UDSM: Hawavumi, lakini wamo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM: Hawavumi, lakini wamo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Jul 27, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Leo nimepata habari za kusikitisha. Kuna shemeji yangu, anasomea Masters yake huko UDSM, zahama anazozikabili, kwa kweli, kama angekuwa mtu mwenye "munkari" wala asingemaliza masomo yake...

  Taarifa nilizonazo ni kwamba, baada ya kumaliza Bachelors yake hapo UD alifanya kazi kama Graduate Teaching Assistant (wengine wanasema Assistant Lecturer-Trainee). Aliifanya kazi yake hiyo kwa ufanisi mkubwa, na kwa kuwa aligraduate top of his class, basi, kupata full academic scholarship (international) haikuwa ngumu sana kwake na wenzake. Siwezi kutaja yuko idara gani, kwa kuhofia yeye kufikwa na madhara ambayo yanaweza kuhatarisha mustakabali wake hapo UD.

  Kimsingi ni kwamba, masurufu yake na wenzake, shemeji yangu huyu, yanatoka nje... siwezi kutaja nchi gani pia... lakini yanapitia mkono wa UD... na kumbukeni, hapo kuna "watu". Pesa ni shetani, ukiipitishia mkononi mwa mtu itapigwa panga.... na kweli, panga linapita hapo, mpaka fungu linapowafikia wanazuoni hao, linakuwa dogo kiasi cha kukatisha tamaa.

  Wenyewe hawawezi kusema ukweli - kwa kuwa wahadhiri, wanaomega fungu hilo ndio wenye kushika mpini, wakati wanazuoni wameshika makali - kwani wakithubutu kulalamika, habari zitarudi UD, na wao watakuwa wamejiweka kwenye tafrani ya kunyimwa hata vyeti vyao, kwa kufelishwa mitihani MAKUSUDI!

  Ninachouliza, hawa wahadhiri wanataka nini? Maisha yenyewe haya ni ya shida. Wanazuoni wamesoma, kwa shida, wamefaulu, wanastahili kupewa mafungu yao kwa asilimia 100! Wahadhiri wanalipwa mishahara lukuki, lakini wana tamaa kupita kiasi. Fedha za ufadhili zinatumwa kwa matumizi ya wanazuoni, hususan wanapofanya utafiti kwa ajili ya Shahada zao za Uzamili (Masters).

  Je, hili, pamoja na lile za "maksi za chupi" yatakwisha lini?

  Jamani, huu si ufisadi huu?

  Kazi kwenu!

  ./Mwana wa Haki

  NA BADO, ntasema zaidi.... vitisho havintishi.... kwani kufa si WAJIBU tu? Niogope? Nyoooooooooooo!
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tell me about i had a friend who had a degree there, before doing another in europe even to do a research is a problem righting an essay is a nightmare i used to look at some of her essays via e-mail it was scary.

  I know they're some clever people coming out of that institution but its more to do with their natural intelligence it seems and commitment than the reputation of the uni. but my god some of the students that come out of there uhh to boost she had one degree already with her reasoning ability it questions the quality of education they offer there.
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Juma, your post should be in Kiswahili please.... tuelezane ukweli kwa Lugha ya Taifa!
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani kwani hicho kizungu chenyewe cha hivyo basi.
   
 5. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #5
  Jul 27, 2009
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiswahili mhh !!! mwanahaki usilazimishe watu wajibu kwa lugha ipi we ngine sio wazuri saana katika kiswahili ila ni wazuri katika swanglish

  nawakilisha
   
 6. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #6
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  hahaha! Swanglish?
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sawa sawa
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  MwanaHaki: sio rahisi kupindisha fedha za ufadhili wa shule kwa sababu zinakuwa clearly stated kwenye contract. Halafu huyo jamaako kama hawezi kusema ukweli atapataje haki zake? Wakati mwingine tunajinyima haki wenyewe, sasa wewe upo chuo kikuu, tena mhadhiri unaogopa kusema ukweli...grrrrrr! Yaani tupiganie haki za wananchi huko vijijini na za wasomi pia, hiyo ni shida kubwa sana.

  Hebu ni-pm details zake huyu jamaako nifuatilie, au nitumie kwenye email: kitilam@edu.udsm.ac.tz
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Hebu ni-pm details zake huyu jamaako nifuatilie, au nitumie kwenye email: kitilam@edu.udsm.ac.tz

  mnataka kula kichwa mkuu kitila???
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Mheshimiwa spika naomba sasa nieleze kisa kinacho fanana na hicho na hapa sita ficha. Pale UDSM, college of Engineering & Technology hayo yamefanyika kwa vijana waliokuwa wanasoma masters ya materilas engineering under the sponsorship of Swedish people (SIDA-Sarec).

  Kuna pia wale wamesoma masters za electrical engineering, wote pesa ilikuwa inatoka sweden ikionyesha walipwe dola 300 za marekani na hapa tunazungumza mwaka 2002 lakini walikuwa wanalipwa kiwango cha UDSM ambacho kilikuwa ni shs. 150 000/-. Ukiwauliza kwa nini wazungu wale wanapokuja mbona hamlalamiki wanasema Dr. Tesha atatumaliza.
   
 11. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  I wonder if this is really true, unless the Hill has changed overnight, even though the changing from our broken English speaking to Europian English, I still wonder how a true University graduate can fail to write an Essay???? with all those timed Essay we used to write before and in our final exams??? may be she has a fake one?? and please don't judge it by looking at only one example.
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kitila Mkumbo:

  Haya mambo mbona yapo UDSM toka enzi!! Nenda Energy Engineering Deptt. ni uozo mtupu, pesa inatoka SIDA-SAREC ikisema candidate alipwe US$ 400 per month as stippend lakini kawaulize wale vijana wanalipwa shs. ngapi?

  Ndiyo maana DAAD wao pesa wanampa mwanafunzi husika na walifanya hivyo baada ya kugundua uozo huo wa maprofesa wetu wenye njaa. Kwa hiyo bila kuficha pesa zinazotolewa na SIDA-SAREC kutoka Sweden ndo watawala wa UDSM wanazipiga panga na kuwaacha vijana wakilia njaa, kama Mkumbo unaweza fuatilia lakini najua hilo huliwezi.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sio wote wanao elewa kizungu kwa ufasaha mkuu unakuwa kama Pundit?
  Ndo nyie mkisha ishi majuu na kizungu kingi mkirudi home utakuta bibi yako unamwongelesha kizungu wkt hata Kiswahili hajui.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hapa husemi ukweli, huyo uliyekutana naye akiwa boga ni wale wachache wanapenyeza kwa ufisadi lakini UDSM will remain a model in East and Central Africa Universities. Hata ukienda Harvad nadhani lazima kaboga kamoja utakakuta tu.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unacheza na Mangi kwenye pesa tena US akichange kwenye madafu zinakuwa lukuki aisee baba angu msee anafungua bar kabisa.
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  We Fidel80 unakesi ya kujibu, kuvunja mbavu zangu asubuhi asubuhi! teh tehee..

  Ila kweli hilo la kukata kichele cha wanafunzi kwa kisingizio cha kustandardise, ili hali kwa wafadhili zinatoka kamili hiyo ipo sana!

  Njia nyingine wanayo tumia ni mfano mfadhili bajeti ipo kwa dola, kwa mfano mwanafunzi anatakiwa alipwe dola 300, lakini wakija mlipa wanampa kwa madafu na wanampa laki 3 tu. badala ya 300X1325 = 397500 (kwa sasa)! Ile change yaani 97500 wanajua wenyewe, na kumbuka hiyo ni kila mwezi na kwa maanafunzi mmoja!.. kwahiyo huo ujanja upo sana!
   
 17. L

  Lukundo Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jipiganieni na kujitoa katika utumwa wa akili na mawazo, hakuna mtu mwingine isipokuwa ninyi wenyewe mtakaojiondoa katika minyororo hiyo na kuacha uhuru wa mawazo yenu. sasa mtu yupo chuo, anashindwa kudai haki yake, tena sio kwamba anasomea kazi, bali nyongeza ya elim, kisa abaki UDSM, acheni ujinaga jamani, maisha hayapo sehem moja, msipojifunza kujitoa mhanga, mambo yenu hayawezi enda kabisa. Na hili ni tatizo kubwa la hawa tunaosema walikuwa wanafanya vizuri darasani, ndo maana hata intellectuals wetu UDSM wapo kimya wakati nchi inanyonywa.
  AIBU IWE KWENU WASOMI WA TANZANIA KWA UKIMYA NA UNAFIKI.
   
 18. E

  Evy Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i dont know if wht i heard some years back was correct or not. wht the udsm do if the funds are transfered to its accounts, they just accomodate more students to make sure more people got educated..like if the funds are 1000USD intended for 4 students @ 250 USD per person, then they add a fifth student and now they should share the same 1000USD into 200USD per person..i think its something like tht..

  its not possible 4 a lecturer or prof to steal tht money because every expenses deducted from the contract should be justifiable..

  hope tht helps..so guys dont be selfish..
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  You are talking theoretically and that is how the UDSM administration tells the donors that we are increasing the number of students with the same package, but nobody will go and count the number of students added.

  Ndugu yangu kama unasoma ripoti zilizo andaliwa na chuo au wizara umeliwa, hawasemi ukweli hata siku moja.
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Post yangu ya kwanza kujiunga JF nililalamikia upuuzi uliopo UDSM na kila mara naona watu wanakuja na mapungufu ya makusudi kabisa kutoka katika chuo hiki ikiwa ni pamoja na kiburi cha wahadhiri wakubwa kwenye vitengo vyao.
   
Loading...