UDSM mnatia aibu, kwa elimu hii mnayoitoa hili taifa kuja kugundua hata toothpick haiwezekani..

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,520
Habari wadau..

Kiukweli nimeumia sana baada ya kuona huyu binti anavyofanya presentation kwenye seminar akiwa chuoni UDSM

Kweli lecture mzima unakubali na kumruhusu binti wa chuo kikuu ana present hivi mbele yako.. je ada anayolipa mzazi wa huyu binti anapata value for money kweli??

Zama za kulea ujinga zimeisha lazima tuambiane ukweli... mwanafunzi wa chuo kikuu cha taifa hawezi fanya presentation hivi kwa kweli... tazameni hata youtube muone wanafunzi wa vyuo vingine wanavyofanya presentation..

Baadae aki graduate msomi kama huyu anapewa kitengo sehemu na anachaguliwa kuwa mjumbe wa maongezi kwenye mazungumzo ya maana ya rasilimali za taifa na watu wa Barrick.. ( huu ni mfano)..

Ukweli chuo kikuu ndio roho ya taifa.. Lazima vitu vifanyike kwa umakini kuandaa nguvu kazi ya taifa..

Ndege, meli, umeme, computer na vitu karibu vyote duniani leo ugunduzi wake ulianzia vyuo vikuu...

Mwalimu aliesimamia hii seminar ukweli angetafutwa atujibu wazazi tunaolipa ada za watoto wetu.. kwamba haya ndio maarifa mnaowapatia watoto wetu kweli ..

Halafu wakikosa ajira mnawaambia wajiajiri.. kwa elimu ya aina hii mtu ataweza kubuni hata mradi wa maana na kujiajiri??
 
Uko sahihi mkuu hata mm nakupongeza kwa KUONA udhaifu huo, lakini sijui kama

unajuwa kuwa huyo hakuanzia chuo UDSM, kaanzia chekechea, primary, secondary

then chuo, kwa maono yako unadhani huko kote alikuwa anafanya vizuri kaja

kuharibikia UDSM???? Na UDSM wanapo dahiri mwanafunzi hawamfanyii interview bali huangalia matokeo!!!

Ebu chukuwa mda kutafakari hili nadhani utapata chanzo cha tatizo!!
 
Duh
Na akienda kufundisha sekondari ndio wanafundisha hivyo hivyo,
Aisee mabadiliko yanahitajika.
 
AAAAh this is too much ......kwa mwendo huu tutasubiri sana....graduate hawezi fanya presentation kama hiyo
 
Uko sahihi mkuu hata mm nakupongeza kwa KUONA udhaifu huo, lakini sijui kama

unajuwa kuwa huyo hakuanzia chuo UDSM, kaanzia chekechea, primary, secondary

then chuo, kwa maono yako unadhani huko kote alikuwa anafanya vizuri kaja

kuharibikia UDSM???? Na UDSM wanapo dahiri mwanafunzi hawamfanyii interview bali huangalia matokeo!!!

Ebu chukuwa mda kutafakari hili nadhani utapata chanzo cha tatizo!!
Nikadhani labda unaongelea tatizo uliloliona kwa huyo mwanafunzi ambalo liko karibu vyuo vyote hapa nchini, badala yake umetunisha misuli ya shingo kuitetea UDSM na kumshambulia mtoa mada...

Kwa hizi akili zenu nashawishika kuunga mkono elimu ya Tanzania inatakiwa kufanyiwa Reformation haraka sana..
 
Nadhani haya Maelezo umeandika bila kutafakari kwakina.Umejiuliza huyu Mwanafunzi ni Wa mwaka wangapi, na je anafanya presentation ngapi kwa week zinazomuweka fiti, na je ameshaweza kumaster the art of presentation bila kuogopa wanafunzia wenzake?? Na kuwa na hofu kwamba anachopresent kipo sahihi.

Mm sioni ajabu maana hakuna anayejua wote tunajifunza, yaweza kuwa hyo ni Mara yake ya kwanza kufanya presentation. Nasema haya maana najua presentation yangu ya kwanza mwaka Wa 1 Chuo na presentation yangu ya mwaka Wa 3 is totally different. So haijalishi unasoma Chuo gani, mwanzo ni mwanzo tu, na akiweka juhudi+experience ataimprove
 
Nikadhani labda unaongelea tatizo uliloliona kwa huyo mwanafunzi ambalo liko karibu vyuo vyote hapa nchini, badala yake umetunisha misuli ya shingo kuitetea UDSM na kumshambulia mtoa mada...

Kwa hizi akili zenu nashawishika kuunga mkono elimu ya Tanzania inatakiwa kufanyiwa Reformation haraka sana..
Labda hujanipata vzr mheshimiwa,, naungana na mtoa mada wala simpingi kila

ninajaribu kuchukuwa akili ya kawaida mfano kama huyo n mwaka wa kwanza

semister ya kwanza au ya pili, anyway hata kama mwaka wa pili it means

wamfukuze chuo kwa madhaifu hayo??? Au asipewe nafasi ya Ku present??? Au wamfanye nini ???

Ndo nikasema hivi,,tatizo sio hapo chuo maana weredi na mafunzo yote msingi wake n nguzo za nyuma alikotoka,

Maana ake kuna UTOFAUTI wa ufundishaji,,,jiulize kwa nn wengine wanaweza ??? Na wapo UDSM??

Na kuna wanafunzi pia hata huko Oxford wnazidiwa na wenzao!!!!
 
UDSM mnatia aibu, kwa elimu hii mnayoitoa hili taifa kuja kugundua hata toothpick haiwezekani.
... kiukweli nimeumia sana baada ya kuona huyu binti anavyofanya presentation kwenye seminar akiwa chuoni udsm

Tatizo unachanganya madawa, mara kutengeneza toothpicks, mara presentation! Kwanza ulitakiwa kuainisha tatizo. Halafu toothpicks hazigunduliwi upya, ni kiasi cha kuzitengeneza tu labda na kuweka ubunifu kama vile kuziwekea toothpaste kwenye ncha.

UDSM imetengeneza turbine ya kufua umeme 50 kW kwa kutumia simple materials zilizopo tu karakana, na sio prototype, ni kwamba upo mmoja unafua umeme Uganda na iliyopo inasubiri tu kupelekwa kwenye maporomoko ya maji.

Halafu wewe unakuja kuzungumzia habari za toothpicks! Uwe na desturi ya kutembelea maonyesho ya biashara, especially ya Sabasaba, utagundua mengi usiyoyajua hapa Tanzania. Mwisho, hata kama huyo binti amechemka (bado nasubiri maelezo), hawezi akawakilisha idadi kubwa ya wanafunzi na means of presentation zinazotolewa UDSM. Watu wanaofanya tafiti nadhani wananielewa vizuri zaidi (sorry sijajua level yako kama ulishafundishwa tafiti au la)
 
Nadhani haya Maelezo umeandika bila kutafakari kwakina.umejiuliza huyu Mwanafunzi ni Wa mwaka wangapi, na je anafanya presentation ngapi kwa week zinazomuweka fiti, na je ameshaweza kumaster the art of presentation bila kuogopa wanafunzia wenzake?? Na kuwa na hofu kwamba anachopresent kipo sahihi.
Mm sioni ajabu maana hakuna anayejua wote tunajifunza, yaweza kuwa hyo ni Mara yake ya kwanza kufanya presentation. Nasema haya maana najua presentation yangu ya kwanza mwaka Wa 1 Chuo na presentation yangu ya mwaka Wa 3 is totally different. So haijalishi unasoma Chuo gani, mwanzo ni mwanzo tu, na akiweka juhudi+experience ataimprove
Pamoja hoja yangu ya pili nimesema hili jambo la mwaka wa ngapi,,,,LAKINI mtoa mda hajagusia mqaka it means anaamini kila ANAEPENDA chuo anaweza kufanya presentation 100%

Sio kweli!!!
 
Sio UD tu elimu ya Tanzania ina chechemea haswa kama Bachelor holder anashindwa kujieleza kwa dakika tano kwa kingereza Huyo mtu unamuweka kundi gani?

Lugha sio kuelimika lakn umejiuliza inakuwaje mtu anatumia lugha kujifunza within 10 yrs na akashindwa kuielewa kwa ufasaha? Ndio mana baba J anawaita vilazaaa
 
Nadhani haya Maelezo umeandika bila kutafakari kwakina.umejiuliza huyu Mwanafunzi ni Wa mwaka wangapi, na je anafanya presentation ngapi kwa week zinazomuweka fiti, na je ameshaweza kumaster the art of presentation bila kuogopa wanafunzia wenzake?? Na kuwa na hofu kwamba anachopresent kipo sahihi.
Mm sioni ajabu maana hakuna anayejua wote tunajifunza, yaweza kuwa hyo ni Mara yake ya kwanza kufanya presentation. Nasema haya maana najua presentation yangu ya kwanza mwaka Wa 1 Chuo na presentation yangu ya mwaka Wa 3 is totally different. So haijalishi unasoma Chuo gani, mwanzo ni mwanzo tu, na akiweka juhudi+experience ataimprove
Good comment!
 
Hii ni kawaida mkuu kuna watu wakipresent unaweza ukadhani wanavichwa vitupu kumbe ni ma genius na wanautendaji uliotukuka lakini wamelack presentation skills tu haswaa za kingereza cha kuonges,

Kupresent ni ujuzi na wanao wachache na tatizo kwangu mimi naona limeanzia kwenye hii ishu yakushift kutoka kiswahili primary kuja kiingereza secondary inaua confidence kwa wanafunzi, that's why unakuta wanafunzi wengi waliosomea English medium schools wanauwezo mkubwa sana wakupresent japo general academic performance yao inaweza isiwe kubwa,

SHULE ZETU ZA KISWANGLISH ZIMETUFANYA UKITAKA KUONGEA KIINGEREZA UNAWAZA KWA KISWAHILI THEN UNAZUNGUMZA KWA KIINGEREZA SASA KWENYE PRESENTATION LAZIMA UWE NI MWENDO WA ACTUALLY ,, ACTUALLY,,,, MWENYE KUBISHA AKAANGALIE PRESENTATION ZA KISWAHILI WANAVYOONGEA VIZURI TENA KWA KUJIGAMBA,

Nitumia fursa hii kumpongeza mheshimiwa Raisi wetu kwa kurefrain from using English kwenye public speech. Big Up
 
Back
Top Bottom