Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Jamani mzee wa gumzo hapa nilipo sina amani,hali siyo shwari kabisa hapa mlimani panapojulikana kuwa kitovu cha wanazuoni (sijui kama bado ndivyo au la).Hali bado ni wasiwasi tangu jana mchana.Yaani ni vurugu mtindi mmoja.
Kama hauna habari pengine nikupashe tu kuwa jana hali ya mgomo na maandamano ambavyo vilikuwepo hapa tangu wiki iliyopita jana viliingia katika hatua mbaya baada ya askari wa kutuliza ghasia maarufu kama FFU kumwagwa chuoni wakiwa na gari lao la maji ya kuwasha na kutimuana na wanachuo wenye ghadhabu.
Jana tu wnafunzi 39 walitiwa mbaroni na askari huku polisi wawili wakijeruhiwa,mmoja kwa kupigwa na kukatwa mguu kwa chupa na mwingine akivunjika mguu.
Leo taarifa zimesambaa kuwa wanafunzi watatu wamefariki kufuatia sakata la jana.Bado mpaka sasa hivi hazijadhibitishwa ila niandikapo haya maandamano makubwa ya wasomi wa mlimani yamepamba moto.Nyimbo zinazoimbwa leo siyo zile za kimapinduzi walizozoea kama "solidarity forever" na "kama siyo nguvu zako mwalimu Nyerere...".Leo hapa kama vile kuna maombolezo.Wasomi wanaimba nyimbo tulizozoea kuzisikia msibani kama vile "Haleluya tutaonana mbinguni","nenda nenda kapumzike" n.k.
Kama hiyo haitoshi wamebeba na msalaba uliotengenezwa kwa matawi ya mti.Kama nilivyosema hali bado ni tete na sisi tulio kwenye ofisi tumefunga milango kwa hofu ya kutokea vurugu kama jana.
Hatujui mabosi wa chuo wanajipanga vipi ila wasomi wameapa kuendelea na maandamano mpaka kieleweke.
Hatuna hakika kama kweli kuna vifo vimetokea ila muda siyo muda tutajua.
Pengine umefika wakati sasa jamii tujiulize kuna nini chuo kikuu cha dar es salaam,kila semester migomo,maandamano...mjadala huooooo waungwana.
Mzee wenu sijui nitatokavipi humu ofisini leo