UDSM hii mmewakatisha na kupunguza ari ya kufanya kazi kwa hao vijana wenu

ProtonH

Member
Jul 12, 2020
7
45
UDSM mlitangaza nafasi kwa watumishi wa umma kuhamia, na katika tangazo lenu mliweka mpaka scale za mishahara kwa ambao watafanikiwa kupata nafasi hizo.

Mdogo wangu ni mmoja wa watu waliofanikiwa kuomba nafasi hizo na kufanikiwa kupata! ana siku kadhaa sasa toka ameanza kazi hapo. Kilichoniumiza ni kumpa mkataba wenye kiwango tofauti na salary scale mliyoweka katika tangazo lenu, tena kwa tofauti kubwa sana.

Mdogo wangu amekuwa disapointed sana, kwakuwa anenda kufanya kazi na watu kwenye ofisi ambayo watu wa level yake na kada yake wanalipwa mshahara wa juu zaidi karibu mara mbili!!

Japo ni kijana ambaye hana cha kufanya lakini sisi ndugu zake tumeumia,ni bora mngewaambia hao vijana na sio kuwasainisha tu kisa hawana pa kusemea!! hili halikubaliki kibinadamu! watu waliomba kuhamia kwa vigezo mlivyoweka, kwanini mbadilike wakati tayari wameshapewa barua kutoka katibu mkuu utumishi?

Ni bora msingeweka salary scale, ili basi mtu ahamie kwa risk yake mwenyewe!

Sasa ivi mdogo wangu ni kama amekosa muelekeo wa hatma yake! hili jambo limeniumiza sana,

Kwakweli, hata hao utumishi sijajua walitoa vipi kibali cha kiruhusu nafasi za uhamisho alafu mwisho wa siku mnawageuka! Jamani hii sio sahihi, fikirieni tena kuwaweka watumishi wenye elimu ngazi moja, sifa sawa, uzoefu miaka sawa, lakini mmoja analipwa juu zaidi ya mwingine! hii sio sawa.

Utumishi wasaidieni hawa vijana walio hamia UDSM, maamuzi yenu yamemuathiri sana mdogo wangu, japo kwa maelezo yake anasema wapo wengine pia wamekutana na masaibu hayo, na hawana pa kusemea.

Naamini wenye uwezo watasaidia .
 
fox

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
301
1,000
"Mdogo wako" atakuwa ni wewe mwenyewe ila sielewi kwanini hutaki kuwa wazi.

Anyway mwambie "mdogo wako" hasiogope maisha kupanga ni kuchagua,akiona pesa ni ndogo aache kazi afanye kitu kingine.

"Mdogo wako" lazma atambue kitu kinaitwa kirithika,akiamua akubali kuanza kidogo kidogo mpk atapofika huko anakotaka.Hasiwe kama MWANANZILA akapotea mazima mazima.
 
ProtonH

Member
Jul 12, 2020
7
45
"Mdogo wako" atakuwa ni wewe mwenyewe ila sielewi kwanini hutaki kuwa wazi....

Anyway mwambie "mdogo wako" hasiogope maisha kupanga ni kuchagua,akiona pesa ni ndogo aache kazi afanye kitu kingine.

"Mdogo wako" lazma atambue kitu kinaitwa kirithika,akiamua akubali kuanza kidogo kidogo mpk atapofika huko anakotaka.Hasiwe kama MWANANZILA akapotea mazima mazima.
Me nimejiajiri mkuu, na nilisoma hapo hapo UDSM.

Ila kwenye haki na ukweli sikatazwi kuongea, nimeona namna dogo alivyoathirika kisaikolojia.
Kuwa positive Fox! watu wananyanyasika na kukosa haki zao za msingi.
 
ProtonH

Member
Jul 12, 2020
7
45
fox,
Muktadha wa ujumbe wangu umeshindwa kuujua, na sidhani kama utaujua kwa huo uelewa wako

Nadhani fox, bora ukae kimya, acha waelevu wasome ujumbe, inapowezekana watasaidiwa, ikishindikana bado kuna room kwa wahusika kuchukua hatua zaidi, kama unavyoshauri wewe!!

Pia, sio lazima kila kitu uchangie, mengine unaweza kukaa kimya!!

Tangazo lilisema wazi kuwa utalipwa kiasi flan! mtu amehangaika, leo unachukulia rahisi tu.
Basi mlipe gharama alizotumia mpaka sasa kukaa dar zaidi ya mwezi, na mengine mengi ili arudi kwa muajili wake wa zamani!

Watu kwanini hampendi watu kuonesha mapungufu ya mambo yanavyoenda katika baadhi ya ofisi za umma,

Leo amefanyiwa huyu, ipo siku atafanyiwa ndugu yako wa karibu,
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,138
2,000
Me nimejiajiri mkuu, na nilisoma hapo hapo UDSM.

Ila kwenye haki na ukweli sikatazwi kuongea, nimeona namna dogo alivyoathirika kisaikolojia.
Kuwa positive Fox! watu wananyanyasika na kukosa haki zao za msingi.
Mkuu mimi kuna kitu sijakielewa hapo,wakati anasaini huo mkataba wa kuanza kazi hapo UDSM hakuusoma na kujua maslahi yake kabla hajaanza kazi?
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,507
2,000
Hakuna kazi....... kapata kazi.... mshahara ndogo...... nanyanyaswa.... Acha kazi tafuta yako.
 
ProtonH

Member
Jul 12, 2020
7
45
Mkuu mimi kuna kitu sijakielewa hapo,wakati anasaini huo mkataba wa kuanza kazi hapo UDSM hakuusoma na kujua maslahi yake kabla hajaanza kazi?
Mkuu, kesi yao iko ivi! walitoa tangazo, mpaka grades za salary, mwisho wa siku kilichotokea ni kuwa mkataba umekuwa tofauti na namna walivyo tangaza.

Mfano, badala ya ngazi A ya mshahara kama walivyo tangaza unakuja kumpa ngaz c ambayo haikuwepo kwenye tangazo.

Hii ni sahihi? naamini watu waliomba kwa kuangalia aina ya msharaha na maisha ya dar es salaam yalivyo.
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,138
2,000
Mkuu, kesi yao iko ivi! walitoa tangazo, mpaka grades za salary, mwisho wa siku kilichotokea ni kuwa mkataba umekuwa tofauti na namna walivyo tangaza.

Mfano, badala ya ngazi A ya mshahara kama walivyo tangaza unakuja kumpa ngaz c ambayo haikuwepo kwenye tangazo.

Hii ni sahihi? naamini watu waliomba kwa kuangalia aina ya msharaha na maisha ya dar es salaam yalivyo.
Wewe jamaa kuna kitu unamess up.
Tangazo sio kitu cha kutilia maanani,tangazo linaweza kubadilishwa muda wowote watakavyo huwezi kumfunga mtu kisheria kwa ajili ya tangazo.
Ndio maana nakuuliza mkataba alipewa na akausoma vizuri kisha akasaini kwa kuelewa vizuri maslahi yaliyoandikwa?
Mkataba ndio kitu cha kuzingatia na ndio kitu muhimu hata mkienda mahakamani kitu cha kwanza kuuliza na mahakimu/mawakili ni mkataba.
Sasa sisi tunakuuliza maswali ya msingi ili tujue tunakusaidiaje wewe umeshikilia tu tangazo tangazo.
Halitakusaidia kitu hilo tangazo lako
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,379
2,000
Uhamisho aliomba au alihamishwa bila kuomba?

Alibadili kada au alihamia kada ileile?

Alienda cheo kilekile cha kwa mwajiri wa zamani au alienda cheo kipya?
 
We jamaa, hufaham maana ya tangazo? ile ni sehemu ya mkataba.
Ongea kitu kingine! nini maana ya zile condition zilizowekwa ili mtu ajitafakari na nafasi tajwa?
 
ProtonH

Member
Jul 12, 2020
7
45
Uhamisho aliomba au alihamishwa bila kuomba?

Alibadili kada au alihamia kada ileile?

Alienda cheo kilekile cha kwa mwajiri wa zamani au alienda cheo kipya?
Mbona maelezo yako wazi?
aliomba kuhama kulingana na maelezo au mahitaji ya Muajiri yaliyowekwa kwenye tangazo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom