UDSM kutumia vijana wa bodaboda na bajaj kulinda usalama wa chuo

Mwandwanga

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,059
1,568
HABARI YA MAJUKUMU WANABODI.

Dhana ya ulinzi shirikishi imeendelea kushika kasi katika jamii zetu pamoja na kuwa na msukumo mdogo au kutokuwepo au kutotambulika kisheria.
ni ukweli usio pingika kwamba usalama wa jamii ni kazi ya kila Mwanajamii lakini linapo fikia hatua ya kukabidhi jukumu hili kubwa kwa vijana wasio na mafunzo maalum inatilia shaka uwezo wa viongozi tulio wapa mamlaka ya kusimamia usalama wa raia na mali zao.

Tumeshuhudia mambo ya hovyo sana ya hawa vijana wa kuitwa ulinzi shirikishi, wamekuwa ni chanzo cha uporaji na rushwa za nguvu katika maeneo mbali mbali, wamekuwa wakitumiwa na polisi hasa hawa wa barabarani kukusanya rushwa.

Jambo la kustaabisha fedheha hii imetua CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. Siku ya leo ya tarehe 15/03/2019 askari polisi kwa kushirikiana na askari wa msaada (POLISI NA AUXILIARY POLICE) wameshirikiana kukusanya vijana wote wanaojihusisha na kufanya kazi ya kubeba na kushusha abiria katika viunga vya Chuo na kuwa amrisha kushiriki katika kulinda mazingira ya chuo.

Maadhimio yaliyofikiwa na UONGOZI WA CHUO kwa kushirikiana na POLISI ni kuanzia kesho siku ya Jumamosi vijana hawa wapewe mafunzo ya ukakamavu katika viwanja vya chuo kikuu na baadaye waanze kutumika katika kulinda mazingira ya chuo.

MAONI YANGU
Hawa vijana wapo walio jiajiri na wengine wameajiriwa, hivi wakiacha kazi zao na kuingilia jukumu hili wataweza mudu kutunza familia zao kama hapo zamani?

Ni kweli Chuo Kikuu DSM wameshindwa linda mazingira ya Chuo mpaka wameamua watumia vijana wa mtaani ilihali pale Chuo kuna AUX POLICE NA POLICE WA KAWAIDA?

Kama kuna upungufu wa askari kwanini wasiajiri badala ya kurudisha mzigo kwa wananchi/ vijana ambao watapoteza muda wa kutafuta riziki wakifanya kazi ambayo tayari kuna watu wanalipwa?
Hawa vijana wakidhurika je, chuo kitakuwa tayari kubeba dhamana ya matendo ya hawa vijana?

Prof. Anangisye litazame hili jambo kwa jicho la umakini, siamini kama Auxiliary Police na Police wa Kawaida waliopo hapo chuo hawatoshi kulinda mali za chuo mpaka muwatumie vijana wa bodaboda na bajaj.

Mwenye uelewa zaidi anisaidie!
 
naona tunarudi enzi zile za kukimbizana vijijini na maafande wakitulazimisha kufanya mafunzo ya mgambo, alafu ukikimbilia mjini unakuta maisha poa tu hakuna biashara za kucheza mgambo.
 
Hujaelewa. Hao ndo wanahusishwa na uhalifu hivyo hapo ni kumpa mchawi alee mwana ili akimroga ajue kibuyu cha dawa kipo wapi.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Ni sahihi kabisa, ukiruhusiwa kufanya biashara kweny taasisi una jukumu la kushiriki kulinda ustawi wake. Safi sana, hawawezi wasipite chuoni maana wakati mwingine wanahusika au kushirik kubeba wezi bila kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HABARI YA MAJUKUMU WANABODI.

Dhana ya ulinzi shirikishi imeendelea kushika kasi katika jamii zetu pamoja na kuwa na msukumo mdogo au kutokuwepo au kutotambulika kisheria.
ni ukweli usio pingika kwamba usalama wa jamii ni kazi ya kila Mwanajamii lakini linapo fikia hatua ya kukabidhi jukumu hili kubwa kwa vijana wasio na mafunzo maalum inatilia shaka uwezo wa viongozi tulio wapa mamlaka ya kusimamia usalama wa raia na mali zao.

Tumeshuhudia mambo ya hovyo sana ya hawa vijana wa kuitwa ulinzi shirikishi, wamekuwa ni chanzo cha uporaji na rushwa za nguvu katika maeneo mbali mbali, wamekuwa wakitumiwa na polisi hasa hawa wa barabarani kukusanya rushwa.

Jambo la kustaabisha fedheha hii imetua CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. Siku ya leo ya tarehe 15/03/2019 askari polisi kwa kushirikiana na askari wa msaada (POLISI NA AUXILIARY POLICE) wameshirikiana kukusanya vijana wote wanaojihusisha na kufanya kazi ya kubeba na kushusha abiria katika viunga vya Chuo na kuwa amrisha kushiriki katika kulinda mazingira ya chuo.

Maadhimio yaliyofikiwa na UONGOZI WA CHUO kwa kushirikiana na POLISI ni kuanzia kesho siku ya Jumamosi vijana hawa wapewe mafunzo ya ukakamavu katika viwanja vya chuo kikuu na baadaye waanze kutumika katika kulinda mazingira ya chuo.

MAONI YANGU
Hawa vijana wapo walio jiajiri na wengine wameajiriwa, hivi wakiacha kazi zao na kuingilia jukumu hili wataweza mudu kutunza familia zao kama hapo zamani?

Ni kweli Chuo Kikuu DSM wameshindwa linda mazingira ya Chuo mpaka wameamua watumia vijana wa mtaani ilihali pale Chuo kuna AUX POLICE NA POLICE WA KAWAIDA?

Kama kuna upungufu wa askari kwanini wasiajiri badala ya kurudisha mzigo kwa wananchi/ vijana ambao watapoteza muda wa kutafuta riziki wakifanya kazi ambayo tayari kuna watu wanalipwa?
Hawa vijana wakidhurika je, chuo kitakuwa tayari kubeba dhamana ya matendo ya hawa vijana?

Prof. Anangisye litazame hili jambo kwa jicho la umakini, siamini kama Auxiliary Police na Police wa Kawaida waliopo hapo chuo hawatoshi kulinda mali za chuo mpaka muwatumie vijana wa bodaboda na bajaj.

Mwenye uelewa zaidi anisaidie!
Huo ni mpango wa kupiga.
Zitaletwa kipikipi za kijani tupu na sare zake mpaka viatu! Madeini bongoland!
Na usisahau posho za mafuta ya kipikipi, lanchi, nk! Hakatwi mtu!
 
Hakuna hata senti watakayo pewa, maana wamejaribu ulizia hili wameambiwa wanao dhani hawawezi fanya kazi hii ya kujitolea hawata ruhusiwa kupita chuo kikuu na pikipiki zao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa hapa umeeleweka,utulie sasa watu wakuelewe sio waelewe ulivyoelewa wewe.

Hao vijana watafanya ubodaboda wao sanjari na kuchukua hatua kuzuia uharifu.

Wewe kwa akili yako ya kawaida unaweza mzuia mtu asifanye kazi inayomuingizia kipato,umpe kazi nyingine asiyoingiza kitu kilazima kwenye inchi huru!!!!??
 
Kuna barabara mbili ambazo kwa uelewa wangu ni 'public '.Kuelekea Msewe na Ch' keni kutokea Ubungo au Savei. Sasa Chuo kinapozungumzia ulinzi wa 'viunga' vyake ni pamoja na hizo barabara?Au ndio sababu wanakagua hata 'guta "yenye shehena ya mazao kutoka Mabibo sokoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sahihi kabisa, ukiruhusiwa kufanya biashara kweny taasisi una jukumu la kushiriki kulinda ustawi wake. Safi sana, hawawezi wasipite chuoni maana wakati mwingine wanahusika au kushirik kubeba wezi bila kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo na Madereva wa Daladala na Makondakta wao wanatakiwa kushiriki zoezi hili kwakuwa gari zao zinapita chuo?

Vipi wenye migahawa, na vibanda vya M-Pesa na Tigo Pesa kwenye viunga vya Chuo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom