UDSM inatumia vigezo gani kuwatunuku viongozi wetu PHD za heshima! au ni KUJIPENDEKEZA!!!!

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
UDSM ni chuo chenye heshima ndani na nje ya nchi. Wanasiasa na wataalam wengi ndani na nje nchi wametokea hapo. kwahiyo chuo kama hiki kinapotaka kutoa tuzo za heshima kwa mtu yoyote ni lazima kuwe na misingi na vigezo vya kutosha kufanya hivyo ili kisipoteze heshima yake ndani na nje ya nchi.

Tunasikia UDSM inataka kumtunuku JK PHD ya heshima, imetumia vigezo gani kutaka kufanya hivyo!, Au ni kujipendekeza tu kwa huyu kiongozi! na kujaribu kuficha mabaya yake.

Wapo viongozi wengi hapa nchini ambao ni wazalendo na wanapigana kila siku, hawalali, pamoja na kufichua maovu mengi katika kujaribu kuokoa maisha ya mtanzania hasa wa hali ya chini. na hawa viongozi wanajulikana ndani na nje ya nchi (mnaweza kusaidia kuwataja). kwanini viongozi hawa wasipewe hizo tuzo za heshima!!. na hapa ndio napata wasiwasi kwamba huku ni kujipendekeza kwa UDSM kwa Rais huyo ambaye ameshapoteza mvuto machoni mwa watanzania. UDSM inatuambia nini kwa hili!.
 
Nsabhi

JF-Expert Member
Feb 23, 2011
1,093
161

Ni kweli Mkuu. Udsm iachane kabisa na mpango wa kumpa tuzo mtu ambaye ameshindwa kutatua matatizo ya msingi yanayowasumbua Watanzania kwa sasa. UDSM ikianza kufanya hivyo itapunguza credibity yake.
 
twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,786
Kama amepoteza mvuto kwani tunataka kumuoza?.mbona mnawivu za ajabu?,angepoteza mvuto Igunga wakachagua chama chake?.Kwa mtu asiye kipofu ameyaona mapinduzi ya elimu yaliyofanywa na JK.Upanuzi wa shule ya elimu na sekondari.Leo hi kila kata kuna sekondari huku vyuo vikuu vikiögezeka.Kajenga UDOM au hamkijui chuo hiki?,najua kuna watu hapa watakurupuka kama wamemwagiwa uji wa moto kwa kuorodhesha changamoto za haya nilioyataja hivyo kujenga hoja feki ati hajafanya kitu.Prof. Mukandara usirudi nyuma ktk hili mmpe PHD yake anastahili wakupasuka na apasuke.
 
Kama kweli upo makini ndugu yangu huwezi kuisifia CCM kwa ushindi wa Igunga. Pamoja na michakachuo mliyoifanya Igunga bado ni aibu kubwa sana kwa CCM kushinda kwa 48% wakati ni juzi tu hata mwaka hujaisha mlishinda jimbo hilo hilo kwa zaidi ya 70%. Aibu!!!

Kwenye elimu hakuna kitu amefanya zaidi ya kuturudisha nyuma kielimu, tangu aingie madarakani vyuo vyetu vya elimu ya juu vimekuwa vikishuka kiwango barani Africa, mfano ni juzi tu UDSM ilikuwa ya 13 kwa ubora barani Africa, leo hii ni cha zaidi ya 30 na bado kinaporomoka, ni lipi amefanya kurudisha au kuongeza heshima ya hichi chuo tangu aingie madarakani pamoja na wabunge wengi kuongelea sana bungeni. kifupi ni hakuna. Elimu sio majengo, na hata hiyo UDOM kama hatakuwa makini itabaki kuwa museum.

Kimsingi nadhani wewe ndio umekurupuka kuandika hayo kama vile umemwagiwa tindikali, bora hata ungekuwa huo uji wa moto.
 
mtalae72

Member
Feb 4, 2011
92
23
Well, huyo mkuu wa chuo Rwekaza Mukandala ni mshikaji wake wa siku nyingi. Walisoma BA hapo chuo pamoja JK akisoma Economics na RM alikuwa Political Science. Hivyo ni ushikaji unaendelea ndiyo maana akamrushia ukuu wa chuo na REDET iliyoanzishwa na Mukandala imekuwa ikimpigia debe kila kukicha...Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba Mukandala ndiye aliyempa kauli mbiu ya ARI MPYA KASI MPYA NA NGUVU MPYA mwaka wa 2005 alipokuwa anautafuta urais kwa mara ya kwanza. These are politics and honorary PhDs of connection in the era of networking. Gangsters on the move!!!
 
Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
191
Kama amepoteza mvuto kwani tunataka kumuoza?.mbona mnawivu za ajabu?,angepoteza mvuto Igunga wakachagua chama chake?.Kwa mtu asiye kipofu ameyaona mapinduzi ya elimu yaliyofanywa na JK.Upanuzi wa shule ya elimu na sekondari.Leo hi kila kata kuna sekondari huku vyuo vikuu vikiögezeka.Kajenga UDOM au hamkijui chuo hiki?,najua kuna watu hapa watakurupuka kama wamemwagiwa uji wa moto kwa kuorodhesha changamoto za haya nilioyataja hivyo kujenga hoja feki ati hajafanya kitu.Prof. Mukandara usirudi nyuma ktk hili mmpe PHD yake anastahili wakupasuka na apasuke.

wakimpa PHD sawa lakin PhD hatutakubali.
 
Moses msisia

Member
May 3, 2011
57
9
Kama amepoteza mvuto kwani tunataka kumuoza?.mbona mnawivu za ajabu?,angepoteza mvuto Igunga wakachagua chama chake?.Kwa mtu asiye kipofu ameyaona mapinduzi ya elimu yaliyofanywa na JK.Upanuzi wa shule ya elimu na sekondari.Leo hi kila kata kuna sekondari huku vyuo vikuu vikiögezeka.Kajenga UDOM au hamkijui chuo hiki?,najua kuna watu hapa watakurupuka kama wamemwagiwa uji wa moto kwa kuorodhesha changamoto za haya nilioyataja hivyo kujenga hoja feki ati hajafanya kitu.Prof. Mukandara usirudi nyuma ktk hili mmpe PHD yake anastahili wakupasuka na apasuke.

jk sio jembe .kwanza akipewa phd ndio ataongeza ufanisi wa kazi? Aende huko na ushamba wake.
 
Alwatan

JF-Expert Member
May 19, 2009
409
126
Hivi JK kaiomba hiyo PhD au watu wenyewe wanajipendekeza kumpa?... Maana nashangaa kuona tangia juzi watu povu linawatoka hapa jamvini.
 
Kolero

JF-Expert Member
Apr 11, 2010
492
121
Wakati umefika sasa kwa vyuo vyetu kutojishusha na kuwashusha waliopata PhD za ukweli katika vyuo hivyo kwa kuendekeza kutoa PhD za heshima. Heshima tunaihitaji lakini si PhD za heshima bali za kufanyia kazi za kitaaluma.
 
jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Huyu jamaa kweli kakurupuka halafu hajui kama kakurupupuka na si tu kukurupuka lakini pia hajui kama hajui,hivi kweli unaweza ukazungumzia maendeleo ya elimu Tanzania?ETI kajenga UDOM,kajenga sekondari kila kata kuna sekondari,halafu,what next!hii ni njaa na kutokujua kwamba hujui,kiwango cha elimu hakipimwi kwa majengo hili lazima ukubaliane,hakuna elimu hapa wala majengo nayo hakuna,hivi huna habari majengo ya UDOM yalikuwa yanavuja miezi kadhaa iliyopita na kupelekea chuo badala ya kuendeleza ujenzi kikaanza ukarabati?kichefuchefu cha shule za kata sikitaji,ubora vyuo wakuuu wameshakuambia,kiwango cha ufaulu hiki nacho sikuambia ila nakuelekeza neda kwa Dr Ndulichako hapo baraza la mitihani atakupa takwimu,kiwango cha watoto kumaliza la saba huku hawajui kusoma na kuandika nlo hukulisikia hivi juzi,
hukupata ubwabwa -magamba walikufisadi nadhani usingekurupuka na suala la Elimu,ila kama ni zawadi au Jeykeyi kaimoba ili aongeze mvuto mpeni tu ikibid kila mwaka mnatunuku kitu manachojisikia hilo wala mm sisemi kwani najua hawazi jilinganisha na Jembe.sina haja ya kulipinga hilo la kumtunuku maana ni karatasi tu hata kariakoo zipo,je kilichopo kichwani kinauzwa wapi?
Mkumbuke nyie magamba hatukubali kuilipa dowans-hiki nakupa kidokezo maana naona ulitumwa nami nakutuma ila sina mgawo wa ubwabwa na elfu ya maji,maana ndicho mnachoambulia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom