafuni au kuacha milango wazi kwa sababu yeyote ile wanaigia vyumbani na kutoka hasa katika pilikapilka za kujiandaa kutoka kuelekea katika shughuli zao. mara nyingi wanafunzi wa kike wameripotiwa kubakwa hasa wale wanaoishi mitaani; msewe, changanyikeni na golani. miongoni mwa maswali yakujiuliza ni haya:

1. usalama ndani ya chuo umezorota kiasi chuo sasa ni shamba la bibi? kila mtu anaweza kuingia na kufanya anachokitaka.mfano gari la VC kuibiwa kioo na mengineyo.
2. ama ni upungufu wa wafanyakazi (auxilliary police),vitendea kazi vichache na maslahi duni? iliwahi kusikika miongoni mwao wanashirikiana na vibaka kuwaibia wanafunzi npamoja na mali za chuo hadi wanafunzi wamekosa imani nao tena, na kilichobaki ni kuua kila wanaemkamata....JAMANI UDSM INAELEKEA WAPIIII!!!!!!!!!
3. ulinzi shirikishi kwa wasomi haujawaingia akilini au hapa UDSM si mahali pake? Mr. KOVA upoooooooooooooooo! SHERIA SI MSUMENO HAPA UDSM AU?
4. tunafundishwa haki za binadamu, wengi wetu ni wanachama wa chama cha haki za binadamu hapa chuoni, nini maana yake? thamani ya simu,laptop na chochote kile cha thamani wanafunzi wanapoibiwa ni zaidi ya thamani ya uhai? au kuua ni sasa ni sehemu ya maisha ya watanzania? Mungu epusha hiki kizazi na laana hii!!!!!!!!!!!!VC Mkandala, Mshauri wa wanafunzi, profesa Kabudi mkuu wa shule ya sheria na mlezi wa chama cha haki za binadamu(UDHRA) na timu zenu tunakosea wapi?


CHUI ALETA KIZAZAA NA SITOFAHAMU KILA KUKICHA
uongozi wa chuo ulitoa tangazo mwezi uliopita kuwa kuna chui anaonekana maeneo ya chuo hasa sehemu inayoitwa kileleni. wakasema idara ya wanyama pori wilaya ya kinondoni inafuatilia kujua ukweli wa huyo chui. wanafunzi walihoji na bado wanjiuliza maswali mengi sana..........lini tutapata ukweli? hivi chui huyu katokea wapi? aliwahi kuonekana maeneo ya jirani kama vile msewe, changanyikeni na chuo cha Ardhi au ni wa hapahapa tu? inasemekana kuna watu wamewahi kumwona lakini haiwekwi wazi kama ni kweli chui au walifananisha na paka shume?

NI HAYO TU LEO,TUJADILI!MIAKA 50 INAYOCHANGAMOTO NYINGI SANA HAPA MLIMANI. HATA ****** ANAJUA HILO JAPO HAWEZI KUKANYANGA HAPA, ATABAKI KWENDA UDOM TU.
NAWATAKIA WANAFUNZI MAANDALIZI MEMA NA KILA LA KHERI KATIKA MITIHANI YAO INAYOANZA JULAI 11,ALUTA CONTINUA
 
nimesoma weee ila nimechokea njian ntarud tena ila kama hoja ni vibaka kurestishwa in peace let them be killed pambav wamekata drisha lang wakanchomolea digital cam yangu tena nkikuta pahali anabondwa naleta wese wammalizie kbsaaa
 
kuwea ulinzi hapo UDSM ni very simple..mamlaka ya chuo haitaki
Mkuu kama tumeambiana. Siku hizi technolojia ya electrinic iko juu, wao bado wanangangania enzi za mishale na mikuki wapi na wapi. Sasa hapo mlimani si ndio kwenye wasomi wenyewe? Wanashindwa nini kuwa wabunifu.....?
 
Auxiliary hao wanajua maficho yooote ya vibaka,na kuna baadh ya vibaka hushiriliana nao......
Shame on them.......
 
ila haw wezi sometimes kunakuwa hakuna adhabu mbadala ya hiyo ya kuuawa maana wakipelekwa polisi baada ya muda wanaonekana mtaani na wanaendeleza kazi yao..
 
Hiyo ishu ya chui ni hatari kama ni kweli yupo katika mazingira hayo....
 
Mkuu kama tumeambiana. Siku hizi technolojia ya electrinic iko juu, wao bado wanangangania enzi za mishale na mikuki wapi na wapi. Sasa hapo mlimani si ndio kwenye wasomi wenyewe? Wanashindwa nini kuwa wabunifu.....?
hakuna haja ya kubuni..sosimple kununua cctv kamera na kuziweka sehemu muhimu.camera brings discipline
 
Suala la usalama nilishawah sikia chuo kina mikakat ya kujenga ukuta kuzunguka chuo, japo nna shaka sana na ujenz huo maana yaweza pita miaka mingne 50 bila ya kukamilisha huo ukuta.
 
Hiyo ishu ya chui ni hatari kama ni kweli yupo katika mazingira hayo....
ni chui kweli au duma....watu huwa wanawachanganya hawa....kama ni chui kizaa zaa chake huwa si cha kitoto
 
Kwa ufahamu wangu mdogo nilionao pale chuoni kuna ngedere wa kutosha tu. Sasa kama kuna chui tena basi si mbaya nadhani si kitambo itakuwa zoo. Hata hivyo Wanazuolojia wapo pale kazi kwao!
 
nimesoma weee ila nimechokea njian ntarud tena ila kama hoja ni vibaka kurestishwa in peace let them be killed pambav wamekata drisha lang wakanchomolea digital cam yangu tena nkikuta pahali anabondwa naleta wese wammalizie kbsaaa
ina maana digital camera yako ina thamani kuliko uhai wa mtu?
 
Back
Top Bottom