UDSM - Hill Campus nao watishia kugoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM - Hill Campus nao watishia kugoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Dec 28, 2010.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Chuo Kikuu cha Dar es salam nao karibu wataanza mgomo, kisa bodi ya mikopo kuwacheleweshea stahili zao za kujikimu chuoni. Hivi hii bodi ya mikopo nayo ni dili la wakubwa? Hivi hawaoni kama ndio chanzo cha vurugu vyuoni? Tatizo ni muundo wa bodi au watendaji, kwa nini serikali isiianglalie hii bodi jamani ili hawa wanafunzi wakae darasani kusoma? Mh Kawambwa acha siasa kwenye mambo muhimu na nyeti kama elimu, please act.
  Jihabarishe hapa chini
  UDSM watishia kugoma
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  jJK hajamaliza hata miezi 6
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Laiti serikali ingewasikiliza UDSM kuhusu uanzishwaji wa bodi ya mikopo tusingefika hapa.
  HELSB is a failure na ni chanzo cha kuporomoka elimu ya chuo Tz.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HII 'CCM MIZIMU CHAKACHUZI' HAITOKAA ITULIE MPAKA KATIBA MPYA

  CCM 'Mizimu Chakachuzi' wa uchaguzi baada ya kutimuliwa Komoro sasa inatafuna vyuo vikuu Tanzania. Baada ya kunywa damu ya wawili UDOM sasa hatujui ataelekea wapi. Wanaodhani kwamba swala hili ni la muda tuu na kwamba litajitatua tu lenyewe - what a sweet dream!!!

  Lakini bila MAOMBI YA DHATI KABISA NA KUTUBU, hata vyama vya wafanyakazi na taasisi nyinginezo nyeti nazo huenda wakasema BASI kwa dhuluma zaidi, uchakachuaji zaidi na udini zaidi nchini mwetu endapo suala nyeti la kudai KATIBA MPYA itachukuliwa mchezo na sehemu ndogo sana ya watawala kama tunavyowaona wakiichezea KARATA TATU hivi sasa
  .
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rasimu halisi juu ya uundwaji wa bodi ya mikopo ulipendekezwa wa walaji wa mwisho (yaani wanafunzi wa vyuo vikuu) kupitia kwenye umoja wa serikali zao TAHLISO.

  Rasimu hiyo aliipenda sana Waziri Mkuu wa wakati huo Mhe Fredrick Sumaye. Rasimu hiyo ilipelekwa na watu ambao sasa hivi baadhi yao ni wabunge, madokta tena huko huko vyuo vikuu lakini ni wazi HELB ilitia kapuni rasimu hiyo.

  Prof Masenge alikua mgeni rasmi kwenye uundwaji wake kitaifa. Lakini ndio hivyo, mdharau mwiba tena.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hizi habaari ndio maana aliye toa hakutaka kutaja jina lake ni uongo mtupu hakuna hata tetesi ya mgomo!
  Bodi mbona imeweka hela tayari?

  Ilibidi wanafunzi wapate hela week ya 8,lakini week ya 7 saivi.

  Jumamosi (25.dec.2010) watu wenye account za nmb na nbc walipata hela zao.

  Jana (27.10.2010) watu wenye account crdb wamepata hela).nikiwemo pia

  Note:ni week ya 7 sasa na ilibidi waweke week ya 8,....hao wanao taka kugoma naona wamechoka kusoma au kitabu kimewakamata sana!
  Kuna taratibu zinazo eleweka kuahirisha mwaka wakapumzike kwanza na sio kuvuruga wengine tuna mambo ambayo inabidi tuwahi kufanya baada ya kusoma!
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red unanichanganya, uongo wa habari ni kutokuwa hata na tetesi ya mgomo au sababu ya mgomo iliyotolewa kwenye habari sio yenyewe, maana mwanzo umesema hakuna hata tetesi ya mgomo then kwenye note yako unasema wanaotaka kugoma wamechoka kusoma, which is which, hakuna mgomo au upo lakini sababu ni watu kuchoka kusoma?Clarify please, we need to know the truth, tumechoswa na habari za migomo
   
 8. njoro

  njoro Senior Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanasubiri kugoma kwa ajili ya hela,mambo mengine wala hayana msingi,kwi kwi kwi...duh wasomi wetu kazi kweli kweli.
   
 9. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Nasikia wale wanaoanzisha migomo huwa kitabu kimepiga chenga kwa hivyo ikifika karibu na mitihani ndiyo huchanganya kabisa. Njia rahisi ni kuanzisha migomo ili kupata afuweni.
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni tetesi hakuna,na kama zipo (na sija zisikia) basi sio kwa sababu ya hela!
  Kama ni sababu nyingine (ikiwamo kukamatwa na kitabu) wafuate utaratibu wa kuahirisha mwaka
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  OK Nimekupata mkuu
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kinyesi!
   
Loading...